Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MTOTO MZURI labda JAMBA tu usiahirishe,...

>> Saturday, February 27, 2010

.... kwa kuwa  kama umewahi KUBANWA na kijambo,....
..... wajua  JUHUDI  na  JEURI za waliobanwa kijambo WASIOJAMBA HADHARANI  sana sana ni za kusogeza MUDA tu  WAKUJAMBA iliusisikie wakijamba  ,...
.... na AFYA YA KIJAMBO  CHAO kwa bahati mbaya bado huwa iko PALEPALE.:-(

Na MTOTO MZURI  labda   NI BUSARA PIA  kijambo usilazimishe,...

....kwa kuwa ALAZIMISHAYE KUJAMBA  anaweza akafanikiwa KUHARISHA PIA juu ya kijambo hasa KWA KUWA  nukta ya kutolea uharisho NI ILEILE ambayo ukizidisha JUHUDI hewa itaongezewa CHEMBECHEMBE NA ROJO  katika MTOKO  utumiao tobo   ambalo wengi hutambua kuwa  HUWA linanunia shughuli  sehemu mbali mbali lakini katika tundu lililopo  PALEPALE.:-(

Swali:
  • Unafikiri kwa kuahirisha UJUACHO utafanya WATU WENGINE wasipokuwepo kuna badili kuwa utakachofanya ni KILEKILE?

  • Unafikiri ukidokoa MBOGA bila kuonekana  kitendo chako hugeuka kuwa NI kuonja MBOGA?

NDIO,...
... moja ya BUSARA za BINADAMU ni kuficha  vitu vijulikanavyo SIO SIRI na  kuwageuza wavifanyao HADHARANI mahawayani ingawa LABDA uhawayani WENYEWE WENYE TAKO KUBWA  ni ule   UTU na HESHIMA ZA MTU   zenye misingi  ijengwayo kwa kuwa tu NI HESHIMA eti MJUACHO ANAFANYA kafanya SIRI.:-(

NIMEACHA!

Tahadhari: MHESHIMIWA  hii taralila HAINA uhusiano na KUJAMBA!:-(

Hebu tubadili wazo HASA kwa kuwa kwenye taralila isiyona uhusiano na KUJAMBA inaneno JAMBA  lisilo la HESHIMA kwa  BAADHI YA WAUNGWANA WAJAMBAO  kwa kuwaachia En Vogue wadai- My Lovin' (Never Gonna Get It)

Salt N Pepa wazungumzie - Shoop

Au tu NAUGHTY by NATURE warudie tu.- FEEL me FLOW

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 5:42 pm  

Mmmmmhhh hapa leo sisemi kitu! wikiend njema Mtakatifu!!!

Masangu Matondo Nzuzullima 7:45 pm  

"moja ya BUSARA za BINADAMU ni kuficha vitu vijulikanavyo SIO SIRI na kuwageuza wavifanyao HADHARANI mahawayani ingawa LABDA uhawayani WENYEWE WENYE TAKO KUBWA ni ule UTU na HESHIMA ZA MTU zenye misingi ijengwayo kwa kuwa tu NI HESHIMA eti MJUACHO ANAFANYA kafanya SIRI.:-("

Umesema kweli Mtakatifu. Kila mtu aliyezaliwa anajua kwamba wazazi wake walifanya lile tendo - japo kwa siri. Ndiyo maana nilicheka niliposoma dokezo lako kule kwa Yasinta kuhusu birthday za mpigo kati ya binti yake na yule wa Da Mija. Ulisema kwamba kuna kitu ambacho walikuwa wanafanya "at the same time" mpaka wakawa na watoto wenye birthday moja - kitu ambacho - japo kila mtu anajua kwamba kinafanyika, hakipaswi kutajwa wala kurejelewa!

Ati, yupi ni bora?: ng'ombe ajisaidiaye hadharani au binadamu ajifichaye japo akitoacho kina uvundo zaidi ya kile kitolewacho na ng'ombe hadharani?

Simon Kitururu 11:55 am  

@Dada Yasinta: Asante sana dada!

@Matondo:

Labda kisa kizima cha BINADAMU kujificha zaidi wakati anakunya,... zaidi ya wakati anakojoa kuelelezwako na staili za kuchimba dawa WATU WAKIWA safarini BONGO ni kutokana na hilohilo kuwa KINYESI cha binadamu hata ngombe anastukia kinanuka zaidi.:-(

Lakini nafikiri katika swala la UMUHIMU wa KUJISAIDIA ukilifikiria kiumuhimu TU , Ng'ombe na MTU wanyavyo vyote NI SAWA kiubora hasa kwakuwa VYOTE hutatua zaidi shughuli ya kuondoa makapi tu MWILINI.

Ila sitashangaa kama kuna mwanasayansi sasa hivi ambaye RESEACH YAKE ni kuangalia uwezekano wa mtu ajambe pafyumu na KINYESI kigeuke biskuti.

Si umecheki jinsi NASA walivyohakikisha mikojo inageuzwa maji ya kunywa ili kusaidia uwepo wa maji kirahisi katika SPACE STATION yao angani?

Kwa hiyo nafikiri tatizo la kutokunya sebuleni kwa BINADAMU WASTAARABU SIKU HIZI linawezekana kuwa ni la kizazi chetu tu kwa kuwa hapo baadaye ambapo ujanja itakuwa ni kwenda holiday MARS au JUPITER ,...na hasa kwa kasi ya ukuwaji wa IDADI ZA WATU WAHITAJIO CHAKULA ulivyo ,....labda watu watawezeshwa kunyeshwa malighafi tu za CHAPATI au CHAKULA tu kwa ujumla HAPO BAADAYE na mjanja atunzaye MAZINGIRA atakuwa ni yule ahakikishaye haendi hovyo msalani maporini.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP