Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UTULIVU wa kichwa KICHAA!

>> Tuesday, May 12, 2009

Ndani ya mtu,...
..... kichaa ni KICHWA

Akitulia mtu , ....
......kilichotulia ni KICHWA.




Kichaa akitulia bado ni kichaa,.....
....na akifanya fujo kichaa atahakikishia tu umati kuwa yeye kichaa.

Cha ajabu aaminikaye si kichaa akifanya ukichaa kwa kufanya fujo ,...
... atajulikana kwa fujo na hataitwa kichaa.

Na asiyeaminika ni kichaa hata katika kuonyesha penzi akilamba vikojoleo ,...
... bado itaonekana anatoatu staili ya penzi na huo si ukichaa.

Lakini ukimwangalia vizuri kichaa,...
... waweza kusahau kujiuliza kwanini unadhani yeye ni kichaa,...
...hasa katika dunia hii kichaa ambayo mpaka wasio vichaa ilikuonyesha jamii kuwa si vichaa wanafanya ukichaa.


Na kichwa na jinsi ya kubalansi yaliyo mukichwa,...
.... bado kisipotulia kichwa cha ajabu unaweza usiitwe na walimwengu kichaa.

Ingawa maadili na vitendo,..
...mwanawani ukimuangali tayari ni kichaa.

Katika dunia hii kichaa,..
...unauhakika nani katuliza kichwa wakati kazungukwa na ukichaa?

Na katika dunia kichaa mtu akitulia,..
... unadhani utulivu huo wa mtulivu atuliaye kwenye ukichaa si ukichaa?

Hebu angalia wasifiwao kwa akili,...
.... na ugunduzi wao wa vitu viharibuvyo dunia na kugeuza watu vichaa!

Hebu nenda kuwachungulia waomba Mungu,...
... utajiuliza hivi Mungu hajiulizi kwa nini kaumba vichaa?

Hebu watazame waumini walio wengi,...
...washafikia mpaka kumtetea Mungu muweza yote asiyehitaji utetezi,

... na kuchukia na kumua binadamu mwenzao mnyonge kama vile vichaa.

Hebu leo muangalie tena vizuri umuitaye mheshimiwa,...
..... unadhani huyo hata kwa kukubali uheshimiwa yeye si kichaa?

Hebu muangalie na ajifikiriaye mzuri na kwa juhudi ajaribu tingisha tako,..
....au hata ajifikiriaye ni mbaya sura kama tako, wadhani hao kwa wazo hilo si vichaa?

Na yule udhaniaye ana akili,....
......umesahau yasemekana wenye akili sana ndio huonekana vichaa?


------------------------_____________________------------------


NIMEACHA na kumbuka ni moja ya wazo tu Kingunge!

Ngojea nimuachie WAZIRI MKUU wa ITALI afanye kitu cha kiheshima kwa vitendo...(Warning usiangalie kama mtoto au utakwazika)


Au tuangalie Wajamaika wakimkarimu mtalii....(Warning: dalili za uasherati, usiangalie kama mtoto au utakwazika.)
...


Au niache tu ujumbe kwa wamuaminio Nabii Issa a.k.a Fundi seremala Yesu.

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:11 am  

Simon:-( kazi kweli kweli mi nimeridhika na hiyo ya ukristo bwana. We kweli ni bwana mawazo

Simon Kitururu 7:57 am  

@Yasinta: Umeridhika na hiyo kwa sababu wewe Mkristo?

Yasinta Ngonyani 1:48 pm  

Hapana kwa sababu mimi ni mimi Yasinta

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP