Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Chandarua CHENYE manufaa NA CHA BUSARA kwako katika KUZUIA MBU ni nyavu nzuri za KUVULIA SAMAKI kwa MWENZIO!:-(

>> Thursday, February 18, 2010

Wewe katika MAISHA sio WAO,...
..... kitu hicho hicho kikabiliwacho na swala la kuwa MIMI sio WEWE na  nipendacho MIMI ni kutokana na nikabilianavyo mimi KITU KISABABISHACHO  kwangu  kupenda upendacho wewe yawezekano inahitaji NIJIFUNZE.:-(

Na kujifunza inahitaji SABABU,.....
... na tatizo linarudi pale pale kuwa SABABU ZAKO zilizokufunza  KUTOPENDA hata SINDIMBA na ujanja kwako ni BONGO FLEVA labda yabidi nikuelewe kwanini katika NGOMA nzito zote TANZANIA  wewe ikudakayo DAR es SALAAM kirahisi sio MDUNDIKO na ni KWASAKWASA ya kutoka kwa BABA MOBUTU ambaye ndio juzijuzi WANASIASA wetu TANZANIA wanastukia KUMUIGA katika UFISADI.


Swali:

  • AU?
 Tukiachana na hilo, kumbuka tu .....

Kwa aaminiye katika KUCHEZA peku  hata uumpe KONDOMU za BURE,....
......kama staili ya UMUHIMU uuonao hauangalii kwa jicho na ujuzi wa kunogewa UTAMU  kama wewe uchezaye MAMBO KWA SOKSI,....
.....hata kama ATAKUFA atakufa wakati  anachezea kinjegele  PEKU kwa raha zake wakati UJUMBE wa UDAICHO NI MUHIMU alikusikiliza..

Swali:
  • Kwani unafikiri  wangapi waambukizwapo UKIMWI walikuwa na KONDOMU na hawakuamua kuitumia tu?

Na NDIO,...
.....chenye manufaa kwako hata ukigawe bure kama wagawavyo VYANDARUA kuzuia MBU na MALARIA ,...


.... CHANDARUA kinaweza geuzwa TU  kuwa ni nyavu za kuvulia SAMAKI ingawa ulihubiri na kupigiwa makofi  ukiongelea  CHA MUHIMU KWAKO ambacho  NI KUZUIA MALARIA wakati CHA MUHIMU KWA UWALENGAO NA MSAADA ni nyavu kama za CHANDARUA ambazo ni muhimu zaidi kwao KWA kuvulia SAMAKI.:-(


Swali:
  • Unafikiri  ni kwanini kuna WANAWAKE wateteao umuhimu wa KUKEKETWA wakati wanogewao maswala kwa kuwa na kinjegere wanasimulia tamu za kutokeketwa?


Ndio,...
...mwisho wa siku  LABDA ,...

... cha muhimu kwako  na ambacho unaamini kina umuhimu kwa wengine bado ni CHENYE manufaa ZAIDI  kwako kwa kuwa UMUHIMU WAKE una  MTAZAMO WAKO.:-(


Na kama chako UAMINICHO kinamanufaa kwa wengine ,....
..... ukitaka WENGINE waambukizwe kunogewa kwako  katika hicho,...
... labda kabla hujachukua HATUA YOYOTE ,....
...FIKIRIA wanogewavyo wengine kabla ya kuwapanulia hicho wengine WATU na  kufaidisha NZI  tu wakati uliotaka waonje ni WATU,...
...na wala sio hao INZI  wenye kunogewa na upanuacho vingine.:-(




Swali:

  • Si unajua kuna uwezekano kabisa UFIKIRIACHO NI MSAADA KWA WENGINE ni kwa kuwa tu kwa kufikiria hivyo hicho ni msaada kwako?



NI TAFAKARI tu HII Mheshimiwa! 

Na MSOME,...
.....Kadinali Chacha o'Wambura NG'WANAMBITI  aliyeiotesha TAFAKURI HII  kwa kuzungumzia jinsi VYANDARUA VIGEUZWAVYO    sehemu za kupoozea maisha magumu KUKU HAPA









Au HEBU Mr.CHEEKS na STEPHEN MARLEY wabadili kabisa hali ya hewa kijiweni kwa kitu  - Guiltiness


Mr CHEEKS alete-Double B Flow



Au tu Mr.Cheeks amalizie kwa - Lights, Camera, Action

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP