Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa hata SAMAKI aringe vipi BADO ukweli uko palepale kuwa ana SHOMBO!:-(

>> Friday, January 29, 2010

Samaki weye kisura, na kwa ladha ni mtamu
Napenda yako sura, na kukugida mtamu
Kwa protini kinara, kukukaanga na hamu

Ila samaki kipenzi, we una harufu mbaya!:-(


Samaki we unanuka, vundo lako sina hamu
Harufu yako kunuka, shombo lako sina hamu
Na samaki unanuka, kwenye ya wali karamu

Hivi samaki kwanini, wanuka ila mtamu?:-(


Na siri yako nyingine, weye una miba ndani
Nje wapendeza vingine, kwa miba kuficha ndani
Wanikumbusha wengine, roho zao watu ndani

Kweli kipenzi samaki, wanuka bila kuvunda.:-(


Swali:
  • Hivi unapenda kunukia harufu ya samaki?
  • Hakuna mtu KIROHO akukumbushaye samaki, kwa nje tamu ukimjua undani roho miba?
  • Unafikiri samaki angenoga zaidi kama angenukia kama manukato?

  • Unafikiri ni kwa nini samaki hunuka kama samaki?
  • Unauhakika Mtu ananukaje ikiwa watu hutofautiana hata harufu ya ushuzi?
P.S
Ndugu Samaki;...
Kwa kunuka mwanawane ,....
..... wewe wanipagawisha. :-(


NIMEACHA na ni wazo tu dhaifu HILI Mheshimiwa NA halikuhusu kama wewe ni MPENDA SHOMBO YA SAMAKI na kwahiyo USIKONDE!

Nakutakia IJUMAA na WIKIENDI njema MKUU!


Hebu Keith Sweat abadili kwa kurudia -TwistedAu tu Peter Tosh apoze mchecheto na kukumbusha- The poor man Feels itAu tu Peter Tosh akumbushe tu kuwa tupo watu kama mie Simon Kitururu tunaugua- Reggae Mylitis

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 6:19 am  

Mkuu umeandika beti tamu za samaki ukasahau kuna mtu kama Askofu mie nanogewa kwa utamu wa tenzi za samaki.
Kingine hiyo 'reggae mylitis' nami ninayo.
Mkuu big up sana.

Simon Kitururu 2:25 pm  

@Askofu Fadhy: Tuko pamoja!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 9:52 am  

hata shemji ananuka japo mtamu as sio Simoni

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP