Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Swala la busara za KUJIHAMI na MTONGOZO!

>> Wednesday, May 27, 2009

Labda,..
... kama unajihami na mtongozo basi weye UNATONGOZEKA!


Lakini,...
...inasemekana KUNA watu inabidi uwakwepe KUWASIKILIZA usipotaka kuwakubalia MTONGOZO!

Kuna watu hata kama hukubaliani nao kisiasa,...
.... ukiwapa muda wa kuwasikiliza unaweza kujikuta unawapigia kura wakati bado hukubaliani na siasa zao.

Kuna njemba mwanadada akijilogo alipe muda limng'ate sikio hukawii kustukia mwanadada anavuta majani kwa kukosa tikitaka ya maneno ya kukataa zaidi yakutoka mbio a.k.a baruti!

Nachojaribu kusema ni kuwa kuna watu unaudhaifu nao na ushakaa mkao wa kukubali na kikusitishasho ni woga wa kuwa ni dhambi, itauma, watu wengine watasemaje kama ukikubali kula bata wakati kwenu chakula ni nguruwe.

Nachojaribu kusema,..
... LABDA sio ukali wa kauli ya mtongozaji ikufanyayo upende CCM, bali ni mkao wako wa kuzimia CCM ndio usababishao hustukii hoja za Mchungji MTIKILA kama zina kuna KIPELE!


Na ukimkalia mkao wa kumkubali Mwanadada,...
... hata akibinya chunusi inavutia na kukutia mshawasha.

Swali:

  • AU?

Sikatai lakini kuwa kuna watoaji Mtongozo kama akina Nyerere ambao wakikukalisha chini na kukuambia a.k.a kukupiga siasa kuhusu UMUHIMU wa chama kimoja utakubali, na wakidai vyama vingi bomba unakubali na wakikaa kimya bila kukujibu unajazia mwenyewe wanafikiria nini hata kama hawafikirii kitu na fikira zimekwama!:-(

Narudia ,...
... LABDA ukijihami na mtongozo basi weye unatongozeka!

Na atongozekaye kunauwezekano alikaa mkao wa kutongozwa na atongozaye!


Swali:
  • AU?
NIMEACHA!

Ngojea Papa Wemba alete za-Ye TE OH


Au to tujikumbushe Geto BOYS waongelee - 6 feet Deep

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 7:58 pm  

Mm kweli kuwaza kazi. Ila Simon:-(

SIMON KITURURU 5:50 am  

@Yasinta: Kazi kwelikweli!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP