Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ujumbe wa mahubiri ya askofu leo USIOENDANA na vitendo : ''USIDOKOE MBOGA!''

>> Wednesday, May 06, 2009

Fanya nayosema sio nayotenda, kuna waungwana ndio washaurivyo.


UTAAMBIWA:

  • Usizini.
- kama uletewavyo ujumbe kutoka kwa Askofu-mchungaji au na sheikh mzinzi.

  • Twendeni gezaulole tukajishughulishe na kilimo.
- ujumbe wa bwana kilimo kutoka chuo cha kilimo asiye na shamba na ni chekibobu asiyependa tope wala kwenda shambani.


  • Miye sipendi wanafiki
-ujumbe kutoka kwa mnafiki.

  • Acha ujinga
-ujumbe kutoka kwa mjinga.

  • Usifanye nakadhalika kadhaa
-ujumbe wako na nakadhalika.



Na ni kweli labda binadamu huwa wanakuambia wanachofikiri ila wanaondoa kipande kikubwa cha wanachoamini na kufikiri ambacho ndio unaita UMEWAFUNANIA ukikuta wanakigina sehemusehemu.



UJUMBE wa mahubiri ya usidokoe mboga pia yanaweza KUKUSHANGAZA kwa kukutia nyege za kudokoa mboga kama tu ukimdaka aliyekuhubiri usifanye uasherati ATAKAVYOKUSHANGAZA ukimfumania ANAKULA KITENGO a.k.a tunda.

LAKINI bado wakati unamtumbulia macho anaweza kutumia sentensi maarufu na kukukata kauli kwa kukukumbusha:
  • ''FANYA nayosema na usiige VITENDO VYANGU NAVYO TENDA! Ubarikiwe sana mpendwa tutakutana basi kwenye BIBLE STUDY!:-(''


NA kama WASEMAVYO WATANZANIA wangekuwa wanatenda, TANZANIA INGEKUWA NI NCHI ILIYOENDELEA NA INAFUATA UJAMAA na KUJITEGEMEA MPAKA LEO, halafu wala wasingekuwa wanamuhisi Rais Mkapa na Rais MTARAJIWA LOWASSA kuwa labda kuna kitu wamedokoa ambacho mwalimu wao MJAMAA a.k.a NYERERE alikataza .


Kama wasemavyo watu wangekuwa wanatenda kweli , labda sasa hivi ungekuwa na LIMCHUMBA zuriii ambalo uliliona kwenye gazeti na unamapesa BWELELE , mwenyewe umetulia ukifyonza aishikirimu kwa juisi ya UKWAJU.

Swali:
  • Unauhakika ungefanya yote unayosema ungekuwa hai?
  • Hivi wewe na mimi sio wanafiki kwa kukana hamu ya kitendo hadharani kama ni kitendo fulani ?
  • Hivi unasema zaidi au unatenda zaidi?
  • Hivi kusema sio kitendo?

MIE TOPIKI imenishinda na labda nachosema sifanyi kwa vitendo!:-(

Namuacha tena SHIHAN azungumzie - FLASHY WORDS


Au tena SHIHAN azungumzie -This Type of LOVE



Au tu Babyface arudishe kitu katika -I'll make love to you & end of the road

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 8:48 pm  

Kasi kwelikweli:-(

Simon Kitururu 7:30 pm  

@Yasinta: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP