KUNA NYIMBO MAMILIONI za MAPENZI DUNIANI ,....
>> Sunday, February 21, 2010
....HASA ukilinganisha NA wingi wa NYIMBO ZILE za UMUHIMU wa jinsi ya KUBWIA UGORO!:-(
[Tahadhari: Taralila hii ina neno KUNYA!:-(]
Naanza;....
Kwa kuwa kuna NYIMBO MILIONI zizungumziazo MAPENZI katika kila wimbo mmoja uzungumziao KUNYA,....
... haina maana KUNYA hakuna sifa ziwezazo kutungiwa NYIMBO MILIONI katika kila wimbo mmoja UUSIKIAO wa MAPENZI.
Swali:
- Si unakumbuka watu hufikiria KWENDA kunya mara nyingi maishani kuliko wafikiriavyo MAPENZI au wampendavyo MTU?
- Unauhakika ingawa huwezi kulazimisha watu waimbe NYIMBO ZA KILIMO wakulima wenyewe UKIWAACHIA WACHAGUE unadhani watasikiliza ZAIDI nyimbo zizungumziazo KILIMO?
Ndio...
... usidanganyike na usikiacho kwa kuwa KINATAMKWA MARA NYINGI HADHARANI na kutungiwa nyimbo NYINGI ,...
... NA UKAAMINI na kufikiri HICHO ndicho chenye umuhimu zaidi kuliko vingine kwa WATU.:-(Ndio,...
... usidanganyike na USIKIACHO kwa kuwa KINATAMKWA mara nyingi na kutungiwa NYIMBO nyingi,...
.... MPAKA UKAAMINI KWA KUSAHAU kuwa usichokisikia mara nyingi kina sifa nyingi tu za kutungiwa NYIMBO MARA NYINGI kama hichohicho ukisikiacho MARA NYINGI ,na watunzi HAOHAO watu.:-(Swali;
- Si unajua unaweza kuishi bila kupendwa lakini huwezi kuishi bila KUNYA ingawa nyimbo za HAJA KUBWA huzisikii vyakutosha REDIONI?
- Katika kuangalia ni kwanini kuna aina nyingi za nyimbo zenye neno HALELUYA kuliko zenye sentensi ``kudokoa MBOGA´´ , unafikiri wewe sio usababishaye hakuna nyimbo nyingi ziongeleazo umuhimu wa kunya vizuri kwa KUWA unasikiliza KIRAHISI zaidi nyimbo za ``Mpenzi nakupenda zaidi maungo yako´´?
NIMEMALIZA.:-(
NI WAZO TU hili MKUU na unaruhusiwa kulitukania mama!:-(
JUMAPILI NJEMA MHESHIMIWA!
Au ngojea Peter Tosh akumbushie-U can't BLAME the YOUTH
Peter Tosh adai - ARISE Blackman
King YELLOWMAN anyambulishe kwa kitu- Fools go to church on Sunday
Au EEK a MOUSE abadili kwa kulainisha MSHAWASHA kwa stori ya -The man and the mouse
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Dominika njema kwako pia Mt.Simon.
Asante Dada Yasinta!
Mtakatifu Simon, kila siku unanifanya kufikiria sana hizi taralila zako. Ila nashukuru u always make my days!
Pamoja sana.
@Askofu Fadhy: Nami nashukuru tena sana kwa wewe kutochoka kunitembelea hapa Mkuu!
Tuko Pamoja Sana tu Mkuu!
Post a Comment