MINDSET a.k.a ULE MKAO UBONGO wa ANDUNJE wakufikiri na kukabili mambo UNAVYONG'ANG'ANIA unachong'ang'ania.
>> Saturday, February 13, 2010
Jinsi mtu AFIKIRIAVYO kitu ,....
....HUATHIRIWA na mkao wa BONGO LAKE ulivyozoezwa jinsi ya KUTUMIWA a.k.a MINDSET yake katika MAswala.
Na aingiliaye swala moja au kimoja kitu,...
.....waweza kujua staili yake ya KUFIKIRIA MAMBO mengi kwa kuchunguza tu anavyofikiria hasa STAILI na VIGEZO atumiavyo kuongoza MUELEKEO wa anavyofikiri WAKATI analiingia SWALA.
MTU anavyofikiria kipya kitu,...
... kuna VITU VYA ZAMANI ambavyo UBONGO ULISHAVING'ANG'ANIA ambavyo alishawahi kuvifikiria au KUFUNZWA na kuviamini ndio kweli ambavyo vinachangia MKAO WA FIKIRA za MTU katika vitu VIPYA kitu kisababishacho UDHAIFU au UMADHUBUTI wa staili ya kukabili fikra ya jambo jipya ambayo mara nyingine haihitaji kuoanishwa na la zamani ambalo liko ubongoni SWALA.
Swali:
- Si unajua BONGO lako likisha unganisha USIKU wa GIZA na UCHAWI makaburini unaweza kusahau wajifichao makaburini wanaweza kuwa ni MAJANGILI wajiandaao kupora mtu na wala sio WACHAWI?
- SI umeshakutana na wacha MUNGU wenye akili ambao BADO kwao ni vigumu kuelewa mtu yoyote ambaye matatuzi ya maswala yake hayahusishi kumcha Mungu au hata kumuomba Mungu kwa kuwa kwao UBONGO ndio ushang'ang'ania staili ya aina moja ya kukabili mambo na hakuna walionalo bila kuingizia ANGLE YA MUNGU a.k.a mchepuo wa Padre au shekhe anasemaje katika swala?
- Kwani hujawahi kukutana AU KUSIKIA kuna mtu ambaye kwake BONGE la ugali ndio chakula na hata umpe wali kiasi gani haamini umempa msosi kwa kuwa KIFIKIRA kashaamini hivyo?
- Kwani humjui angalau MTANZANIA MMOJA ambaye MINDSET a.k.a MNG'ANG'ANO wa KITEKENYA STAILI YA AFIKIRIAVYO KUKABILI MASWALA umemuaminisha MWAFRIKA hawezi na MTANZANIA hajui , ambaye hata awe Mkufunzi wa CHUO CHA UAFRIKA ambaye haki ya nani tena HAWEZI kutetea ajuacho HATA AMBACHO NI KWELI katika UAFRIKA hasa akibishiwa na Mzungu , Mchina, Muarabu,..... au Mhindi ?
Tatizo la BONGO kukaa mkao fulani tu,...
....ndio kisa baadhi ya MATATIZO YAKO fulani uliyokuwa nayo mwaka juzi labda utakuwa nayo MWAKA kesho kisa tu hata MWAKA KESHO utakuwa bado unayakabili kifikira a.k.a APPROACH YAKO,....
....katika swala kikutumia ubongo itakuwa ileile iliyosababisha ushindwe mwaka JUZI.:-(
Swali:
- AU?
- Unafikiri huna staili moja utumiayo katika kufikiria kila jambo kiasi kwamba kama sasa hivi wewe ni KIBAKA kwa ufikiriavyo lazima ukiwa meneja wa choo cha stendi , Mbunge, waziri au hata Rais tu wa KIBAHA au PEMBA zikijitenga kutoka TANZANIA utaiba tu?
- Si unajua kiruka njia sio mavazi lakini kuna mavazi fulani bado yanakufanya ufikirie usiye mjua ni kiruka njia kutokana na UBONGO wako ulivyojifunza yaliyopita NA KUYAKARIRI ambayo sio lazima ni sahihi leo?
NI HILO TU na HILI ni wazo tu MHESHIMIWA !:-(
Au tu Richard Bona abadili kwa kitu- One Minute
Au tu Richard Bona arudie- EKWA MWATO
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
duh! mkuu leo umenifikirisha kuliko.
@Askofu Fadhy: :-)
Post a Comment