Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WAKATI tunajiandaa na SIASA chafu za BLOGU ambazo hazina uhusiano na kinacho BLOGIWA!:-(

>> Monday, February 08, 2010

Siasa ziko kila mahali ,....
..... na ukifikiria SIASA NI NINI waweza kujistukia kuwa WEWE MWENYEWE ni mwanasiasa ingawa LABDA siasa zako unazifanya katika dini hata kama sio MSIKITINI au tu KANISANI.




Na ukiwakusanya watu mahali,....
.....hasa ili jambo walitimize KAMA KUNDI waweza shangaa kazini kwenu jinsi mtofautianavyo kisiasa za kampuni na makampuni mengine hata katika zenu siasa za MSALANI.:-(


Swali:
  • Unabisha?


Ndio,...

... ukiniuliza mie ntasema kila sehemu wawapo watu wenye nia YAKUTEKELEZA JAMBO fulani kuna siasa zake ingawa MWANASIASA maarufu KWA KAWAIDA ni yule aliyefanikiwa kulipwa mshahara kwa kucheza na hiyo SIASA tu.


Na kwenye siasa kunamisingi iliyotayari kwa ajili ya kufanikisha SIASA CHAFU!



Swali:

  • Kwani kama wewe ni Mkristo wa KILUTHERI Tanzania , kwani hujastukia siasa chafu za kanisa hilo hasa UPARENI?

  • Unauhakika weye sio mwanasiasa tu wa MTANDAONI ingawa wajifanya hupendi siasa ofisini na twakukoma kama vile ubwabwajayo MTANDAONI yanaleta mabadiliko yoyote vile MTAANI?

  • Si umestukia siasa za wengine ZILIVYO tamu kweli kuzinyoshea vidole?

NI WAZO tu hili MHESHIMIWA na labda laishi hapahapa MTANDAONI!:-(



"Politicks is the science of good sense, applied to public affairs, and, as those are forever changing, what is wisdom to-day would be folly and perhaps, ruin to-morrow. Politicks is not a science so properly as a business. It cannot have fixed principles, from which a wise man would never swerve, unless the inconstancy of men's view of interest and the capriciousness of the tempers could be fixed." [Fisher Ames (1758–1808)]

- HABARI kimkao fulani NDIO HIYO!


Hebu baadhi wajikumbushe madisko fulani Ulaya kwa kwenda SPAIN kukutana na LAS KETCHUP wakirudia- The ketchup SONG



Au tu twende tu SWEDEN wengine wakumbushwe kitu na huyu MSWIDI Dr BOMBAY yaliyojiri katika madisko ya SWEDEN kwa kitu- Calcutta


Au tu SALLY NYOLO arudishe UAFRIKA kwa kutuliza manyanga KWA kitu- AWOU

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 6:23 am  

Mkuu mimi nina uhakika siyo mwanasiasa kabisa.

Simon Kitururu 10:33 pm  

@Askofu Fadhy: Blogu yako iitwayo ``MWANANCHI MIMI´´ hudhani hakuna afikiriaye misingi ya jina hilo ni kifikira za kisiasa umekaa wapi?

Fadhy Mtanga 6:57 am  

Hapo umeniweza. Maneno yameniisha ka' simu isiyo na vocha.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP