Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

JINSI ya KUJIFUNZA kukitaka kidude ULICHONACHO!

>> Tuesday, February 23, 2010

Tatizo ni:

... WATU WENGI hufikiri  ILI WAWE NA FURAHA,...
... wanahitaji WASICHONACHO,...


.. wakati WALIVYONAVYO hawana hata MUDA  WAKUVIFIKIRIA kwa kuwa WAKO BIZE wanahangaikia WASIVYONAVYO.:-(



MTU alichonacho tayari ,....
... kinaweza kirahisi kuwa NDICHO MUHIMU ZAIDI MAISHANI kuliko chochote ASICHONACHO ambacho kinamtoa raha kwa  jinsi tu ANAVYOHENYA kupigania KUKIPATA.


NA usichonacho,....
..... hicho HUNA na labda huna nafasi yakukifikiria  na kujua kitakavyokupoza ROHO ukilinganisha na AMBACHO unacho TAYARI.:-(

Swali:
  • Unafikiri umeshajifunza KUFURAHIA kikojoleo chako kabla ya KUTAKA  na kile kikojoleo  cha MWENZIO usichonacho?

  • Kwani  umeshajifunza KUHESHIMU elimu yako ya SHULE YA MSINGI ULIYONAYO TAYARI iliyokusaidia kujua kusoma na kuandika kabla ya KUJIKOSESHA FURAHA kwa kufikiria inahitajika  uende CHUO KIKUU au UWE PROFESA ili ufurahie KUELIMIKA?


KUMBUKA,...
.... kunauwezekano MKUBWA,...
.... ukijifunza KUKITAKA na KUHESHIMU ulichonacho TAYARI,...


.... unaweza kustukia WALA huhitaji cha ZAIDI kingine ili  MAMBO YAKO yawe DUKINAA,....
.... kwa kuwa kuridhika hakuna uhusiano na ni kiasi gani UMEJILUNDIKIA ndude .:-(

Swali:
  • AU?
  • Si unajua hata uelimike vipi utakufa wakati kunakitu HUJUI?
  • Unafikiri maishani mwako  UMEFANIKIWA kujifunza kuendelea   KUKITAKA ulichonacho?




...kabla sijaacha ngojea nibonge ung'eng'e kwa kudai,...
.....FIKIRIA kwa kuwa labda ;...
- ``HAPPINESS IS NOT what YOU WANT;.... its WANTING what YOU HAVE!´´.:-(


NIMEACHA!

SIKU NJEMA Mheshimiwa!


Au tu ISASHA abadili tu kabisa kwa ndude-Don't U know?



Au tu Dr Remmy arudie -NDUMILA KUWILI

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 1:20 pm  

Inahitaji uwe na mantiki ya hali ya juu kuchangia hii hoja mkuu. Bado Ninakuna kichwa

MARKUS MPANGALA 5:36 pm  

Kwa uhakika kile kidumu chama cha maasi kinaendeshwa na usukani wa profesa mwenye kidude cha karatasi kitolewacho na waandika vikaratasi vya LIJIZI.
Ndue nzuri ni ile yenye matusi na vipele vya kudondoshea kama wino ili a.k.a saa sita awe na mguno wa kujua kuwa akitakacho hakiatakiki bali alinde alichonacho.
Ndiyo hapo liprofesa lizima lenye ndude ya karatasi iliyohakikiwa kuwa nacho wakati kinakkaa kweny bahasha yenye maazimio ya wizi wa ndude ya jandoni. mmmh

o'Wambura Ng'wanambiti! 9:43 pm  

Yes! Na si ajabu kwa mtu kutafuta upendo kwa mtu ilhali upendo anao yeye mwenyewe.

Swali ni: kwa nini asijipe upendo huo ama wahenga a.k.a waswahili wanaosema 'raha ujipe mwenyewe' wanakosea? :-(

Yasinta Ngonyani 11:12 pm  

nimenukuu "HAPINESS IS NOT what YOU WANT;.... its WANTING what YOU HAVE!´´.:-("mwisho wa kunukuu:- Ni kweli kabisa.

Upepo Mwanana 11:25 pm  

Siku nyingi nilikuwa sijatembelea hapa. Mh, kuna mada nyingine Hm!
Lakini yote heri, nakusifu kwa uchambuzi wa mawazo yako.

Baraka Mfunguo 6:11 am  

Asante Mkuu kwa posti za ukweli zinazogusa.

Halil Mnzava 8:37 am  

Bro! hapo poa!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP