Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KWA wanaojisahau na SIRI na kuendelea kuishi wakitunza SIRI ZILIZOEXIPAYA!:-(

>> Tuesday, May 19, 2009

Mara nyingi ni ghali kutunza siri yako hasa kwa kuwa asilimia kubwa za siri za watu zitunzwazo zilishaexipaya longitaimu!:-(

Na kwa kuwa wote tunajua jinsi gani watu ni wasahaulifu, labda siri yako isingekuwa wewe binafsi unaiendekeza iendelee kuwa siri , siye wengine tungelishasahau uhusiano wako na hiyo yako siri.

Siri kiboko!

Inaweza ikasababisha unogewe na hata visivyovitamu kwa kuwa tu unavilia migombani kisiri na kama ungetandikiwa mkeka ungelistukia zamani unogewavyonavyo vimechacha kwa mbaali na vinanuka kwa kuwa si siri kuwa ni kweli vinakosewa kuoshwa.


Na,...
.... umuhimu wa siri mara nyingi unazidishiwa sifa zaidi kuliko unavyostahili.
Matokeo yako unaweza kunogewa na kutunza siri huku kumbe kama tungeijua hiyo siri wala tusingeioanisha na huo udhaniao ni umuhimu.


Swali:

  • Unauhakika siri zako bado hazijaexipaya na unaendelea kuzitunza kwa mazoea tu?
  • Hivi weye sio miongoni mwa wadaio kwa kuwa siri yako anajua mtu mmoja tu a.k.a rafiki mpendwa, basi hiyo unadhani bado ni siri?

Kumbuka, kutunza siri ghali kinoma!

Inashangaza lakini kwa jinsi watu wasivyostukia ughali wa kutunza siri ingawa hao hao ni mabingwa wa kunyemelea vitu vya chee!:-(

Kumbuka kama siri yako ni kuwa unamakengeza, kama nakupenda basi wewe kwangu KAMWE HAUNA MAKENGEZA na ukiniuliza ntakuhakikishia kuwa hayo ni macho malegevu na kwa kurembua katika mahaba hauwezekani.

Swali:
  • AU?
  • BADO unauhakika na umuhimu wa siri yako?

NIMEACHA na kumbuka ni moja ya wazo tu Kingunge!
Nakutakia siku KIBONGE na kila la kheri kwa kupafekti sanaa ya kuficha siri!

BAADAYE basi KINGUNGE!

Ngojea tu Lupe FIASCO amkaribishe mtu katika - Welcome Back Chilly



Au tu Ricky James azungumzie -COLD BLOODED

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 7:09 pm  

Simon kuna siri umeificha nini:-(

Simon Kitururu 4:39 am  

@Yasinta:Sina uhakika!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP