Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

BINADAMU ananuka!(wazo lililopinda)

>> Tuesday, May 26, 2009

Bin- ADAMU hata baada ya kumaliza kuoga,...
..... huwa bado ANANUKA!

Kama unabisha muulize MBWA anamtambuaje mmiliki wake hata asiye na bahati ya kunuka kikwapa!


Na Bin-ADAMU akishakufa ,...
.... ndio huacha KUNUKA kama unaamini akigeuka udongo huacha KUNUKA!

TUKIACHANA NA HILO,...

....ni kweli ,...
....DUNIA INANUKA!

Kama hujastukia labda ni kwa sababu umeizoea ndio maana hushangai kwanini mtoto akizaliwa na kunusa dunia cha kwanza AKIPUMUA ni kulia!

Na labda moja ya visababishavyo DUNIA KUNUKA ni BINADAMU KUNUKA na uozo wa miili ya binadamu kabla haijaacha kunuka!

Swali:
  • AU?
  • Baada ya kunisoma BADO unauhakika umewahi kukutana na binadamu anayenukia na asiyenuka?

Ni wazo tu Kingunge, USITISHIKE!

Ngojea BEN WESTBEECH aongelee kuhusu kesho katika- So Good Today

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 6:29 pm  

Nuka nuka nuka:-)

SIMON KITURURU 5:51 am  

:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP