Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

DOA,...

>> Thursday, February 04, 2010

... ni urembo kama tu,...
.... SURA ya mrembo mwenye mwili MWEUSI TII na sura itiayo mwili DOA kwa kuwa YA MAJI YA KUNDE kwa kuwa tu mrembo KAJIPODOA.



DOA,...
.....labda ni kama katika PENZI ilivyo NDOA tu,...

....ukizingatia PENDO ni HURU na kulikosesha uhuru PENDO au PENZI ni kuliwekea mipaka hata IKIWA ni kwa kulifungia NDOA.




DOA,...
....laweza kuwa ni KITAMBULISHO katika ramani tu,...
.... na ukilitafuta katika RAMANI ya uchi wa MNYAMA waweza kuelekezwa MPAKA ni wapi kuna tundu lifanikishalo kwa WANYAMA ufanisi wa tendo la ndoa kwa kukodolea liko wapi la uchi DOA.


DOA,...
.... labda LATAFSIRIWA tu ,...
... kuwa ni DOA na sio urembo kwa ajifunzaye KUBAGUA kuwa kuna kilichotofauti kwa kuwa ni tofauti na kwa hiyo si pambo la kitambaa bali ni DOA.


Kwa hiyo DOA,...
.... kama ili yote yawe kirangi saresare maua HUINGIZWA tu,...
... basi KICHOMOLEWACHO katika uwiano wa mtazamo wa mtu ni DOA.



Na kumbuka DOA,...
...mara nyingi hulalamikiwa ZAIDI tu,...
... hasa na wasiodhurika au KUATHIRIKA na MADOA.:-(







Swali:
  • Lakini si unakumbuka DOA likiwa NA ukubwa wakutosha huwa haligunduliki au kuonekana kama doa?

  • Unafikiri BINADAMU katika sura ya dunia sio MADOA?

  • Hivi umeshawahi kumuelewesha Kipofu ni nini doa?

  • Unauhakika elimu haijatia ubinadamu wako doa?

  • Unafikiri chupi hushindwa kazi ya kulinda sehemu za siri ikiwa na madoa?


Ni wazo tu hili MKUU na NIMEACHA!:-(


Au ngojea nimuachie original shock rocker kwa jina Screamin Jay Hawkins katika kubadili hali ya hewa kijiweni hapa arudie - I Put A Spell On You





Au tu Nina Simone arudie wimbo wa Screaming Jay Hawkins wa -I put A spell on You

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 9:55 am  

na kwa kuchukulia mfano wa warembo wenye rangi ya fanta (usoni) na Coca cola (miguuni) unadhani madoa yanaweza kuficha siri ya ukiwazacho akilini? :-(

unadhani wanachokitamani ndicho doa ama wanachokiweka mwilini ndo doa? :-(

Simon Kitururu 10:08 am  

@Kadinali Chacha Ng'wanambiti:

Naamini madoa yanaweza kuficha siri ya nikiwazacho akilini kwa sababu mwenye madoa kuna wakati awazacho ni choo kiko wapi.:-(

Na nadhani wanachokitamani chaweza kuwa doa iwapo tu kitamaniwacho hakijitegemei kikishapatikana. Kama kitamanicho kinajitegemea na hakiwekwi juu yakingine basi hakuna kitiwacho doa. Au niseme kama kitu ni FIKIRA inabidi uwe na FIKIRA kwanza kabla hujaitia fikira doa. Na wanachokiweka mwilini chaweza kuitwa kujipodoa.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP