Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mkusanyiko wa KINACHOFIKIRIWA ambacho kwa sababu MTUZ zinajiheshimu HAKISEMWI.

>> Monday, February 15, 2010

 MKUSANYIKO wa VIFIKIRIWAVYO visivyotamkwa,....
... labda vina siri ya MATATUZI ya YADUNIA ambayo sio siri yaonekanayo hayana MTATUZI.




KINACHOFIKIRIWA  ambacho KWAKO ni chepesi kutamkwa,...
... labda sio  chepesi hivyo hata kama sio CHA KIJINGA kwa kuwa  kunauwezekano mkubwa kimepitia MCHUJO uchambuao ni YAPI MTU AYAFIKIRIAYO anataka kuyafanya  kwako iwe SIRI na aropokacho ni asilimia tu fulani la MROPOKO hata kama kwa kukuficha kitu anakucheleweshea muda wa kustukia staili ya kukaa kwako haimfai kimwana asiye vyaa kificha nyeti ambacho katika swala la kuchunguliwa ni TATUZI.




 NDIO, kwa kujiheshimu kunavisivyo tamkwa,...
.... na matokeo yake labda ufikiriavyo ni siri wala SIO SIRI na kwa kukwepa kwako kutamka neno bado sentensi uifikiriayo isiyo na heshima yajulikana na kwa ukimya  wako na ufikiriacho NI SIRI  wala tatizo lako  la kuficha siri zako HALIPO kwa kuwa HUNA SIRI na kwa hiyo  halihitajipata ulilengalo TATUZI.


Swali:
  • Unafikiri  kukwepa kwako kutamka baadhi ya maneno kwa kuwa UNAJIHESHIMU hakuchangii mkusanyiko wa SIRI MBOVU duniani?

  • Madhumuni ya kukwepa kwako kudakwa unashabikia TOPIKI FULANI HADHARANI au tu kukwepa kwako tu baadhi ya maneno -kama mtu, - unafikiri  hufanya ufikiriavyo SIRI kwa wakujuao kama mtu?

  • Ukimuona mjamzito hata bila kutamkiwa kwani hujui jina HALISI AMBALO HULITUMII  la KITENDO ambacho unafikiria  au KUHISI alifanya ingawa mwenye mimba ni  bonge la mpole?



NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA!
JUMATATU NJEMA!



Hebu Milton Nascimento arudie-Travessia



Au tu hebu Gilberto Gil alete-Toda menina baiana




Au tuondoke tu BRAZIL na kurudi BONGO NYOSO kupata dozi kutoka kwa USWAZI waongelee-True Love

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 3:14 pm  

hii kali, kwa upole woote kumbe alikuwa anahangahika na kuklalamika bila kupigwa na kulia lia, Mimba ni matokea ya mitelezo

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP