Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KINYAA!

>> Wednesday, February 03, 2010

CHAKO ,...
....hakikutii kinyaa HATA kama kina usaha.

CHAKO,...
...
hata kama kikitamkwa kwa waungwana ni LUGHA CHAFU kwa kukiamini hukigeuza nasaha.


CHAKO,...
...
kwa kunuka kwake kwa WENGI wengine LABDA hukulinda kama silaha.





NA,....




KINYAA chako ni chako ,...
.....na CHANGU ni changu.



KINYAA chako ni uamuzi wako kutokana na yako,...
.... KWANGU na yangu ni halihalisi KWANGU .



Na kitiacho kinyaa kwako ,....
..... KWANGU chaweza kuwa ndio MAISHA YANGU.:-(



Swali:

  • Unafikiri kama KITU CHAKO ni hali halisi KWAKO utasikia kinyaa kwa chako?

  • Unafikiri KIDONDA NDUGU kinukacho kama ni chako utakuwa na jeuri ya kusikia KINYAA wakati ni chako?

  • SI unakumbuka siri ya KIINI cha staili ya KINYAA CHAKO ni maisha yako?




Na LABDA,...

.... kinyaa ni UAMUZI TU,...
... na ikibidi au IKILAZIMIKA,...

.... hakuna kitiacho KINYAA na wala hakuna MWENYE KINYAA.:-(





NI HILO TU na ni wazo tu hili MKUU!


Au ngojea tubadili kwa kumdeku mbwa atuonyeshe jinsi ya kucheza MAMBO -Mambo Dancing Dog



Au tu sasa tutafanyaje labda ngojea naye Lou Bega arudie tu- Mambo Nr 5

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 8:23 am  

kinyaa ni jinsi unavyoweka hisia katika ubongo wako.
Mfano wataalamu wa afya, hata kama una donda ndugu, wanakuhudumia kama vile umelitia pafyumu.
Matopaz pia wanapozibua vyoo, hawana noma kabisa.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 9:28 am  

@Chib: uminena mkuu :-)

kwa kuwa kila kitu kiko akilini.

huwa nashangaa mtu akihitilafiana na mtu akamtukana 'mshenzi wewe'. Njemba linakasiriiiika :-(

Unadhani kwa kumuita mshenzi anageuka kuwa mshenzi hata kama hajawahi kuwa wala si mshenzi? :-(

yaweza kuwa mshenzi ni SIFA nzuri siku hizi hivo mtu akikuelekezea KINYAA chake usikonde mkubwa :-)

Simon Kitururu 12:31 pm  

``Na LABDA,...
.... kinyaa ni UAMUZI TU,...
... na ikibidi au IKILAZIMIKA,...

.... hakuna kitiacho KINYAA na wala hakuna MWENYE KINYAA.:-(´´

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP