Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UMESHAWAHI kujiuliza ni nani alitafsiri BIBLIA kwenda KISWAHILI?

>> Friday, January 15, 2010

Huwa natamani sana kuwajua walio tafsiri BIBLIA kwenda KISWAHILI kwa mara ya kwanza,...

.....NA,....

.....huwa natishwa na maneno haya:

``This Biblica translation of the Bible is for the Tanzanian dialect of the Kiswahili language, which is primarily used in the United Republic of Tanzania. This translation uses an informal language style and applies a meaning-based translation philosophy. It was translated consulting the biblical languages and was completed in 2006.´´
- kila nikiendea BIBLIA ya online ya BIBLICA



Kinitishacho sana ni maneno: ``.. This translation uses informal language style and applies a meaning-based translation philosophy. It was translated consulting the biblical languages...´´



Swali:
  • Wanamaanisha nini katika sentensi hiyo?
  • Hiki kitu huwezi kuona kuwa kama wakitafsiri biblia WAKATOLIKI biblia HIYOHIYO itakuwa tofauti na ikitafsiriwa na WASABATO?

  • Kwa kusoma sentensi hiyo huwezi kustukia misingi ya hoja ya nguvu ya Waislamu ya kutotaka KORANI itafsiriwe kwa lugha nyingine?
  • Si unakumbuka tafsiri za kitu mara kedekede huathiriwa na mtu atafsiriye kitu?


Sitanii!

NISAIDIE Mheshimiwa kwa hilo kama unajua vizuri historia ya BIBLIA ya KISWAHILI na niakinani walihusika kuitafsriri hasa kama umeshastukia ki- meaning-based translation philosophy,- Mtakatifu Simon Kitururu akitafsiri BIBLIA kuna watakao kuwa na wasiwasi na dini zao.:-(


TUKO PAMOJA!

.... na moja kwa moja ngojea FELA KUTI abadili hali ya hewa KIJIWENI kwa kushauri- Let's Start


Au tu GEORGE NOOKS alete pambio- How Great Thou Art

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 11:09 am  

hapa na nami ninahofu zaidi! japo labda naweza ishi bila kutafsri biblia

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP