Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

LABDA kuhangaikia KUJUA UKWELI hakuna tofauti na kuhangaikia KUJUA KUDANGANYA vizuri!

>> Wednesday, May 27, 2009

Kafuraha kakujiridhisha NDIO CHANZO cha kuhangaikia uridhike!


Si UKWELI ndio ukusababishao utake kujua UKWELI , bali kafuraha KAKURIDHIKA na ahueni ya kuwa sasa unajua ndicho kikuhangaishacho na kukugalagaza utake kujua UKWELI.

Tatizo ni,...
... hata ukitaka kudanganya halafu ukafanikiwa kudanganya vizuri, mwili huachia kemikali a.k.a homoni a.ka kibaruti kile kile kilichokufanya uridhike kwa kujua UKWELI.

Kwa kifupi,..
.. labda KAFURAHA kakusema kweli tu kwa madoido KANA UTAMU sawa na KAFURAHA ukapatako kwa kumwaga bomba la uongo VIZURI!

Swali:

  • Hivi si bado kuna uwezekano KAUKWELI kako bado kana KAUONGO?
Na,...
... LABDA mpe tu shughuli BINADAMU ili umcheleweshe kufikiria ukweli au uongo wa lini ni siku yake ya kufa.

NA labda MTU akiwa bize na maisha , UKWELI hauna tofauti na UONGO katika umuhimu wakufanya wewe kama BINADAMU ustukie unaishi.

Na labda ndio maana,...
.....UONGO na ukweli vina mchezo wakufuatana hata mpaka chooni, ukizingatia vingi wadanganyanavyo watu huambatana na shughuli ziambatanazo na jinsi ya kupata uhakika wa maakuli usaidiao kumpatia mtu choo!:-(


DUH!


Swali:
  • AU?
NIMEACHA na samahani kama unastukia ujinga zaidi ya busara katika hili MHESHIMIWA!

Nakutakia siku Kibonge na mapumziko Bwanyenye!


Au ngojea CHRISETTE MICHELLE akuongelee katika- Love is U..


Au tu BAABA MAAL airudishe AFRICA kwa kibao-Souka Nayo(I will follow U)

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 11:23 am  

Ha ha haa, ukweli na uongo kukufuata hadi chooni!!!!

Fadhy Mtanga 10:00 pm  

Duh! Heshima yako mkuu.

Yasinta Ngonyani 11:37 am  

Kazi kweli kweli:-( Simon ni MUHIMU NINA UJUMBE WAKO. TAFADHALI

malkiory 9:51 pm  

Kitururu huyo homoni au kemikali uliyozungumzia kwenye artiko yako, unaweza kunidokezea jina lake? kama sijakuelewa vinginevyo nadhani utakuwa ukizungumzia homoni aitwaye adrenaline.

Simon Kitururu 5:49 am  

@Fadhy na Chib: :-)

@ Yasinta:Ntakutafuta leo kwa vyovyote.

@Malkiory:Nilikuwa nazifikiria feel-good endorphin hormones.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP