Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KWELI si kila MTU anapenda KACHUMBARI,....

>> Saturday, January 23, 2010

...na kwa bahati mbaya,...
... huwezi KUMLAZIMISHA mtu upendacho AKIPENDE,...

....ingawa unaweza kumshikia KIBOKO asiyependa UJI KIFUNIKO akanywa UJI BILAURI na kukuchekea wakati ANAGUGUMIA huo uji wa muhogo ingawa UKWELI UKO PALEPALE KUWA kwa uji hana PENDO.:-(


Na kwa kuwa si kila mtu anapenda KACHUMBARI,...
....kwa hiyo mpenda kachumbari kama unajali watu wengine kumbuka kuangalia wenzio kama wananogewa KWELI NA KACHUMBARI YAKO KWELI kama wewe hasa ukikumbuka labda kachumbari yenyewe unogewayo nayo labda imezidi nyanya HATA KWAKO ila wanogewa zaidi na si kachumbairi hiyo , ila tu wanogewa na lako la KACHUMBARI pendo.:-(


Swali ndugu katika hoja kwa afikiriaye:
  • KACHUMBARI kama ni SHEREHE YA BIRTHDAY ambayo KWA kawaida hausherehekei kwa misimamo YAKO, unafikiri unaweza kulazimisha watu wasisherehekee birthday yako kwa kuwa wewe husherehekei?



Kwa kifupi,...
.....SI KILA mtu alaye kachumbari anapenda KACHUMBARI na ,...

... kama ASIYEPENDA KACHUMBARI alaye kachumbari bila kudhurika kwa kuwa kwa kitendo hicho wamuandaliao KACHUMBARI wanafarijika na kitendo zaidi ya utamu wa kachumbari ,..

.....UKINIULIZA naweza kudai LABDA hiyo ni moja ya VIITWAVYO kutokuwa MBINAFSI KWA AJILAZIMISHAYE KACHUMBARI ajuaye hadhuriki na kachumbari KWA kuwa anaheshimu WAPENDAO KACHUMBARI, ingawa asiyedhurika hapendi kachumbari NA anashiriki KACHUMBARI.:-(



Swali:
  • Unafikiri kunaapotezacho Mgogo akijiunga na sherehe ya Wamasai KATIKA kusherehekea kupoteza Umasai wao kwa kuwa ni Krismasi ambayo haihusiani na UGOGO na anaamini Wamasai hao hawadhuriki na shamrashamra zao za Krismasi ingawa KIMILA Krismasi haina uhusiano na Umasai?
  • Tukirudi palepale kwenye kipele cha hoja, SI unakumbuka kuwa hata kama unapenda VIPI KACHUMBARI lakini BADO UKWELI UKO PALEPALE kuwa sio kila MTU anapenda KACHUMBARI?

NAACHA WAZO na ni RUKSA kutolielewa HASA KAMA wewe ni MVIVU KUFIKIRIA kwa kuwa haki ya nani HILI ni wazo tu MKUU!

Hebu tupooze kwa kwenda tena CUBA Ray Baretto na MONGO Santamaria warudishe- Congo Bongo




Au tu Santana Ft Rob Thomas warudie- Smooth

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 8:05 am  

Kama ambavyo mtu asiyependa kilaji anaamua kujilazimisha sababu ametoka mtoko na Mtakatifu Simeone Mkirene!

Fadhy Mtanga 8:05 am  
This comment has been removed by the author.
Simon Kitururu 2:56 pm  

@Papa Fadhy:Si utani!:-(

Mija Shija Sayi 10:44 pm  

Basi kwa vile umetibuana na Kitururu unanilazimisha na mimi nimchunie Kitururu!

Simon Kitururu 1:08 am  

@Da Mija: Si utani Da Mija!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP