Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WALI uliokula JANA kama tu PENZI la msichana kipenzi ALIYEKUACHA JANA!:-(

>> Friday, February 19, 2010

[Tahadhari: Taralila hii inatafakari iliyopinda kidogo maeneo!:-(]







Hiii ni STORI ya WALI  ulioula JANA, uulao LEO na utakaoula KESHO.

Wali kwa mlenda ULIOULA jana  LEO ni stori TU.

Wali uulao leo ndio nguvu yako LEO .:-(

Wali utakao kula kesho NI WAKUFIKIRIKA TU  kwa kuwa unaweza kukojolewa KWA BAHATI MBAYA  na MBUZI kabla huja-UGIDA kesho.:-(





Swali:
  • AU?



Hii ni STORI ya MSICHANA KIPENZI  wako wewe MSAGAJI  aliyekuacha JANA, umfikiriaye LEO na utakaye mfikiria KESHO.

Alivyokuacha jana ,...
.....mengi utakayoyazungumzia kuhusu yeye LEO  ni ZILIPENDWA TU  za kabla ya jana na JANA.:-(

Leo kama unahamu KAMA tu VIDUME wapweke wamkumbukao KIPENZI ZILIPENDWA ALIYE WAACHA SOLEMBA JANA ,...
....KWA BAHATI MBAYA leo kilichobaki ni KUJIGALAGAZA na  kumbukumbu tu za JANA ambazo zinaudhaifu  KIMPEKECHO katika kukuna  ya LEO.:-(

Kesho,  kama hutafuti tibabu   ndani ya HIYOHIYO  KESHO,...
... na  kuachilia mbali ya JANA,....
....kwa bahati mbaya  kama hutaendelea na MAISHA yako kivyako  aliyekuacha JANA bado hatibu  NG'O mshawasha wako hasa kwakuwa HAYUPO hiyo KESHO.:-(





Swali:
  • AU?



Samahani naanza upya hiii taralila...:-(





Nachojaribu kusema ni;....

-HATA kama WALI kwa ROJO  uliula JANA,....
......kama  una njaa leo, WALI MZURI JANA ni stori tu LEO.:-(


Na hata usimulieje  jinsi ulivyowahi kufaidi sana tokea ZILIPENDWA za kabla ya JANA,....
..... kwa mwenye njaa leo bado  UJANJA ni kula LEO.:-(


Na KAMA UNAWASHWA LEO,...
.....kumbuka stori za jana za ULIVYOKUNWA mara nyingi ni za JANA ,....
.... na ni kawaida kuwa  MATIBABU ya kipele leo huhitaji KUKUNA na mkunaji kipele LEO:-(.





Swali:
  • Unafikiri simulizi za nilivyowahi faidi bonge la UKOKO mwaka jana kama NA  njaa sasa hivi inanisaidia kitu MIMI sasa hivi katika kutibu njaa?
  • Unafikiri  simulizi  ZANGU  za nilivyofaidi bonge la UKOKO na UTANDU kwa mbali lililomwagiwa ROJO TAMU bila kusahau CHACHANDU na KACHUMBARI pembeni    mwaka juzi , ambazo hazinipozi  NJAA leo mie mwenye njaa leo hazikufunzi kitu  tu weye LEO ambaye huna njaa,  .... kuhusu ya KESHO?





LABDA niseme:

Tunza cha leo, ....
... JANA na ya jana YAMEPITA  na kwa leo  YA JANA kwa zaidi ni STORI tu LEO.:-(

.
NA ya KESHO,....
.....kama wewe ni BINADAMU ,....
....BASI hayo bado ni ya kufikirika TU.:-(





Swali:

  • AU?





Lakini pia,...
.... kumbuka tu kuwa PAMOJA na ALIYEKUACHA JANA  kukuacha  na hahusiki katika TATUZI lako la  hamu yako ya kusikia tamu LEO,....

..... usisahau lakini kuwa YA JANA BADO NI SHULE,....


...na staili ya ulivyong'ata kidude au SENENE  jana yaweza kuwa  FUNDISHO , na inafundisho katika staili yako ya kulamba KIDUDE  au kugida tu  KUMBIKUMBI kesho katika ukabilivyo vyenye uwiano na kilichobakia kuwa ni ZILIPENDWA MUKICHWA ,....

.....kwa kuwa KWA LEO hata ufanyeje bado KILIFANYIKA , kilionjwa au tu kilikuwa chako JANA hata ya dakika tano zilizopita na ndio IMETOKA HIYO!:-(




Kumbuka tu  pia ,....
.... pamoja na YOTE ,....
..... wali uliokula  jana huwa ndio uumpao MTU NGUVU ya kuweza kukata tonge LEO.:-(




NIMEACHA!

NI Tafakari tu  HII MHISHIMIWA Bwana MKUBWA jaribu hilo KUKUMBUKA !

IJUMAA na WIKIENDI NJEMA MKUU!




Hebu TPok JAZZ wajaribu kutusaidia kubadili hali ya hewa kijiweni kwa kitu- MAMOU




Au tu Kassav warudie tena -Zouk La Ce Sel Medicament Nou Ni

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 8:47 am  

Mtakatifu Simon,
Ni tafakuri nzuri sana kwa leo.
Wacha nami nifikirie zaidi ya lleo maana ya jana zilipendwa.

Mija Shija Sayi 12:14 pm  

Asante kwa busara Kitururu.

chib 5:00 pm  

Haya mkuu, umeniacha na tafakari kubwa ya wikendi.

EDNA 1:19 pm  

Mtakatifu unaniacha hoi na kiswahili chako, maana ili nielewe unachomaanisha huwa inanibidi nisome zaidi ya mara 3, kweli wewe ni Mtatifu wa watakatifu....otherwise asante kwa shule ya bure unayotupa.

Simon Kitururu 7:49 am  

@Wote: Asanteni WOTE!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP