Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hamu ya MKE WA TATU!(simulizi iliyopinda)

>> Thursday, May 14, 2009

Mke wa kwanza amemzoea,...
.. na ubunifu kaacha , kashazoea.



Na hata kwa harufu chooni ajua ni yeye,...
... na mpaka kwa harufu ajua alichokula, kamzoea.

Na hata akimdanganya hanuki kikwapa ajua amdanganya,..
... ingawa haachi kuulizia ya kikwapa au ya atingishavyo singida dodoma, kazoea.

Sijui ni kwa mazoea,....
.... ghafla mwanawani wa nyumba ya jirani ukifumba macho anasogea.



Sijui mazoea yaua shahuku,....
..... uhakika wa kitu wamfanya asiharakishe kutoka sokoni awahi ile ile faragha aliyoizoea, kaizoea.


Na kama nguo na kitafunio cha chai hubadilishwa,...
... sijui mke wa kwanza asipobadilishwa nayo tuite ni mazoea?


Na labda mme wa kwanza anafaa zaidi kwa porojo,....
..... na wa sita ananoga kama gari jipya kwa tendo na kitengo , hujamzoea.

Na kama unahamu na nyama ya kuku,..
..... kunauwezekano nyama ya bata si tamu , hujaizoea.

Tatizo la mazoea,...
.....ukianza kubadilisha itafikia unatakakubadili visivyobadilishwa na unafanya kwa mazoea.

Na mazoea ni mabaya,...
..... na hata kuumizwa roho waweza zoea.

Na labda hamu ya mme wa pili,....
..... hainatofauti na ya mke wa sita kama ukizoea.

Na kabla hujabadili chuo,...
.... jiulize kama kuna umuhimu au ni yako tu mazoea.


Na katika kujizoelesha mazoea,...
..... waweza kujikuta umejilimbikizia wakati yote ya muhimu katika utamu yalikuwapo kwenye ya mke wa kwanza uliyoizoea.


NIMEACHA!
Kumbuka ni moja tu ya wazo!
Ngojea twende Zimbabwe kwa Oliver MUTUKUDZI adai -NDAKUVARA.....



Au tu tupitie tena Zambia kukutana na K'Millian adai-NIZAKUKONDA

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:38 am  

Kumbuka mazoea hujenga tabia. Ni rahisi kufanya jambo na kile ulichokizoea kuliko kipya:-(

Simon Kitururu 3:13 pm  

@Yasinta! Kweli kabisa!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP