Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama Rais Jacob Gedleyihlekisa Zuma na wale tuwaheshimuo wangekuwa wanatumia kweli KONDOMU!

>> Tuesday, May 12, 2009

Tupendao HIPHOP tusingemshangaa P.DIDDY kwa kumzalisha mtu akiwa katikati ya kampeni ya MTV ya kuhamasisha matumizi ya KONDOMU.

Tusingemshangaa mgombea URAIS wa Marekani JOHN EDWARDS kumpa mimba msaidizi wa kampeni yake ya Urais ili amshinde Obama wakati anasafiri na mke.

Tusinge mshangaa PAPA WA KIROMA a.k.a Papa BENEDICT akichukuliwa kama mshauri mkuu wa maswala ya KONDOMU wakati yeye bikira na ujuzi wake wakuvaa kondomu ni ziro au ni ule wa kuvalisha kidole gumba cha mkono kondomu katika kuwaza inakuaje jidume linaweza kuvalisha kajidume kake mpira yote ikiwa ni katika kuwania kikojoleo.

Tusingemshangaa Rais ZUMA kwa kuwa na watoto wa mke na mke mtarajiwa wapishanao mwezi na kudhani akioga anaepusha UKIMWI.


Tusingeshangaa ni kwa nini kampeni za matumizi ya kondomu Afrika zinachukua muda mrefu namna hii na mpaka sasa tunafundishana jinsi ya kuvaa soksi, wakati barani chakula hakitoshi.


Swali:

  • Unauhakika ni kweli Mungu aliumba wanadamu ili wagundue Kondomu na madawa na sio aliwaumba ili wazaliane na kufa upesiupesi dunia isijae kirahisi kiisidingo?

  • Unauhakika na asilimia za utamu ambazo kondomu inashea nawe au huvai kwa kuionea wivu tu?


NIMEACHA!

Nakutakia siku KIBONGE Mkuu!

Ngojea nimuachie tena MATONYA aongelee -Taxi BUBU...



Au tu James Dandu a.k.a Mtoto wa DANDU adai-- Sina Makosa..

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP