Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama huna HESHIMA ulijuaje?

>> Friday, January 08, 2010

Jamii NI MPAKA ijue HUNA HESHIMA ndio itakupa adhabu .



Matokeo yake wanajamii wengi WASIONAHESHIMA wanaishi kinafiki katika kujaribu kutunza muonekano ambao JAMII inautambua kama ni HESHIMA!


Chakusikitisha,..
..... JAMII wakati HUO inaadhibu mtu inaweza kuwa ndio yenyewe HAINA HESHIMA.



Ila kwakuwa JAMII kwa ujumla ndio itafsiriyo kitu HESHIMA ni nini ,...
... ni rahisi kuwa kwa hilo la HESHIMA jamii yenyewe ni KIPOFU.



NA,...

.... JAMII ni watu na katika watu kuna mtu ambaye ni kiini katika MTAZAMO mzima wa HESHIMA ni nini.:-(



Kwa hiyo mtazamo mzima wa nini ni HESHIMA kwa kizazi cha BAADAYE mhasisi yawezekana ni WEWE usiye na heshima LEO.:-(


Ndio ,...

...kwa hiyo mtazamo MZIMA kama ULE wa ``KIZAZI cha sasa hakina HESHIMA kwa WAKUBWA´´ ni moja ya ishara kuwa HESHIMA ni kitu kilicho kwenye MWENDO na HAKIKUSIMAMA na muelekeo wa HESHIMA iendako kimtazamo ni MTU ambaye anaambukiza WATU mpaka kufikia kuwa ni mtazamo wa JAMII.


NA chakusikitisha ni kwamba MTAZAMO wako wa ni nini HESHIMA wa jana, LEO taka usitake kuna uwezekano umepitwa kwa SIKU moja ingawa mpaka ustukie kuwa yote udhaniayo sio HESHIMA yanaonekana ni KAWAIDA kama sio mfikiriaji utastukia hilo ikifikia PALE idadi kubwa ya JAMII IFIKIRIAYO KAMA WEWE itakapostukia.:-(


Swali:
  • Kwani kutoa kitu kidogo au RUSHWA TANZANIA unafikiri ilianza ghafla tu?


Ndio,...
....KAMA HUNA HESHIMA na UNATAKA KUTAMBULIWA KAMA MHESHIMIWA chakusikitisha ni kwamba WALA USIHOFU kwa kuwa KWA WATU WENGI inatosha WASIPOJUA tu kuwa WEWE HUNA HESHIMA!:-)


Ndio ,...
....KWA kuwa JAMII ni kipofu katika iliyoamua ndio KWELI YAKE, unaweza ukafikiri UNA HESHIMA mpaka UTOKE kwenye JAMII YAKO ,...

.....na hapo ndio utashangaa kumbe KUSONYA wazazi wako ni kukosa HESHIMA, au tu kustukia karibu wote UWAITAO WAHESHIMIWA katika JAMII ya waheshimiwa ni VIONGOZI waiibiayo serikali waiongozayo ulikuwa unakosea maana nzima ya HESHIMA ni nini.:-(


Swali:
  • Kwani HESHIMA ni nini?
  • Mkuu hivi tukikusachi moyoni/ROHONI unaheshima au una heshima kwa kuwa unajulia muonekano na kauli za HESHIMA?
  • Kwani weye kama MTANZANIA hujisikii ulikuwa huna heshima kwa ng'ombe kabla ya kukutana na MHINDU wa INDIA?

  • Kwani unafikiri ni MTANZANIA ngapi haziheshimiwi mpaka na serikali yao ukilinganisha na jinsi MBWA waheshimiwavyo kama watu ULAYA na MAREKANI?






Swali zaidi katokori:
  • Si umeshastukia kukosa heshima HASA katika JAMII MASIKINI huwa kunawahathiri zaidi WANYONGE na walalahoi?

NDIO ,....

... kwa shingo upande labda NIKIRI,....


.... kama hali yenyewe ndio hii DUNIANI labda HESHIMA ni MUONEKANO na usikikavyo.

TUSIPOSHUHUDIA vitendo vyako vya kinyama na KUSIKIA kauli zako zisizo na heshima labda unahaki ya kuwa ndani ya JEDWALI la WENYE HESHIMA Mkuu!:-(


Nsikutishe MWANIWANE hili ni WAZO tu Mheshimiwa KIKORE!



Ngojea USA for AFRICA katika KUJIANDAA kujisaidia kujisikia vizuri kwa kusaidia AFRIKA tuwachungulie katika- DAY O


Au tu HARRY BELAFONTE mwenyewe adai-DAY O

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Koero Mkundi 2:52 pm  

HII NAJUA UMENISEMA MIMI..........................................................................................................

Yasinta Ngonyani 3:10 pm  

MMMMhhhh! mie simo kabisaaaa ila kuna kitu hapo!!!

Simon Kitururu 3:17 pm  

@Da Koero: Wala mwaya!
@Da Yasinta: Mhhh!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP