Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

ELIMU ni moja ya SABABU kila mjinga umjuaye ni mjinga HIVYO!:-(

>> Wednesday, January 13, 2010

Unawezakubisha ,...
.....lakini kila mtu KAELIMIKA!:-(



Na kwa bahati mbaya ,...

....elimu IWEZACHO SANA KIRAHISI ni kuubadili tu JINA ujinga waidaiwaye AMEELIMIKA kuliko kitu kingine chochote kielimu.:-(


Na kwa bahati mbaya zaidi,...

... elimu yaweza kumzidishia UJINGA aliyeelimika ndio maana inafikia kuanzia aliyeshiriki kugundua BOMU la nyukilia, WAUANAO kwa KUTUMIA ELIMU iwashauriyo wapigane vita kuzuia mabomu ya nyukilia yasisambae, aliyegundua kondomu na asiyeitumia makusudi kondomu ukiwachunguza utagundua wote KIVYAO wameelimika kitu......



Swali:
  • Wakati unamtambua aliyeelimika huwa unakumbuka kufikiria ni mangapi hajaelimika?
  • Si unakumbuka duniani , elimu itumikayo zaidi ni elimu dunia ambayo kila mtu anaweza kujiuliza hivi katika elimu hii hivi Profesa ni nani?
  • Unafikiri kuna aliyeelimika kwa yote?
  • Hivi baada ya kuelimika bado ulijistukia hujui kabla ya kupata uzoefu ?


NDIO,...
.... inajulikana kuwa kwa kawaida wale idaiwao WAMEELIMIKA SANA kwa mara nyingi huajiriwa na iaminikao NA wengi hawajaelimika sana hasa katika elimu ya kipimo ni VYETI ambao kwa bahati mbaya ndio waanzishao mahali watu WENGI wapaitapo KAZINI.


NA,...
....kisahaulikacho ni kwamba ELIMU ya yoyote YULE kuna eneo IMELENGA ndio maana Mganga wa MENO kwa kuwa na elimu kuhusu MENO si lazima anajua kutibu kichaa kama mwenye elimu ya VICHAA.

Na kibaya katika elimu,....
... kuna WAIJUAYO kwa nadharia WENGI kuliko kwa VITENDO ndio maana WADAIO wanajua matumizi ya kondomu katika kuzuia UKIMWI ni WENGI tu kama ambao ni rahisi kukiri kupata gono kuliko UKIMWI.:-(

Swali:

  • Unafikiri ni wangapi tujuao kufikiria tutakacho kuandika na kivitendo hatupatii kuandika ?
  • Unafikiri ni wanasiasa wangapi wasioijua siasa kivitendo ambao unafikiri ni wanasiasa?

  • SI unakumbuka kila mwenye elimu umtambuaye kwa hilo kuna kitu unamuunganisha nacho kielimu kama tu yule ufikiriaye mjinga na hajaelimika UMUUNGANISHAVYO na kitu fulani tu ambacho kwako kinapiga kelele kuwa hajaelimika ingawa UKWELI NI KWAMBA anaweza kukufundisha kitu?


NDIO,...
.....ELIMU ni aina ya kubagua nini unataka kukiacha ubongoni kiendeleze UJINGA au tu kibakie hakijaelimika,....

...na kuna uwezekano mkubwa aheshimiwaye kwa KUELIMIKA inategemea sana na ujinga au UDHAIFU wa mtu katika swala zima la ni nini KUELIMIKA na ni nini katika ubongo wake KIMEELIMISHWA.:-(



Swali:
  • Unafikiria kielimu hakuna profesa wa uchawi kwa kuwa wewe sio mchawi?
  • Unafikiri elimu imekuzidishia ujinga upi wewe ?
  • Umeshawahi kusikia kuwa kila isemekanaye kaelimika kuna ajiongezeacho KUTAKA katika asivyohitaji?

NI wazo tu HILI Mkuu!:-(


Hebu twende Afrika dauni anda , Penny PennY alete- IBOLA



Au tu PENNY PENNY alete na - Makantia Jive

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP