Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama kuna KISASI, labda KISASI cha KUKU angetaga mayayi VIZA!

>> Tuesday, May 26, 2009

NDIO,....
..... labda unafikiri UMEMKOMESHA!

Swali:

  • Hivi utamu wa kisasi unadumu dakika ngapi?

NDIO,...
.....alikufanyia, na unafikiri roho haitatulia usipo mparura na utafaidi ukimfanyizia!
Swali:
  • Hivi tukibadili jina la KISASI na kuliita URODA ukimfanyia kama alivyokufanyia hivi nyie hamtazalisha MTOTO MAUMIVU ambaye atakuwa nimaumivu yenu wote wawili ?

NI kweli,..
....KISASI kwake ni KISASI kwako!

Na hata ukibisha ,...
... inasemekana kisasi kizuri ni KUSAMEHE!
Swali:
  • Unafikiri unaweza kujilazimisha kusamehe?
  • Unafikiri utamu wa kisasi ni nini?

Na,..
...kusamehe ni sanaa,kusamehe ni taaluma na kila mtu ni bingwa katika hii fani ingekuwa hatuchagui ni nini cha kusamehe!

NDIO,....
.....NAAMINI Bin-adamu huchagua vya kusamehe na mara nyingi hudai hawajasamehe leo baadhi ya vitu ambavyo walivisamehe tokea mwaka juzi ila hawajastukia tu kuwa walisamehe kwa kujiamisisha kuwa mpaka leo vina leta MAANA.


UKINIULIZA mimi ntakuambia KISASI NI UGONJWA WA AKILI na kama unabisha, hebu tazama kuanzia mkao wa alipizaye KIASASI hata kabla ya kushuhudia VITENDO vya alipizaye KISASI!:-(

Ni wazo TU Kingunge na kuna uwezekano nakudanganya!
KASIRIKA basi na tunza kisasi kama unadhani inalipa!:-(

NIMEACHA wazo KINGUNGE!

Ngojea Ali Kiba adai tena- NICHUM

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP