TUKIACHANA na DUNIA tuishiyo SASA ambayo WENYE NGUVU ndio walindwao na MABODIGADI !:-(
>> Tuesday, February 23, 2010
[TAHADHARI : Taralila HII imelalia mtazamo wa KIUME ZAIDI katika kugusia na kulishikashika SWALA!:-(]
Hadithi Hadithi!
Hapo zamani za kale kulikuwa na WENYE MABAVU na WANYONGE,...
...ingawa kwa kawaida ilikuwa WENYE MABAVU ndio wanalinda WANYONGE.
Na ilikuwa ni jambo la kujivunia kweli kama NJEMBA bode lako a.k.a MWILI lina mamisuli ya KIKULIMA na sio KITAMBI , kwa kuwa WEYE USIYE na KITAMBI ulijulikana unaweza kulima PUNDA KASINGIZIWA na kwa hilo tu MADEMU warembo wa kijijini walikuwa hawakawii kukuchekea KISIMANI na kukuchungulia ukienda kuoga MTONI ,wakati ndoto zote zao hata zile za wakati TU ndio wanavunjavunja UNGO zilikuwa zina DONDOO mpaka za unavyonukia vizuri KIKWAPA CHA NGUVU kwa jinsi tu ulivyo na juhudi SHAMBANI.
NGUVU ilikuwa inamaanisha NGUVU kweli na kama wewe KIDUME unalegalega a.k.a UMELEGEALEGEA , wazee wazima walihakikisha hutoki JANDONI kwa hata kudai uliliwa na simba huko; kitu ambacho Wapare walidai umemezwa na MSHITU. JANDO lilikufunza sehemu ya MWANAMKE na jinsi ya kumshungulikia apate kirahisi mbele yako kujisikia MWANAMKE.
Na hapo zamani za kale mwenye akili alikuwa ni yule ajaliye famili na jamii yake. Mwenye akili alihakikisha familia na jamii yake INAPATA MSOSI , inalindwa, ina nyumba ambayo umejenga kwa nguvu zako MWENYEWE , na angalau kila mtu aliyepita UMRI WA KUCHEZA UCHI WA KITOTO a.k.a kila aliyekaribia kuanza kuota NYWELENYWELE KUNAKO umehakikisha kavaa vazi la kisasa KIJIJINI ; ambalo la weza kuwa ni chupi ya MKEKA au tu ile CHUPI ya ngozi itokanayo na MNYAMA uliye mdaka kazubaa msituni MWENYEWE , ambaye kitoweo chake kingine bado kimekaushwa kwa moshi jikoni juu ya jiko la kuni.
Hapo zamani za kale , ukishajulikana unamiguvu ya kutosha na umetahiriwa safi au tu KUFUNDWA VIZURI kama unatoka katika jamii yenu ishabikiayo magovi, BADO NI WAZAZI ambao walihangaikia swala la kukupatia POOZEO LAKO la maisha a.k.a kukutafutia MZAZI MWENZAKO.
Na binti mzuri alikuwa SIO yule mwenye bomba la tako au tu chuchu ya kutosha , kwa kuwa ilibidi kwanza WAZAZI wafanye utafiti kuangalia MASWALA YA FAMILIA YA KIGOLI , kama yale ya UKOO wa Kimwana MNONO mlengwa KUWA hawana KIFAFA kwao , BIBI YAKE hana UKOMA au tu kama UCHAWI KWAO haupandi vizuri.
Kwa hiyo MTOTO mzuri aliyenona kabisa waliweza kumstukia DNA yake ni ya KICHAWI KABLA HUJADAKA KIMWANA , na kwa hilo ukastukia VIJANA BOMBA wanukao kikwapa cha kutosha kukuhakikishia ni wakulima safi WAMEFUNGA BREKI ZA MATAMANIO na wakawa wana Mruka KIMWANA MZURI mwenye macho ya gololi, mashavu ya KUMIMINA, tako mtikisiko ´´SINGIDA-Dodoma´´, kwa kuwa tu kwao MAMA YAKE MKUBWA anakifafa na aliwahikuzaa MAPACHA kitu ambacho kwenye MILA zenu ni NUKSI..:-(
Swali:
- SI kunauwezekano MWENYE NGUVU siku hizi siye yule alindaye wengine, ila ni YULE alindwaye aepukane na wanyonge na ASKARI?
- Si mwenye nguvu siku hizi ni yule MWENYE PESA?
- Si mwenye akili sikuhizi ni yule AJILIMBIKIZIAYE MALI wakati wengine hawana , aliaye katika ofisi ya UMMA mali za UMMA , na unaweza kumtambua KIRAHISI kwa kuwa kwa kawaida yuko katika KUNDI ambalo huitwa MHESHIMIWA?
- Si Msichana aonekanaye Mzuri siku hizi Tanzania ujazo wa TAKO kipimo chake kimepunguzwa ingawa titi saa sita bado lakubalika?
- Na si unajua kwa wadada LIMJAMAA lao WALILENGALO au WALITEGEMEALO sasa hivi kwa kuwa ni jizi kwa kukusaini tu MAKARATASI na lina MIPESA KEDEKEDE hapo zamani kuna uwezekano wangekufa -NALO kwa njaa?
- Si unakumbuka PIA hapo zamani bonge la demu lazima linuke KIKWAPA vya kutosha ili KIJIJINI NJEMBAZ na WAZAZI WENU mjue ni bonge la mfanyakazi na likiingia shambani hilo ni BONGE la TREKTA na lafaa kuwa MKE?
NDIO,...
.....HAPO ZAMANI kulikuwa na MABAYA na MAZURI kama SASA HIVI.:-(
Swali:
- Unafikiri kizazi cha SASA hivi kimejifunza ni yapi MAZURI ya zamani yafaayo kutunza na ni yapi hayafai kuyang'ang'ania kwa kuwa tu bado yana tamu zake sasa hivi kwa baadhi ya watu?
Hapo zamani,...
...... kulikuwa na TAMU zake lakini pia usisahau MABAYA kwa kuwa tu unajuakubonga UNG'ENG'E siku hizi na kamsemo ka ``OLD is GOLD ´´ umeshakakariri na KUKAAMINI kuwa NI KWELI TUPU.:-(
Hapo zamani labda UNGEKEKETWA usikiliziacho tamu wewe ,OOOHO wee SHAURI YAKO!
Hapo zamani kabla ya watu kuanza kuwa na NGUO na VIATU vya JUMAPILI au IDI ungekuwa unabonge la chupi la NGOZI au MKEKA wewe, Ohoo wee SHAURI YAKO !
....eti siku hizi linaturingia na chupi lake la GUCCI na wala sio la KITENGE.:-(
Tukiachana na mzaha,....
Swali:- Unafikiri siku hizi si WENYE MABAVU ndio walindwao na MGAMBO , POLISI , MAHAKAMA na mpaka JESHI wakati wanyonge hawana Mlinzi?
- Na siku hizi si mpaka WIZI ni shughuli ya asifiwaye kwa MIAKILI?
Na katika HITIMISHO la hii HADITHI HADITHI,...
..... napenda kukukumbusha Mheshimiwa kuwa HIVI SASA bado kuna WENYE MABAVU na WANYONGE ingwa labda kuna ukweli kuwa siku hizi mambo yote ni MNYONGE MNYONGENI na HAKI ZAKE CHUKUENI na sio MNYONGE MNYONGENI lakini HAKI zake MPENI.:-(
NI HILO TU na ni Mwisho wa HADITHI HII!
KUMBUKA TU, NI wazo tu HILI MKUU!
Hebu Ringo Madlingozi na Oliver Mtukudzi wabadili kwa kurudia kitu-Into Yami
Au tu Sipho Hotstix Mabuse arudie tu -Shikisha
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment