Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UBWABWA wa MSIBANI vs UBWABWA wa HARUSINI!

>> Tuesday, May 05, 2009

Tatizo la UBWABWA wa harusi, unahitaji uuvalie ULIMBWENDE na probulemu za UBWABWA wa MSIBANI , wahitaji staili za mkao wa MAJONZI!:-(

Kuna wengi watakao kuambia kuna kautamu tofauti kapatikanako kwenye pilau ya Msibani au Harusini ambako hakako kwenye pilau iliyopikwa kwa ajili yako nyumbani.

Afadhali hata na pilau ya kimada ambayo hata kama ni mbichi hutastukia kwa sababu ya kuharakisha kuila ili mvue nguo upate muda wakuwahi nyumbani bila kustukiwa.

Na wapo watakao kuambia hustukia MSIBA kutokana na harufu ya ubwabwa na sio KILIO kutokea kona ya sita.

Lakini ukitaka kustukia jinsi gani ubwabwa wa msibani au harusini unamvuto tofauti, mtafute aliyezamia msibani iliuone umahiri utumikao katika kuhakikisha pilau linanoga.

Ngojea nikupe kastori ka enzi za High School Mazengo DODOMA......

''Nisikufiche chakula kilikuwa kibaya ile mbaya pale shuleni mpaka ikifika siku ya ubwabwa ingawa ubwabwa wenyewe ulikuwa kama ugali , shughuli yake mesini lazima uistukie maana hakuna aliyetaka kumisi siku ya ubwabwa.

Halafu eti wajanja walikuwa wanaonekana wajanja kama wakipata mchuzi wa maharage wenye dalili za mafuta tuliokuwa tunauita TOP LAYER.

Basi bwana pale Mazengo kulikuwa na akina mama watuuziao , Vitumbua, maandazi na Chapati. Hawa walikuwa wanasababisha mpaka baadhi ya watu wale mpaka ada, ikiwa yote ni katika kukwepa kula chakula cha shule.

Na kwa bahati mbaya naweza kusema kwa uhakika kuwa kuna miezi ilikuwa inafika karibu kila mtu kachacha, na labda hata nauli shule ikifungwa hajui ataitoa wapi.

Kipindi hiki kili saidia kuwapa watu ujasiri wa kuzamia misiba na harusi kwa mafanikio.''
STORI yakijinga IMEISHA hapa .

AU ngojea nirudie!

Tatizo la UBWABWA wa harusi inabidi uuvalie suti na wamsibani uukalie mkao wa MAJONZI.
Basi hapa ndio kazi ilipo katika shughuli nyeti ya kuzamia SHUGHULI!

Unaweza ukajikuta unalilia mtu mzima MSIBANI kumbe aliyefariki ni mtoto.

Afadhali ya kuzamia harusini unaweza ukaonyesha juhudi mpaka ndugu za mme wanafikiri wewe ni ndugu ya mke na ndugu ya mke wanafikiri kuwa wewe ni ndugu ya mme , kama sio tu pande zote wanadhani wewe ni A LONG LOST NDUGU, wakati wewe unasubiria mlo HUKU huachi kupiga chabo upande wa jikoni.

Halafu kuna staili za kula msibani kama unataka ubahatishe kukuta nyama kwenye pilau.

DONDOO ya jinsi ya kula UBWABWA msibani:
  • Safari ya mkono ya kwanza kwenda kwenye sinia ni yakutafuta nyama!
  • Ikiwezekana nenda na kachumbari yako kabisa kwenye mfuko wa rambo.
  • Kula haraka tu ukikumbuka kuna kitu kinaitwa baadaye kitakachokupa muda wakufikiria kuwa umeshiba au UMEVIMBIWA.
NJAA NISHAI kweli!
Halafu nasikia eti WAAFRIKA tulitawaliwa na TUNATAWALIWA kwa sababu wengi wetu ni WAVIVU halafu tunasikia NJAA HARAKA!:-(


NAIKATISHIA hii stori hapa nikupe muda wa kwenda kujenga TAIFA.
Swali:

  • Umestukia ilivyo noma nazungumzia maswala ya ubwabwa msibani na sio marehemu msibani?
  • Unauhakika marehemu huwa anakuwepo msibani?

  • Unauhakika msibani unamfikiria marehemu?
  • Unauhakika sababu zako za kwenda harusini sio kwa sababu ulilazimika tu kuchangia harusi wakati libwana harusi linakuudhi na bado harusini ninamcheki demu wako?
  • Kama umeoa au kuolewa lini utafuata fasheni mpya ya KUDIVOSI?
  • Unauhakika hauko harusini mwanadada wewe kwakuwa unamuonea wivu bibi harusi?
  • Unauhakika hauko harusini kwa kuwa bado unamtamani bwana au bibi harusi ambaye alikuwa mpenzi au mpenzi mtarajiwa?
DUH halafu eti kunawadaio wanajua sababu za wazamiaji kujifunza na kuzoea KUZAMIA SHUGHULI kwa ujasiri na maarifa!:-(

NIMEACHA stori kwa leo basi KINGUNGE , kajenge tu Taifa!

Pata basi MAFIKIZOLO


Au ngojea CCM isifiwe, idawie Nyerere aliharibu nchi na kadhalika kadhaa wa kadhaa saba na nusu ,yote ikiwa nikatika kuendelea na siku......

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Born 2 Suffer 6:43 am  

Simon unakumbuka mbali sana mwanawani wakati ubwabwa ukizubaa ukageuka ukirudi hukuti kitu sahani tupu jeupeee..!! Lakini sasa ubwabwa gani huwa ni mtamu katika msiba au wa harusini?

Simon Kitururu 6:56 am  

@Mzee wa Taratibu: Nadhani unanoga zaidi wa msibani.

Ubwabwa wa harusini unaweza ukauonea aibu kutokana na uwepo wa vimwana macho yagololi, mashavu mimba ya panya waliopendezaaa na kuvutia halafu unahisi kama wanakuangalia vile unapigaje tonge.Si unajua tena akina dada kwenye harusi wote ni wazuri ndio maana inadaiwa na wenye busara tusichague mchumba harusini?Hahahaha:-)

Yasinta Ngonyani 4:55 pm  

Simon:-( Mmh kazi kwelikweli

Simon Kitururu 7:31 pm  

@Yasinta:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP