Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UKIJUACHO ni kama tu jinsi ya kwenda haja ndogo, kama unakijua vyakutosha ULISHAACHA KUKIFIKIRIA wakati UNAKITENDA hicho!:-(

>> Tuesday, May 19, 2009

Kama kuna kitu unakijua, basi hicho kilishaacha kukuumiza kichwa!



Na labda,...
... kama kuna unachokifikiria, KUNA UWEZEKANO hukijui bado hicho!


Na kama unafikiri unakijua kitu,...
... lakini bado kinakufikirisha, LABDA labda kunamapungufu ya ukijuavyo au kinakasoro hicho .

Na kasoro ya udhaniacho unakijua inaweza kuwa ni mtazamo wako wa kudhani unakijua:-(


Na unachokijua unaweza kusahau kipo,...
... kwa kuwa hukifikirii tena hicho.

Na hata kama ukifikiriacho ni MUNGU,...
... kuna uwezekano unafikiria ya MUNGU kwa kuwa kuna kitu kuhusu MUNGU hujui bado hicho.

Na ungemjua MUNGU,labda SHETANI na vya shetani yasingevutia na kukudaka hivyo!:-(

Swali:

  • Unafikiri kuna mtu hapa duniani unauhakika anakujua?

  • Unauhakika hakuna limtu nyumba ya jirani zuuriii NA kwa kuwa unalijua unasahau kulistukia kuwa ni zuri na linafaa kwa matumizi yako ya kuumiza mtu roho?

Unaweza kunibishia,.....
.... LAKINI ni kweli mambo yako unayoyajua kama vile kutawaza, huwa unafanya bila kuyafikiria .

Na unachokifikiria, bado hujakimasta ndio maana kunasiku unajistukia mnyonge na katika kujaribu kusawazisha unyonge kuna WATUTISHAO na watakavyotudhaniye wanajua na katika prosesi wanatuboa.

Swali:
  • Au?
  • Unauhakika kwanini unafikiri unajua wakati wadaio kujua hata kufinyanga tonge la ugali kunasiku hudondosha tonge?

NIMEACHA!
Kumbuka ni moja tu ya mtazamo na wazo Kingunge , usitishike!
Ngojea Marvin Gaye abadili hali ya hewa kwa kibao - Lets get it on



Au tu aendeleze simulizi za uasherati katika- Sexual Healing

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP