Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UJUMBE MZURI ni kama UGALI uhitajio msaada wa MBOGA tamu ili SWALA ZIMA la kusukumiza TONGE lifanikiwe!:-(

>> Monday, February 22, 2010




UJUMBE MZURI labda hautoshi kwa kuwa tu ni UJUMBE MZURI,...
... ukizingatia walengwao  wanaweza wasiupokee USIPOSINDIKIZWA na kulainishwa na  NJIA ambazo walengwa hawafikirii ni MBAYA.:-(

Swali:
  • Si unajua kuna watu bila TAARABU  mahubiri yako YENYE UJUMBE MZURI WA BUSARA kuhusu mapenzi hawatayaelewa?


 UJUMBE MZURI ,..
....kwa kawaida hausikilizwi  kwenye WIMBO MBAYA.:-(

Na kuna wengi WASIKILIZAO matusi  vizuri,...
... ambao ni UJUMBE WASIOUPENDA  kwa kuwa tu wanapenda mrindimo wa muziki  AMBAO KWAO ni  wenye UJUMBE MBAYA .:-(


Ndio,...
....kuna wamsikilizao pia  MTU vizuri ,....
... kisa WANALAZIMIKA kuwa watulivu nakusikiliza  KWA KUWA wanatishwa na sura lake BAYA.:-(



Swali:

  • AU?
  • Si unakumbuka ugali  unaweza usiliwe kama hauletwi mezani na MBOGA tamu? 
  • Si unakumbuka UGALI mbaya unaweza kuliwa kama mboga tamu?
  • Kwani wewe hakuna wimbo uupendao ambao unajua UJUMBE WAKE NI NYOKO lakini hata hivyo unaurudiarudia NA MPAKA KUUKARIRI  WIMBO huo  wenye UJUMBE MBAYA KWAKO na kwa  MATOTO YAKO huku ukitingisha bichwa lako kisa mirindimo ya MUZIKI na SAUTI ya muimbaji  vinakukuna nanihii kunako?


Ndio,...
....TATIZO ni ,...
...ujumbe MZURI katika hata HOTUBA ,....
... labda inahitaji SURA fulani au tu SAUTI fulani  ili walengwao na UJUMBE wasikilize UJUMBE bila kushikiwa VIBOKO.:-(

Swali:

  • Si nasikia kuna wamsikilizao Barrack Obama  Marekani kisa wanapenda sauti na WANAOMSIKILIZA Rais KIKWETE Tanzania kisa wanampenda sura?
  • Si unakumbuka kuna sababu  si kila mtu  WEWE unamsikiliza ?
  • Si unajua kuna uwezekano majibu ya matatizo yako ulishapewa ila hukuyasikia kisa hukupenda wimbo au sura tu ya MTOA suluhisho?
  • Si unajua upendaye kumsikiliza unaweza kunogewa kufuatilia azungumziavyo jinsi ya kutatua matatizo ya kujisaidia kwa bata kuhitajivyo bata wavalishwe chupi kuliko USIYEPENDA kumsikiliza akizungumzia jinsi ya KUTATUA matatizo yako?




Ndio,...
.. labda  HATA MAANDISHI  usiyopenda KUYASOMA yanasomeka bado,...
... na husomi hata  BIBLIA na  KORANI   ingawa unajua vina UJUMBE  MWEMA tu,...

....kama tu kwenye kitabu cha KAMASUTRA ubobeavyo kwenye PICHA na sio MAANDISHI kisa kwa ladha yako VITABU hivyo banangenge vimekosewa kuandikwa VIZURI katika mirindimo  ikupandishayo MDADI WA KUSOMA  kama vile yaandikwavyo MAGAZETI YA UDAKU katika mirindimo iwezayo kukufanya uone HABARI ya KHADIJA hapendi kuvaa chupi ni HABARI MUHIMU SANA kuliko habari ya KUNA MAFURIKO Ludewa. .:-(

 Swali:

  • AU? 
  • Si unakumbuka pia kuwa  UJUMBE MZURI NA WA BUSARA kwa MTU MWINGINE  inawezekana ni KILE ukiitacho wewe  MATUSI?



 Staili ya MUANDISHI wa habari,...
... yaweza kusababisha usomee UANDAJI wa UDONGO walao wajawazito, HISTORI  au tu  angalau upende kujisomea stori za  UCHAWI uziogopazo,.....
..kisa STALI YA UANDISHI  kukufanya usiyependa kusoma uhusudu KUHAMIA mstari unaofuata katika HADITHI kisa kanogewa na SENTENSI ya kwanza ,...


..... kama tu kwa ASIYE PENDA UGALI WA MUHOGO kujikuta kamaliza bonge la sima kisa MBOGA tamu kusababisha tonge la kwanza kumshawishi MLENGWA kukata TONGE la pili na mpaka kumaliza MAAKULI bila kukumbuka huwa HAPENDI UGALI wa MUHOGO kwa kuwa yeye ni MUTU ile inapenda YUGALAI (Ugali kwa Kizungu) iliyopikwa kwa kutumia  UNGA WA SEMBE.:-(



Ndio,...
... UGALI bila MBOGA unalika bado .:-(



NI wazo tu HILI MHESHIMIWA!:-(


Hebu India.Arie, Dobet Gnahore, Idan Raichel na Blue Miller walete- Palea




Au tu India Irie na Dobet Gnahore waendelee na -Pearls


Bila kumsahau ALI KIBA katika kibao-Mac Muga

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 12:57 pm  

Na tumbo likijaa twasema gesi lakini hatujambi.... ndiyo tatizo la kufikiria kujamba ni kupunguza gesi.
na pengine njoo kinaweza kutumika kwa kutema mate au kukojoa tu. Hapo ndipo pagumu wakati ugumu ni akili zetu za kufikiria nikimwonyesha HASIRA MTAKATIFU SIMON KITUTURU ataniogopa na kuniheshimu ukizingatia hata nikimywea pombe za MBEGE nitamtusi LAKINI ITAKUWA UJUMBE! na bora ujumbe lakini kwa njia ya achaguayo mtoa ujumbe. Sijui Mmmmh!

Simon Kitururu 12:20 pm  

@Mkuu Markus: DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP