Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Manufaa MAKUBWA ya RAIS au KIONGOZI MJINGA!

>> Thursday, February 18, 2010

 [Tahadhari: Tafakari imepinda na ni fupi a.k.a imekatiziwa denge!:-(]


Kama KIONGOZI  mjinga si mjinga vyakutosha kuharibu kabisa,......
...BASI labda ....
....KILA NCHI ili ijengwe na kuimarishwa MISINGI YAKE KIBUSARA labda inahitaji mara kwa mara kuongozwa na RAIS au Kiongozi MJINGA!


Kiongozi  MJINGA hata wa KAMATI   YA KIJIJI na SIO  NCHI  ionekanayo inahitaji KIONGOZI asiye MJINGA kama TANZANIA ana manufaa yake katika kuamusha MORI WA WANANCHI  katika kustukia NA KUHESHIMU  ni nini umuhimu wa VIONGOZI BORA wajuao wanafanyanini na si WAJINGA katika UONGOZI  WAO  ambao matunda yake ndio kielelezo bora cha ubora wao wa kutoongoza mambo KIJINGA..



Na Rais MJINGA ni msaada sana hasa akifuatiwa na RAIS MWENYE MIAKILI ya uongozi na bingwa wa  UTEKELEZAJI  kwa  BUSARA  ZAKE hasa katika kusaidia kukubalika kwake na SERA ZAKE baada ya WANAVIJIJI kuchoshwa na YALE YALE  ya danganya toto za KIJINGA..



Swali:

  • AU?
  • Unafikiri HITLER hakuwa msaada kwa KIONGOZI aliyemfuatia UJERUMANI baada ya wananchi kushtukia alichemsha?
  • Unafikiri UONGOZI wa CCM  kama UNAKOSEA sio msaada na  funzo kwa CHAMA chochote kingine kitakacho ingia MADARAKANI Tanzania baadaye?



Lakini.....

  • Hivi katika shughuli, KIONGOZI MJINGA na mtekelezaji swala na KIONGOZI MWENYE MIAKILI a.k.a SIO MJINGA  lakini PIA  si mtekelezaji unafikiri watoto watafanana na nani  kama uzalishaji watoto unahitaji MTEKELEZAJI wa shughuli?



NIMEACHA!

SAMAHANI ni wazo tu fupi hili MHESHIMIWA na ni ruksa kulipinga!

SIKU NJEMA!


Au badili kwa kupata stori ya ndoa na penzi kiduchu....



The LAST POETS warudie tena -Take Your Time



Au tu Fu-Schnickens na Shaquille O'Neal wabadili tena kwa -What's up DOC

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP