Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama kuna tofauti ya MATUMIZI ya LIBINADAMU lililopendeza yaliyotofauti na ASIYEPENDEZA!

>> Saturday, May 16, 2009

Labda KUPENDEZA kumezidishiwa sifa zisizostahili,...

.... sijui kwa nini!


Mpaka unaweza kusahau ni UTU sifa unaostahili,...
... na unajua ni kwa nini!


Kama USHAPENDEZA,...
..... halafu iwe nini...
......wakati wajua mwisho wa siku utaishia kwa kutopendeza,...
... sasa waringia nini?



Kwani tukisema UMEPENDEZA,...
... unafikiri tunamaanisha nini...
....wakati wajua kupendeza kujichoni mwa akupendaye,....
..... na kwa siye wengine weye maning'ining'i, au unabisha nini?



Kwani matumizi ya aliyependeza na asiyependeza,..
... tofauti yake nini...
...wakati wote wafaa katika utengenezaji wa mimba,...
..... asifiwayenawe anacha zaidi nini?



Ukifikiria sana , dhana ya KUPENDEZA ni mtindio wa akili,..
... hapo ndio utajiuliza; hivi binadamu wenye akili huwa wanafikiria nini?



Kama bin-adamu ajua maisha na uhai huishi ndani ya ulio uchi mwili,.....
.... dhana ya kupendeza kwa kujisitiri ,yasababisha mtu amtoe uhai mtu kwa nini?



Mahitaji ya mtu kwa mtu hayako kwa alivyopendeza mtu,..
.... au wafikiri uchi na ukiwa uchi haupendezi nini?



Na kupendeza kwa Kigogo ni tofauti na kwa Kibena,..
.... Je wafikiri Mmasai asilia ukipendeza na bichikoma anaona nini?
Swali:

  • Unakumbuka ni udhaifu kujisikia vizuri kwa kupendeza?
  • Unakumbuka ni kukiri mapungufu wakati unajisikia umependeza?
  • Ukipendeza unafikiri umependeza ili ufae kwa matumizi gani?
  • Kwani usipopendeza unauhakika hailipi?

Ni wazo tu Kingunge na NIMEACHA!

Hebu basi twende tena Kameruni Richard Bona atusaidie wimbo uitwao- - Ekwa Mwato


Au tubaki tu Kameruni Manu Dibango alete tena kibao - Africa....

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 7:24 pm  

Mada uliyotoa ya kupendeza ni kali. Ukiitafakari sana unaishia kupotea!

Simon Kitururu 8:52 pm  

@Mkuu Chib: Siutani!:-(

Yasinta Ngonyani 2:24 pm  

Kweli kabisa Chib mi nishapotea kabisa. Simon:-(

Simon Kitururu 4:42 am  

@Yasinta: :-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP