Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Jiografia NGUMU Tanzania!:-(

>> Friday, February 26, 2010

[Tahadhari: Hii taralila ina TAFAKURI ambayo inaweza isikufundishe kitu hasa kama wewe sio mtumiaji RAMANI !:-(]




Hebu tujifunze RAMANI ya kwenda kwa akina KHADIJA akaaye karibu na kwa FUNDI VIATU,...
....katika kujaribu kukukumbushana jinsi ya kusoma RAMANI ukiwa TANZANIA.





Jinsi ya kumuelekeza mtu mahali TANZANIA ni bonge la SANAA!



Jinsi ya kumuelekeza MTU kwa akina KHADIJA ,....

....kwaweza MPAKA kukujulisha KIPAJI chako MWENYEWE kile cha KUNUSA HARUFU MBALIMBALI  ambacho wazazi wako hawakufanikiwa kukistukia,....

....kwa kuwa waweza kujikuta ili kurahisisha kumuelekeza KIJEBA kwa akina KHADIJA inabidi ugusie mpaka aina za HARUFU mtu atakazo kutananazo NJIANI ,....


....harufu za TOKEA mlipo MPAKA   kwa akina KHADIJA ili tu kuhakikisha NJEMBA MWENYE RAMANI, ramani    haimpotezi MUELEKEO na kumkosesha KUFIKA kwenye  mihadi na KHADIJA MTOTO MZURI,....
....kisa tu  harufu ya mfereji wa chooo hakuinusa.:-(




NDIO,...
....jiografia na USOMAJI WA RAMANI ufunzwao MASHULENI  Bongo NYOSO  hautoshi,...

.....kwa kuwa kirahisi waweza kujikuta inabidi  ili kumuelekeza MTU kwa akina KHADIJA inabidi  bila kuangalia ramani,...



.....  umuelekeze  :


``......ukifika MBUYUNI  weye ulizia kwa Simon Kibaka wa MINAZINI na utaelekezwa,....

......na wakati unaelekea huko kabla ya hata hujafika  MINAZINI utastukia kuna sehemu inanukia mavi,....

......basi hapo kata kulia utaona kuna kauchochoro ,....

... ukishakata kona na uko kwenye UCHOCHORO  weye nenda weee , NENDAAAA WEEEEE,  mpaka mwisho wa uchochoro ambako kunanukia KOROSHO za KUCHOMA, halafu  kata kulia ambako utatokea kwenye nyumba ambayo ina kibao MBWA mkali,....

....hapo KWENYE MBWA MKALI  utatolewa baruti a.k.a  KUTOLEWA MKUKU , nikiwa na maana UTAFUKUZWA NA DOGI a.ka MBWA Mweusi ,....

Wakati unatolewa BARUTI NA MBWA  hakikisha unakimbilia kushoto mwa FENSI YA MICHONGOMA  na MBWA huyo atakufukuza kupita NYUMBA kadhaa.

Akimaliza kukutoa NDUKI MBWA  na kugeuza kurudi kwao angalia kulia utaona kuna nyumba ina BATI jeusi ,...
....basi nenda hapo kwa kufuata barabara yenye mfereji unukao MIKOJO mpaka ukute kuna genge la nyanya. MUULIZIE MUUZA nyanya kwa akina KHADIJA ni  wapi atakueleza.


SI umenielewa EEE?

.....YANI ni hapo hapo tu na haita kuchukua hata dakika kumi utakuwa umefika kwao ambako jifanye unakiu ya Maji kwa kuwa BABA yake Khadija BADO ana UNOKO WA ENZI za wakati  kuna ISIDINGO kwenye TV ZANZIBAR tu,...


....na bara ni kwa NYERERE  TU ambako kulikuwa na TV na wakati huo  MZEE MZIMA alikuwa anadeku BBC  tu kwenye TV a.ka LUNINGA ,...


....na  kwa hiyo usimuulizie KHADIJA kwao kwa jina LAKE  moja kwa moja lasivyo utatolewa BARUTI na KHADIJA kipenzi chako atakula KIBANO na matumizi yako yote ya RAMANI hayatafanikisha uzinzi.:-(´´





Ngojea nifupishe somo hili la  jiografia  ya  kwa akina KHADIJA kwa ufafanuzi zaidi hasa kwa aliyezoea kusoma RAMANI.:


Kwa kifupi,...
....kama nia ni watu wafike kwa akina KHADIJA,....

..... hatua ya kwanza ni kuhakikisha wewe ni BINGWA wakukariri,...

...kwa kuwa KUKARIRI KWAKO ndiko kutamsaidia mwenye ANUANI na RAMANI ya kwa akina KHADIJA wakati anaenda KIMUELEKEO  hafuati tu ramani ,...

....kwa kuwa RAMANI aliyonayo inaweza kuwa hainakazi kama hujatamka RANGI za MABATI , MIBUYU iliyokuwepo NJIANI na bila KUSAHAU HARUFU UZINUSAZO NJIANI  kwa kuwa TANZANIA kwa kiasi kikubwa ujenzi bado haufuati RAMANI ya MJI  na  KIBOSILE hakawii kujenga banda la MBUZI  sehemu ionyeshayo ni njia kwenye RAMANI.:-(


Swali:

  • Unabisha?
  • Ushajisikiliza wakati unamuelekeza MTU mahali Ze BONGO?


Kwa hiyo,...

...jaribu kukariri kila kitu ulichokiona wakati unaenda kwa kina KHADIJA na ikibidi HARUFU zilizo tekenya pua yako na fundi viatu  chini ya MUEMBE ndio alama umekaribi  upalengapo.


Kwa hiyo ,...
.... kumbuka kuwa bado KUULIZIA watu ni muhimu katika RAMANI zetu BONGO na kama huna heshima na HIYO ikupe MOTISHA ya kusalimia watu kwa kuwa huwezi jua ni nani ambaye utamuhitaji angalau kuwa na uhakika  vichaka viko wapi ikibidi uchimbe dawa kabisaa kabla hujagonga hodi kwa akina KHADIJA.
Unajua TENA mara nyingi ni vigumu kuomba kwenda msalani haraka haraka UGENINI na ni balaa ukienda msalani  baada ya mafanikio ya choo kikubwa ukastukia kwa mpenzi KHADIJA maji yamekatika na huja falashi malighafi yenye ukubwa wa kutosha UGENINI.:-(



Tukiachana na hilo:
Swali:

  • Miji ina RAMANI Tanzania lakini unafikiri ni kwanini RAMANI za mipango ya MIJI hazifuatwi mpaka siku hizi katika ujenzi wa nyumba MPYA mahali lukuki?

  • Si unakumbuka tunavyoongea kuna viwanja vinavyoendelea kuuzwa ambavyo haviko katika ramani ya MIJI ?

  • Unafikiri kati ya MJENGA holela na MUUZAJI VIWANJA ambaye ndiye MSIMAMIAJI wa viwanja HOLELA nni nani mwenye kosa?


Ndio,...
...... matatizo yajulikanayo tayari kama tu ya KUPANGA MJI yanaendelea kuachiwa kuwepo TANZANIA na unaweza kukuta azibaye BARABARA na MIFEREJI ya ENEO iliyoko kwenye ramani ndiye MKUU wa eneo KIOFISI na kiutawala katika  eneo.:-(



Ndio,....
....JIOGRAFIA ngumu TANZANIA ,...
...na kuna uwezekano RAMANI kama zifundishwavyo katika somo la JIOGRAFIA MASHULENI hazijitoshelezi ,...


.... na  kwa hiyo RAMANI YAKO labda haitoshi kukufikisha kwenu kama HUKUJUI  KWENU Mheshimiwa.:-(


Swali:

  • AU?


TUNAKUMBUSHANA TU MKUU na usikonde!

IJUMAA na WIKIENDI NJEMA!

Heb kwa wasikilizaji maneno Ras NAS atusaidie kubadili mshawasha kwa kibao-Dar-es Salaam



Eddy Grant arudie kwa wasikilizaji maneno kitu -Gimme HOPE Jo' anna




Eddy GRANT arudie pia kwa wasikilizaji maneno ndude- War Party




Au tu EDDY GRANT amalizie tu na  ndude -Living on the frontline

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP