STAREHE ya kutumia MUDA BINAFSI kuhukumu WENGINE na maisha yao BINAFSI!
>> Monday, January 25, 2010
Ni kweli,...
... kunyoshewa vidole hainogi kama KUNYOSHEA wengine vidole hasa kama kilengwacho ni KASORO.Na kunyoshea wengine vidole KUHUSU MAMBO YAO BINAFSI inasaidia sana kupunguza muda WA mtu kujichunguza mwenyewe BINAFSi hasa kama lengo ni kukwepa kujistukia zako KASORO.
Na mtu asipokuwa muangalifu anaweza akafikiri kutambua kasoro ni kitu rahisi mpaka itakapotokea AKAFIKIRIA na kustukia  ukiwadadisi watu utagundua karibu kila kitu ukionacho hakina kasoro kuna AMBAO wanakikosoa kwa KASORO.:-(
Na haki ya nani  uonacho kina kasoro kama tu MATEGE,...
.... kuna apendaye MTU kisa matege mpaka  KWENYE  ndoto zake za kikubwa  za MCHANA ofisini WAKATI YUKO MACHO, ndoto  zile za uasherati  za kuombea siku moja afanikiwe kupata nafasi ya kufanya dhambi ya uzinzi na MTU mwenye  bomba la matege ambaye atamsalimisha kutoka kwa wanaomfuatafuata  KATIKA MAISHA HALISIA wenye miguuu imenyoka kama fito  za kujengea kigenge cha kuuzia nyanya  na vitunguu MIKESE,- na ni miguu iliyonyoka NDIO  kitu ambacho kwake ndio KASORO.:-(Swali:
- Unafikiri kama mtu ana BONGE la pua kubwa kiuwiano na SURA YAKE imsaidiayo kupumua vizuri na kudaka harufu bwelele NZURI au tu za chooni, huyo anakasoro ya pua au ni yule mwenye pua UJAZO wa kawaida AMBAYO HAINUSI VIZURI na inazingua upumuaji , na ambayo inasababisha astukiwe ZAIDI kwa masikio kama Rais Obama ndio mwenye KASORO ya PUA?
- Hufikiri KASORO kwa asilimia kubwa ambazo SI UGONJWA  zilalamikiwazo ni za KUBUNI kwa aliyenacho ndio maana mwenye aibu kwa midomo minene hushangaa watu wakilipia kujazwa midomo ili LIPS zijazie tako?
Ndio,....
.... kuna watumiao nyenzo ya KUHUKUMU WENGINE katika kuepusha wengine kuwachunguza yao yaliyojaa KASORO.
Na kwa bahati mbaya au NZURI, kwa ung'eng'e wanadai `` IT WORKS!´´,...
... kuhukumu wengine KWA KIPINDI KIFUPI inasaidia sana kukwepa KUJIHUKUMU wewe MWENYEWE.
Swali:
- Wakati unahukumu wengine si unakumbuka kama kuna lako lihitajilo hukumu wala haliondoki na liko tu lakusubiri?
- Je, umefanikiwa kuhukumu mtu leo na kusahau kujichunguza yako yenye KASORO kwa muda leo?
Hebu Aaliyah abadili hali ya hewa kwa kurudia- One in a Million
Au tu Aaliyah adai -Age ain't nothing but number
 
  
 Posts
Posts
 
 




0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment