Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Uwezekano wa KILA KITU UJUACHO kuwa SI SAHIHI!

>> Monday, May 11, 2009

USAHIHI wa kitu maarufu ni ule waaminio wengi wadhaniao ni SAHIHI!

Ukiwa pekee sahihi hukawii kuchekwa hasa kama wewe si maarufu katika jamii hii iwasikilizao waliozoeleka kusikilizwa mpaka imefikia matumizi ya kondomu anaulizwa Papa Benedikti wakati inasemeka hajawahi kufanya ngono a.k.a kutumia koni / kitumbua.

Lakini,...
.... USAHIHI wa kitu ni sahihi hata kama wahusika hawaamini ni sahihi na wanajishughulisha KUSAHIHISHA. Na kuishi siku kwa siku katika KUSAHIHISHA labda hilo ndilo liitwalo MAISHA YA BINADAMU.


Na mara nyingi ni kweli,..
....Kwa BIN-ADAMU usahihi wa kitu ni ule UDHANIWAO TU KUWA NI SAHIHI pale WAHUSIKA wadhaniapo wanajua nini ni SAHIHI.


Binadamu ni mabingwa wakudhania wanajua nini sahihi kwa mfano:

  • Dunia ilikuwa na umbo la meza na mtazamo huo ulikuwa sahihi na wabishi mpaka wakauawa mpaka na KANISA, mpaka baadaye kidogo ilipohakikishwa kuwa dunia ina umbo la kinyeo a.k.a mduara( samahani kwa matumizi ya lugha ya faragha).

  • Na labda Bin- adamu huamini kalaaniwa kwa kuumwa hata kipindupindu, mpaka akistuliwa kuwa staili ya kunya au usafi tu huwa unachangia gonjwa na dawa ya kipindupindu ipo. Na labda ni kweli UKIMWI itaaminika ni laana mpaka utakapo pata dawa na kugeuka kuwa kama gono baada ya dawa kugundulika na uasherati KUFANIKIWA kuibua kaka yaye UKIMWI ambalo litakuwa ni gonjwa ambalo ukimchekea tu mwenye kaka yake UKIMWI basi makende na nyeti yatakuwa ya shadaka KAKA YAKE MDUDU na sio kama sasa hivi ambapo ni mpaka uhangaikenaye.

  • WANYAMWEZI, WAPARE; WACHAGA, WANDENGEREKO,..... nk yalikuwa ni mataifa na ilikuwa ni mtazamo sahihi, mpaka ilipogunduliwa dhana ya kuyaita kuwa ni makabila, na hilo ndilo mpaka sasa hivi huitwa SAHIHI.

  • Tanzania haikuwa nchi na ilikuwa ni SAHIHI, mpaka waaminio katika dhana ya UINCHI walipodai ni NCHI ingawa asilimia tisini ya wananchi wake hawajawahi kufika hata mpakani mwaTanzania na Kigoma, na wakifika hawajui kuwa huu ni mpaka na kama unabisha waulize Wamasai.
  • Na labda ukitaka mifano zaidi jaribu kufuatilia nakadhalika kadhaa saba na nusu zilizo sahihi!


Na,..
....kuna uwezekano kabisa USAHIHI wa UJUACHO utaujua baada ya kufa au katika zile dakika za mwisho kabisa wakati unaingia UVIVU WA KUPUMUA na MOYO kuanza kukosea KUDUNDA KWA kufuata miondoko ya SEBENE, ndipo kuna lijamaa ulilodhani maishani mwako yote linakupenda, linaweza kuingia ujasiri na KUKUNG'ONG'A kabla halijakutakia kheri ya kufa itakayofuatwa na msonyo mnene na wenye uzito wakutosha huku likichekelea afadhali unakufa.

Kuna uwezekano pia kuwa USAHIHI SI MUHIMU na chamuhimu ni KUISHI ukisahihisha na hayo ndiyo MAISHA.


NAACHA TOPIKI hii lakini ingawa ,...
......LABDA kunamambo udhaniayo ni SAHIHI mpaka unagombana au unanipandishia sketi kunisuta( kitu ambacho napenda hata ukiwa hunisuti mwanawali weye ), we yape tu muda MAMBO HAYO na YAnaweza YAKAKUSHUSHUA na kukusuta.

Na labda ,...
.....ni muhimu kwetu WOTE kuyapa muda MAMBO ili YATUSHUSHUE tujue KUNAUWEZEKANO KILA TUJUACHO si SAHIHI.

Na labda,...
.... maisha yote haya wakati tunamfikiria Mungu Mbinguni, ukweli ni kwamba tunaishi ndani ya TUMBO la MUNGU kama tu minyoo idhaniavyo tumboni kwako BIN-ADAMU ni ulimwengu na ukienda haja kubwa, minyoo hudhania kuwa imepelekwa jehanamu baada ya kustukia kijoto cha kwenye tanki la mavi(samahani kwa matumizi ya lugha ya faragha), na ukinya kichakani minyoo wanadhani wamepelekwa mbinguni.



Swali:
  • AU?
  • Unauhakika na mtazamo wako kama unadhani wangu si sahihi?

DUH!
NIMEACHA!
Kumbuka ni moja tu ya wazo KINGUNGE!
Nakutakia tena SIKU KIBONGE!

Hebu twende kidogo tukamsikilize JAJI Saudi Arabia aamue -tumchape kidogo kofi mwanamke....



Au turudi tu kwenye DANCE tujikumbushe staili - ELECTRIC BOOGALOO


Au tucheke tu ....

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 9:02 pm  

kazi kwelikweli Duh!

Serina 9:23 pm  

Una kashughuli. Pitia kwangu kwa maelezo zaidi.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP