Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama unachojaribu NI kupendwa ,basi kunauwezekano UNAHONGA!

>> Monday, May 11, 2009

Pendo ni hongo,..
.... ukinipa pendo wanishawishi nikupe pendo mwanawani.


Pendo kama Pesa lanunulika,...
..... na vyote thamani zake ni mpaka kwa watu ziaminike zinathamani na hazinyonyi kama kupe.


Pesa aina ya noti ni makaratasi na si pesa kama anunuaye na anunuliwaye haamini manoti ni pesa.


Na hapa tunaweza tukabishania tu aina aina ya hongo utumiayo katika kutaka upendwe na kuanzia peremende umpayo mtoto wa binamu nyama ya hamu, sadaka kanisani, mpaka kumpa mtu sehemu zako za faragha pale faragha ,vyote ni hongo na labda walengwa tu ndio tofauti.


Na uchoyo ni bonge la hongo kama linamlenga mlengwa atakaye kustukia kwa kuwa ndio weye pekee umnyimaye, hasa ukikumbuka kuna wazidishiwao kupewa mpaka hawakumbuki burungutu tamutamu ni lipi katikati ya maburungutu tamutamu yaliyopoteza ladha kwa wingi wa utamu .

Nachojaribu kukutonya ni,..
....KWA ujumla kila kitu kinafaa kuhongea na ni staili tu za kuhonga zimleteaye sifa atoaye peremende na lawalawa nyama kwa watoto na zimleteazo achunwaye BUZI sifa mbaya mbele ya wachunwao buzi kwa staili nyingine kama ya kuogeshwa na maji ya karafuu nyumbani, zote katika kuhonga zinalenga KUDAKA atensheni, a.k.a kuhusishwanishwa na UBAB K .

Na hongo lako hata la kujitia mnyonge kwa apendaye WANYONGE ladaka mahaba ili ujistukie babu kubwa na kunasa hata kama kwa mtazamo wako hilo si hongo.

Swali:

  • Unauhakika hakuna utoacho kwa nia ya kupendwa hata kama ni lifti kwenye baiskeli yako ya foneksi ?
  • Kwani unafikiri hongo ni nini?



Na hondo ya pendo ya weza kuwa ni kupenda na kama makaratasi kwa imani huaminika yana thamani na ni manoti-pesa, basi tukiamini ,pendo ni pesa.

Na magimbi yaweza kuwa ndio msaada kwa pendo la leo litamanio mihogo kwa chai na kwa bahati mbaya chai ipo pekee bila kitafunio , na hatuna pesa.


NAACHA WAZO!
Lakini,...
...LABDA uaminivyo ni kweli na kuna haja za MTU kutaka kukubalika au hata kupendwa .

Na,...
....katika kujaribu kudaka upendo unaweza kujikuta unahonga na hongo yako inaweza ikawa ni kukaa tu vibaya kila jamaa likipita wakati unachagua mchele.(samahani kwa wazo la faragha)


Lakini,....
... LABDA kwetu wote , kama unachojaribu NI kupendwa na wenzetu ,labda dawa ni kujaribu kupenda tu WENZETU.
Swali:
  • AU?
  • Unauhakika pendo lako halina masharti kama udaivyo weye mwenye roho nzuri ?

Kumbuka hili NI moja ya wazo tu hapa Kingunge na NIMEACHA!

Nakutakia SIKU Kibonge!


Ngojea Kassav walete kibao- Sye Bwa


Au nimuachie Dany Engobo azungumzie- Pambapamba..

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 9:04 pm  

Simon acha vituko/fujo:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP