Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda umuhimu wa MTOTO kwa baadhi ni TUMIZI la MTOTO,.....

>> Thursday, February 18, 2010

.....katika ajenda za WAKUBWA waliozaa kujisikia kuna kitu ANGALAU KIMOJA TU wamefanikiwa kufanya  KATIKA ya DUNIANI !:-(





NA labda sio utani ,...
... kuwa umuhimu wa  MTOTO kwa binadamu waliozaa ni tumizi  la ya mtoto LIZIBALO na KUJAZIA  kizibwacho na hisia na shughuli zitokanazo na kuwa na MTOTO DUNIANI ambazo huanzia  tokea  mzazi ajue atapata  MTOTO.:-(

Labda si utani ,...
...MTOTO kama tumizi kuna walikabilio kama ni SHUGHULI tu mojawapo iwasaidiayo WENYE MTOTO kujisikia tu kuwa pamoja na matatizo yote  ni kweli WAKO HAI na kithibitisho ni hata mwenye utapiamlo MTOTO.:-(

Labda sio utani,...
... mtoto ni MTAJI wa baadaye , wakati MKE ni trekta la sasa HIVI kama UNA SHAMBA  kubwa na pembejeo ni JEMBE shambani katika shughuli ya kilimo isiyo ya KITOTO.:-(


Swali:
  • MTOTO wako ni wa nini wakati kwa MTAKA WAJUKUU anaweza zaa mtoto atakaye kuwa PADRE  wa KATOLIKI asiyeruhusiwa kuoa au kuzini kwa ruksa iletwayo kwa ndoa?


  • MTOTO wako ni wanini wakati kwa MTAKA WAJUKUU anaweza kuzaa mtoto tasa?

Na kuna wenye WATOTO,...
... kwa kuwa katika kuhusudu URODA mtoto ni ajali kazini.


Kuna wenye MTOTO,...
... kwa sababu  KUWA NA mtoto kwawasaidia tu KUWALETEA  maana ya maisha hapa duniani.


Na kuna wahitajio MTOTO,...
.... kama msaada wa MAISHA uzeeni.


Swali:

  • Unauhakika ni wangapi wana watoto na hata siku moja hawakufikiri ni kwanini wana watoto?

  • Katika watoto waitwao wa mtaani duniani unafikiri ni wangapi wamezaliwa kutokana na wazazi wao kutofikiria yahusianayo na MTOTO kabla ya kuzaa mtoto?

  • Unafikiri matajiri kama akina OPRAH wenye mabiloni si kufuru kutokuwa na MTOTO au akina Rais Clinton kuwa na mtoto mmoja tu si kitendo cha upotezaji wa mbegu na mayai yashughulikiayo  mafanikio ya MMIMBISHO?

  • Hivi MTOTO kwako ni wa nini?


Na kwa wengine ,...
.. LABDA mtoto UMUHIMU WAKE ni kama tu MWANASESERE kwa kuwa,....


..... SI MAMA YAKE YUPO atakaye mshughulikia ambaye yeye ni VIGUMU kumkimbia bila nyonyo kuvuja MTINDI akilia?





Swali:
  • Unauhakika  ni kweli unahitaji WATOTO au hata  ndoa ukizingatia maisha yako ukiyatafutia MAANA kivingine yanaweza kuleta tu maana kama ya  MASISTA wa KIKATOLIKI ambayo bila ZE TOTOZ  yanalipa tu na hutabadili nepi rojo? 


NI tafakari tu hii MHESHIMIWA wakati tunajua  MAZOEZI ya kitendo yanaendelea DUNIANI  na kwa kitendo  KUNA mtu kammegea MTU mahali fulani MIMBA !:-(



Au hebu THE LAST POETS wabadili zaidi kwa tafsiri yao ya - Black is




Au tu The LAST POETS wabadili tena mtazamo wao kuwa -NIGGERS are SCARED of REVOLUTION




Au tu The Last Poets wamalizie kwa - When The Revolution Comes

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP