Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UDHAIFU wa -``Kama tamu KWANGU itakuaje CHUNGU kwako?´´

>> Thursday, January 07, 2010

[Tahadhari: Tararira hii ina ZIGZAG kimtiririko!:-(]

MAKALI ya mitazamo binafsi ya BINADAMU ni moja ya sababu DUNIA ni tamu na KILA LIMTU liamualo kuhangaikia penzi litapata MPENZI,......kwa kuwa hata mtazamo wako BINAFSI ule wa kuwa JAMAA LIMELOSTI a.k.a HALINA MPANGO ,...


... kwa BINTI YAKO mtazamo wake binafsi WA SWALA HILO HILO unaweza tu kuwa

- ``JAMAA halina MAKUU ndio maana linavaa MIDABWADA na halipendi MAGARI ndio maana kila siku linatembea kwa MIGUU hata DALADALA halipandi YANI kwa kutopenda makuu YANI´´ , ...

` `.... na LINAPENDA MAZINGIRA HILO na ili kutunza mazingira haliogi kwa SABUNI halafu napenda kweli harufu yake ya asilia ya jasho lisilokauka vizuri la uvundo wa KIKWAPA chake kizuri,.... ´´


.....-``YANI NALIPENDA HILO wewe we ACHA TU!´´[sentensi hii ya mwisho imebaniwa pua!:-(]

Swali:

 • Si unajua hata HITLER alikuwa na poozeo limpendalo mpaka kufa kwa jina Eva Anna Paula Braun?
MAKALI ya mitazamo binafsi ya BINADAMU ni moja ya sababu DUNIA ni chungu kwa kuwa WASIKIAO UTAMU mara nyingi hawachunguzi kama utamu wao si matunda ya wasikiao UCHUNGU.Swali:
 • Kwani mara ngapi wakati unafurahia utamu wa UBWABWA huwa unafikiria atokwavyojasho na kuwashwa MVUNA MPUNGA ?

Kwa kifupi ILE KITU TAMU KWAKO mara nyingi ili iwe TAMU KWAKO kuna uwezekano umeiachanisha kifikira na swala zima la ni KWA akina NANI tamu kwako ni CHUNGU KWAO.:-(
Na MAKALI ya MITAZAMO binafsi ya BINADAMU hasa waliojiaminisha kuwa wao WANAAKILI na wafikiriavyo na WAISHIVYO ndivyo sahihi,....

....KIRAHISI, ....

......husababisha DUNIA izidi kuwa JINGA kwa IDAIWAO WANAAKILI , BUSARA, NA WANAUZOEFU WA MAMBO kung'ang'aniza kuwa KWELI waijuayo kivyao kwa kuwa KWAO iliwasaidia kufanikiwa waamini hiyo ndio KWELI PEKEE HATA MAISHANI MWA WATU WENGINE kwa kusahau kuwa DUNIANI kuna uwezekano kabisa hakuna WATU WAWILI wanogewao hata UBWABWA sawasawa.Swali:

 • Unafikiri kama wewe HUWA unanogewa UBWABWA huwa unaogewa sawasawa na MAMA YAKO mpenda UBWABWA?
 • Kama wewe ni MTANZANIA na umeshawahi kusimuliwa stori za JKT, unafikiri ushawahi kusikia stori mbili zilizofanana za jinsi WANAJKT uliokutananao wakidai walikuwa wanatoroka JESHINI au tu kazi sawasawa?
 • Unafikiri ijulikanao WANAAKILI hajuilikani hivyo kwa kufuata mfumo huu tu wa sasa na tukibadili MFUMO tutastukia kuwa kuna bonge la UJINGA katika wenye akili wa sasa ndio maana lenye akili sana SASA HIVI DUNIANI ukichunguza labda liko bize linatengeneza bomu.
 • Au unafikiri mwenye akili sana sasa hivi anafanya nini?

Pia kuna SAIKOLOJIA nyuma ya wenye wazo - ``KAMA SIFANYI MIMI NANIHII basi na NYIE WENGINE MSIFANYE!´´ ambayo chimbuko lake kwa wengi ni UBINAFSI ingawa inaweza ikafichwa katika hoja ya ASIYETAKA wengine wafanye ya ``NAWALINDA wengine kwa kuhakikisha nisichokiamini na kutokifanya basi na WENGINE MSIFANYE´´.Swali:
 • Kwa kuwa hunywi pombe si ndio inaweza ikawa ndio hoja yako kuwa na wengine WASINYWE ingawa upendavyo ngono hovyo bado inawezekana ikawa bado hutaki na mke wako nae hovyo aonjwe?Kwa kifupi wala usingehitaji kusoma yote niliyoandika hapa kwa kuwa nilichotaka kusema ni :

-Kama tamu KWANGU inaweza ikawa ni chungu kwako na BONGE la BUSARA na AKILI kwako labda lingenitia uvivu wa kuwa na hamu ya kuwa HAI KESHO.:-(
Swali:
 • Unafikiri ni wangapi hasa walioko kwenye dini ziahidizo PARADISO baada ya kufa ambao TAMU YAO imetiwa utamu na ahadi tu za PARADISO ila bila hilo TAMU yao ni BONGE la CHUNGU?

 • Na si unakummbuka tamu kwako wakati unanjaa inaweza ikawa wala hainogi kama umeshiba na unajilazimisha kula?

...na MAKALI ya mitazamo binafsi ya BINADAMU ni moja ya sababu DUNIANI hakutaisha VITA kwa kuwa tu hata jinsi ya KUMPENDA MUNGU wa AMANI NA UPENDO ,....

..... iaminikao ndio wenye AKILI wanatofautiana MITAZAMO BINAFSI ya kusambaza dini au tu KUMTETEA MUNGU.
Swali zaidi kiduchu:

 • Kwa mtazamo wako ushawahi kumtetea MUNGU?
 • Unadhani Mungu muweza yote kwa mtazamo wako anahitaji mtetezi BINADAMU?
 • Huwa unafikiria kama tamu KWAKO inautamu gani KWANGU?
NI WAZO tu hili MHESHIMIWA na usikonde!


Tutulie na WASELA

Kwanza-CLOUDS Production enzi hizo za mwanzo wa Bongo FLEVA- Msela
Pili- Dopa MAN- Msela


Tatu -Mangwair -Msela
Nne- Nuru THE Light- Msela

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP