Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MATATIZO ya MBUZI na BATA kwa mtazamo wa BINADAMU!

>> Tuesday, February 09, 2010

Labda haki za MBUZI na BATA jinsi zinavyokanyagwa,...
.... ukimpata BINADAMU mtetezi ajuaye kuelezea,....

.... waweza kuamini NI KWELI kuna BINADAMU ajuaye MATATIZO hata ya KUKU kuliko hata KUKU mwenyewe.:-(




Swali:

  • Si unajua LAKINI  kuna uwezekano mkubwa KUKU na JOGOO hawafikirii kama BINADAMU hata katika mapenzi yao kibandani?


Na wakati kwa BINADAMU imefikia kuna BINADAMU anakuhakikishia kuwa ANAJUA tatizo la MBUZI wasiyezungumza LUGHA MOJA ni kwamba anaumwa KICHWA kwa KUWAZA LEO MAJANI ATAPATA WAPI kwa kuwa matatizo ya WANYAMA anayaelewa,.....

.... waweza kujikuta bado unajikanyaga kumuelewa BINADAMU HUYO ambaye mnazungumza LUGHA MOJA kama tu Mtakatifu Simon Kitururu asiyejua KUNENA KWA LUGHA kwa yake ya KIBINADAMU ,...

....nakutomuelewa mtu ANAONGELEA NINI wakati huohuo wakati ayaongeayo ni ya MWANADAMU na vipengele ANYAMBULISHAVYO ni vile vimgusavyo BINADAMU.:-(


Na labda UKIFIKIRIA tatizo kubwa la BINADAMU ni kuelewa,....
.....na jinsi tu MTU anavyoelewa aweza kujigundua alivyo MNYAMA ingawa kwa jina tu na muonekano ndio watu wanatafsiri kuwa ni BINADAMU.:-(





Swali:
  • Unafikiri BINADAMU anatabia ya KIBINADAMU?
  • Unafikiri UBINADAMU unaruhusu BINADAMU kuelewa MATATIZO ya BINADAMU mwingine?
  • Unafikiri UBINADAMU unaruhusu BINADAMU kumuelewa BATA?

  • Ushawahi kufikiria hivi BINADAMU kwa wastani ana- matatizo mangapi na ya aina ngapi tukiachilia mbali tatizo la kuelewa binadamu MAISHANI?
  • Ushawahi kufikiria kuku huwa anafikiria nini?
  • Unafikiri najua unafikiria nini?





Sikatai,....
...labda BINADAMU anaelewa MATATIZO ya MBUZI na BATA kuliko MBUZI na BATA ....hasa UKIFIKIRIA kuwa UKWELI wenyewe wa BINADAMU na anachoelewa kama jaji ni BINADAMU utaeleweka KIBINADAMU tu.:-(


Na kwa bahati mbaya kielewekacho KIBINADAMU ndio mara nyingi kimshangazacho BINADAMU,...
...na kiwezacho kumshangaza BINADAMU kinaweza kuwa;....

..... NI kweli, - BINADAMU huelewa zaidi YA MBUZI na BATA MJAMZITO kuliko hata ya BINADAMU wakawaida tu wakutananaye KILA SIKU ambaye wala hata busha la kike hana na LUGHA yake ya matanuzi ni KISWA- HILI.:-(



Swali:
  • Unafikiri NYAU hamuelewi BIN -ADAMU ki -PAKA SHUME?


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!



HEBU tu katika kubadili hali ya hewa KIJIWENI Maestro Dekula KAHANGA Vumbi arudishe gitaa katika -MAKUMBELE

NGUZA VIKING alete pia kitu- Ni wewe PEKEE



Au tu Papi Kocha na Nguza Viking warudishe- SEA

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP