Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati NYANYA inaringia VITUNGUU!

>> Friday, January 08, 2010

Nyanya kwa maringo yake na KUJISHEBEDUA mbele ya KITUNGUU yaweza kudai INA sura nzuri zaidi kwa kuwa NYEKUNDUU halafu INABONGE la SHAVU nyororo kuliko KITUNGUU!


Swali:

  • Si unakumbuka lakini KITUNGUU kinalika peke yake kama tu NYANYA ilikavyo peke yake halafu bila CHUMVI?





Halafu NYANYA inaweza mpaka kujishebedua kwa jinsi ipatavyo JUA na haifukiwi udongoni karibukaribu na mavi ya kuku a.k.a MBOLEA kama kitunguu na INAPATA JUA tokea utotoni,....


...kwa bahati mbaya KWA BINADAMU ,....

... hata kabla KITUNGUU hakijaanza kufunua sketi ili kuisuta NYANYA kwa kujishebedua kisa ili iwe nyekundu haihitaji MKOROGO ingawa ina NDONYA angalau MOJA na siajabu kuikuta na CHUNUSI ikiingiliwa na VIMELEA,....


... na hata kabla KITUNGUU hakijaanza kutamba kwa jinsi iwezavyo kuliliza mpaka limtu KUBWA ,...



... Kwa BINADAMU aonacho na AFIKIRIACHO katika vyote vya NYANYA na KITUNGUU labda ni viungo tu vya MWIDU, chunga, MAHARAGE au sana sana kachumbari,...




..... na LABDA hata sikumoja hajawahi kufikiria kuna uwezekano NYANYA MSHUMAA inajiona yenyewe ni babukubwa kuliko NYANYA MVIRINGO na nyanya zote kwa pamoja zina ugomvi na VITUNGUU .




SASAAAAA....
Swali katokori:
  • Wakati huu ambao UISLAMU na UKRISTO vinalumbana unafikiri MUNGU anafikiria nini?
  • Wakati Wakristo na Waislamu wanalumbana kuhusu nani ataenda mbinguni unafikiri BUDDHA anafikiria nini?
  • Wakati wake wawili wa Rais ZUMA wa Afrika KUSINI wanagombana unafikiri Rais Zuma huwa anafikiria nini?



NI WAZO TU HILI Mkuu , na labda VITUNGUU na KABICHI , NYANYA na MABIRINGANYA wala havina UGOMVI kama UISLAMU na UKRISTO na ugomvi wa mambo uko KICHWANI TU mwa wanadamu HASA katika tafsiri ya MAMBO!:-(

Nakutakia IJUMAA na WIKIENDI NJEMA Mkuu angalau uwe na uhakika wakupata choo MHESHIMIWA!



Tararila HII ilitunga mimba mawazoni baada ya kusoma articles kadhaa zenye uhusiano na MALAYSIA katika :

``Minister in the Prime Minister's Department Jamil Khir Baharom today urged websites and blogs to refrain from carrying anything negative on the issue of the use of the word 'Allah' by the Catholic weekly magazine, The Herald.´´


Hebu tubadili hali ya hewa kijiweni kwa kupitia Cuba MONGO SANTAMARIA arudie- Me and U baby




Au tu Ray Barretto na MONGO SANTAMARIA waingie kazini kwa kitu- CONGO BONGO




Au tu turudi AFRIKA kwa mara nyingine OSIBISA watulize kwa -WOYAYA

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP