TEKNOLOJIA IPO na katika ulimwengu wa FACEBOOK ,- kuna UJUMBE na status : ``Niko MSALANI!´´
>> Tuesday, February 16, 2010
Katika ulimwengu wa GBuzz,....
... MTONYO waweza kuwa ni ,....
- ``Nimeenda KUCHIMBA dawa!´´Katika ulimwengu wa TWITTER ,....
... UJUMBE waweza kuwa ni ; .....
-``Niko CHOONI!´´
Na katika ulimwengu ambao TEKINOLOJIA ni ala ya NGOMA katika enzi ZETU za MKOLONI,...
..... UJUMBE; Gdu du dududu du ,....
.. tafsiri yaweza kuwa ilikuwa ni ;...
-`` MKOLONI anakuja chimba choo kama hutaki kuchapwa HAMSA ishirini kwa kwenda haja vichakani!``
-`` MKOLONI anakuja chimba choo kama hutaki kuchapwa HAMSA ishirini kwa kwenda haja vichakani!``
Swali:
- Weye uliyebobea kwenye INTERNET na E-mail zako , UNAKUMBUKA jinsi ya kuandika BARUA lakini?
- Si unakumbuka hata teknologia ibadilike vipi haisaidii kutengeneza UJUMBE na ni MTU mwenyewe katika tumizi la tekinolojia aamuaye ujumbe autumao kwa wasio na CHAKULA kuwa ni jinsi CHOO cha kukaa kisafi kiongezevyo upotezaji wa muda wa watu CHOONI ?
Kumbukumbu:
Kuna kipindi barua ya MTU ya kwanza kwa MPENZI MLENGWA kutokana na elimu za vijiwe vya kitoto ,...
...ilifanikiwa kuchorwa mpaka MAUA na kunyunyiziwa poda KWA WENGINE huku yote hayo MTU kiroho kikimdunda kutokana na UZITO wa ujumbe ulioandikwa wa;...
.... ``Helo , mimi nakupenda na NAOMBA URAFIKI!``
Siku hizi MTU ZILIZOPIGA UMRI zinaweza onea wivu wale ambao WAMEZALIWA wakati maswala yote ni TEXT MESEJI za simu na MWALIMU ni TELEVISHENI ;....
.....halafu UJUMBE wa mtafuta MPENZI mwenyewe BADO ni;....
... ``Helo , kunakitu nataka kukuambia NI DIP basi simu yangu haina hela!´´
Swali:
- Unafikiri tekinolojia hizi mpya usipoangalia hazikuondoi hata ujuzi wa kupiga mluzi ili kuita MTU?
- Unafikiri pamoja na HIZI teknolojia kurahisisha upataji wa habari ukweli wenyewe si kwamba habari utakazo kuzipata ushazitengenezea mipaka na kwa mpenda habari za choo asilimia kubwa ya habari na ujumbe apatao ni wakuhusiana na CHOO kama tu mpenda BONGO FLEVA miziki kibao ailengayo na kuisikiliza isivyokuwa ni TAARABU?
- Si unakumbuka ni wewe na sio TEKNOLOJIA itoayo na kupokea UJUMBE na hata kwa kutumia tekinolojia gani bado BINADAMU atafariki akiwa amefanikiwa kujua tu machache katika duniahii yenye mambo zaidi ya KIDUCHU kilengwacho na mtu?
Ndio,....
... kuna wakati madhumuni ya BARUA yalikuwa ni KUKUJULIA hali.
Na wakati tunaishi katika ulimwengu ambao MADHUMUNI ya kuwa ANONYMOUS MTANDAONI yanaweza kuwa ni KUTUKANA MTU, ...
.....tukumbuke tu TEKINOLOJIA haiongezi idadi ya UJUMBE zaidi ya KUFIKISHA tu HATA UJINGA kama UJUMBE ,....
NI HILO TU na ni wazo tu MHESHIMIWA!
Hebu Spike Lee joints ituletee Mo' BETTER BLUES ili akina Denzel Washington , Wesley Snipes,.... wamwage- DA BLUES
Au tu Tabi BONNEY arudie- YOU
Au tu TABI BONNEY aendelee tu kubadili kwa -The Pocket
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mtakatifu Simon leo umeniacha kinywa wazi. Umenikumbusha enzi zile nasoma nilikuwa naenda kutega mingo karibu na geti nikivizia atoke ili nimkonyeze na kuomba hako kaurafiki. Ama nategea katoto kapite nakatuma huku nikikashawishi kasinitaje jina. Kaseme tu "nanihino kuna mtu anakuita pale!" mwenyewe anaelewa ni mchizeni wake anamwita. Anazuga na ndoo kama anaenda bombani kuteka maji.
Sasa teknolojia imerahisisha kazi. Unatext tu "tukutane pale pale uchochoroni sasa mbili giza likishaingia"
Mtoto anategea wazazi wanaangalia ITV habari ye anazuga anamwaga takataka kumbe umebana uchochoroni ukiwa na hamu japo ya ulimi.
Duh!
Imebaki historia.
Ila kweli hao akina 'anonymous' hao kwanini wafiche majina?
Mtatifu Simo na Askofu Fadhi duh! ninyi kumbe mlianza utundu mapema hivi. Nashangaa huo Utakatifu na Uaskofi sijui mmeupataje..:-)
mmmh! tutafika tu ..ndio maana Dr Remmy aliimba kwenye moja nyimbo zake kipenda roho ndio yale yale ya kila moja na KWELI na UONGO wake
Post a Comment