Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NYUMBA hii inalindwa na MBWA KOKO!

>> Wednesday, May 20, 2009

Kama unafuga mbwa BONGO, ni kawaida KUMSINGIZIA kuwa ni MKALI.

Hukawii kukuta mpaka NYUMBANI kwa kijeba mpaka na kibao wamekuandikia;''JIHADHARI MBWA MKALI!'' kama vile ni kweli mwizi atumiaye akili ni tatizo mbwa mkali.

Lakini kama tu WAZAZI wa Libinadamu wadhaniavyo kuwa watoto wao ni spesho kuliko mtoto wa jirani, labda mbwa wa kwenye tangazo mbwa mkali ni mbwa koko na akibweka ni katika kujihami kwake tu na mapopo.

Swali:

  • Hivi bado hujawahi kufikiria kuwa labda kama Tanzania inalindwa na mbwa basi huyo mbwa ni KOKO?
Kumbuka lakini kwa wajanja nchi za magharibi jibwa koko kuwanalo ndio ujanja!

Na haki yanani tena utakuta Profesa wa lilesomo unaloamini linahitaji akili za hali ya juu ndio yuko bize anaongea na jibwa lake na anaamini linamuelewa kuliko binadamu na urafiki na bin-adamu haupi tena kipaumbele ukizingatiwa dogi linahitaji KWALITI TAIMU na usisahau linahitaji kwenda kutembezwa ili liende haja kubwa na lazima likijisaidia uzoe kinyesi.

Kumbuka tu tamaduni na mazoea ndio vyaweza vikawa vinasababisha hustukii mbwa koko ni koko .:-(

Na kama wewe ni miongoni mwa waogopa mbwa, LABDA mbwa koko ni MKALI!

NIMEACHA wazo!
Siku Njema!


Ngojea Tracy Chapman adai- Give me one reason



Au tu Lenny Kravitz adai-I belong to U

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mzee wa Changamoto 5:04 am  

Lahaula

chib 1:51 pm  

Mbwa koko!! Mbona huwa hafugiki huyo!!

Simon Kitururu 4:02 am  

@Mzee wa Changamoto: :-(
@Mkuu Chib: Mbona watu wanafuga mpaka fisi?:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP