Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KWA kuwa njia NZURI ya KUTUNZA AHADI hata kwa MPENZI ni kutoahidi!

>> Sunday, February 21, 2010

AHADI ni faraja ya KITU kwa muda mfupi,....
.... kwa kuwa hata UKITIMIZA  ahadi  LEO hata bila KUDENGUA  ,.....
.... huo ni mwanzo TU  wa kumuandaa mtu ULIYEMTIMIZIA AHADI kukaa mkao wa kuhitaji  AHADI mpya UPYA .:-(






Swali:
  • AU?
  • Kwani ulichoahidiwa kikitimizwa UNADHANI HUO ndio mwisho wako wa KUTAKA  kuahidiwa TENA kidude?



AHADI mpya ni tamu KWELI,...
.....kwa kuwa inatia faraja UPYA!

AHADI hujenga tegemeo la kuwa ingawa sasa hivi huna KIDUDE ,....
... ni muda tu kidogo ambao ndio tatizo kwa kuwa utakacho utakipata  BAADA YA MUDA kwa kuwa UMEAHIDIWA tayari KIDUDE.



Swali:

  • AU?


NA AHADI  ni tamu tu wakati IMEAHIDIWA,.....
.... kwa kuwa utamu wa AHADI ni AHADI yenyewe ,....

...... hasa KWA SABABU  ulichoahidi UKIKITIMIZA HUGEUKA KWA KUTIMIZWA  na kuwa  sio  AHADI  TENA ,...
...na KWA HILO  ladha yake ni tofauti na AHADI ndio maana   bado kuna WADAIO walinogewa na KILICHOAHIDIWA zaidi ya AHADI .:-(


NDIO,...
.....uhakika wa ladha ya AHADI uko  zaidi  katika AHADI tu na sio KILICHOAHIDIWA ,.....
..... kwa kuwa KITU ulichoahidiwa  CHENYEWE ,....


.... kinaweza kuwa KINANUKA uvundo wa MKOJO  au tu KIMEZIDI SUKARI kuliko ulivyoahidiwa na uifikiriavyo AHADI.:-(


Swali:
  • Unafikiri AHADI ya BUSU a.k.a kula denda ina utamu kama kula mate  a.k.a KULA DENDA?

  • Si unakumbuka utamu wa KUHISI UNAPENDWA ni tofauti na kitendo cha KUPENDWA CHENYEWE ndio maana  uhisiye anakupenda wakati anakupa KIDUDE    ili akuaambukize GONO  na MDUDU  unaweza kumpenda zaidi kuliko AKUPENDAYE na kukunyima KIDUDE kwa kukujali  ili asikuambukize HERPES au tu FUNGUS ya kunako hata kabla hana GONO na MDUDU?

NDIO,....
.... KUAHIDI ni kujenga misingi ya KUVUNJA ahadi ,....
.....kwa kuwa KUAHIDI ni mimba ya MATEGEMEO ya ALIYEAHIDIWA ,....
.... na kitegemewacho KWA KUWA NI AHADI  ndicho  chenye  misingi ya MAUMIVU yatakayopewa MOTISHA au  kuvunjwa kwa AHADI hasa kwa kuwa wewe NI BINADAMU na hakuna BINADAMU mwenye uhakika na BAADAYE kiasi cha kuwa na uhakika asilimia MIA atatimiza AHADI.:-(


Na KWA BAHATI MBAYA  kama HUJAAHIDI ,...
.... MKUU kumbuka kuwa haina maana kuwa,...
... HAKUNA MTU aaminiye weye huna AHADI ya KUVUNJA kwake .:-(


Swali:

  • Si unajua kuna watu hata  MSICHANA AKIOLEWA TU ni kama vile KAWAAHIDI na  kahakikishia ukoo kuwa atapata mimba hivi karibuni kwa hiyo ni wakati wakumuangalia ujazo wa tumbo au tu katika mwendo anatikisaje matako , LA SIVYO itabidi  kumuuliza MUME wake kuwa nini kinaendelea mbona KIMWANA HAJISIKII KICHEFUCHEFU ,kitambi hakikui, hali udongo, habanwi haja ndogo mara kwa mara au tu hatema mate ovyo?

  • Si unajua PIA kumchekeachekea mtu ingawa ni kwa kuwa NI  mcheshi  TU kunaweza kumfanya MHESHIMIWA  ACHEKEWAYE afikiri akitongoza atapewa kwa kuwa kicheko chako kimetafsiriwa ni KUJIGONGA na unaahadi kukubali?

Tahadhari,...
....tafsiri za AHADI ziko nyingi kwa wengi na wala HIZO TAFSIRI hazitokani na  sentensi - `` NA AHIDI´´.:-(






Lakini ,....
.....KUMBUKA  kama hujaahidi ,...
... wewe HUJATOA AHADI.




NA kama HUJAAHIDI ,...
.... MKUU kunauwezekano MKUBWA weye huna AHADI ya KUVUNJA,...
..... ingawa TU usisahau UWEPO wako tu labda unawapa watu AHADI ambazo usipoangalia unaweza mpaka KUJILAUMU kwa kudhani ULIAHIDI MTU kitu.:-(



Swali:
  • Unabisha?

 Lakini  kama unajua tatizo  na SILIKA  za MTU ,....
.....TIMIZA usivyoahidi,....

...kwa kuwa hakuna kitu kitamu  KWA MTU  kama kupata kitatuacho TATIZO LAKE  ambacho hakutegemea na HAKUAHIDIWA!


Swali:
  • Si unajua jinsi gani utamu wa shilingi  ulivyo mtamu zaidi ya shilingi kama ukigawiwa shilingi uliyokuwa na shida nayo bila kutegemea hilo?

  • Ushawahi kusikilizia utamu wa kidude ulichopewa ghafla bila kutegemea wakati unahamu na kidude ulivyo tofauti?

NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA !

Hebu King Yellowman abadili kwa - Wrong Girl To Play With



Au tu King Yellowman alete tena-Reggae Calypso



Au tu KING YELLOWMAN amalizie na pambio-Gimme vagina

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP