Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika kuangalia tena UTUMWA wa kuwa na TABIA NZURI!

>> Friday, May 08, 2009

Tabia ni mazoea!

Tabia nzuri ni ile jamii imeizoea hata ikiwa ni ile ikubalikayo katika jamii , hata kama ni ile ya kulamba makamasi kama jamii inaamini huleta afya.

Swali:

  • Unauhakika ni kwa nini kwa mtoto kulamba makamasi kwake mtoto sio tabia mbaya?
  • Unauhakika watoto wasingekatazwa kulamba makamasi utotoni halafu wakakua na taaluma hiyo, unafikiri kusingekuwa na MISS KULAMBA MAKAMASI siku hizi au tu wakumbwa wasinge sifiwa kwa staili zao za kulamba makamasi ukubwani kwa mrija?
  • Unauhakika na sababu zaidi ya kinyaa kwa nini konokono hummezei mate Dar wakati Ufaransa ni chakula cha wajanja?
Na,...
.... kuna uwezekano kabisa WEWE au MTU a.k.a BIN-ADAMU atastukia anatabia nzuri kwa kusifiwa na watu wengine kuwa anatabia nzuri. Kabla ya hapo TABIA ni TABIA tu ndio maana kila mtu akiwa chooni pekee kila tabia ni nzuri kama hujiumizi.

NA ukishasifiwa unatabia nzuri , ndio mwanzo wakujiwekea mipaka ya wapi mwisho wakupekecha ili isitokezee kwenye uwigo wa TABIA MBAYA.

Ukiweka mipaka, ndio imetoka na ndio mwanzo wakuanza KUJAJI WENGINE kuwa wamezidisha hasa kama wanavuka mipaka ambayo umejiaminisha na UMEAMINISHWA kuwa ndio TABIA NZURI.

Na kumbuka ,...
.... kunatofauti kati ya TABIA NZURI ikufaayo na TABIA NZURI ambayo jamii inaiita TABIA NZURI ingawa inaaminika iitwayo tabia nzuri na jamii ndio itakuletea maisha marefu.
Na,...
....Kuna vigezo visababishavyo uamini kuwa tabia nzuri usifiwayo na kundi ndio bomba kwa kuwa tu binadamu ni vigumu kuishi bila kundi ndio maana anampaka Mwenyekiti wa Kijiji.
Swali:
  • WEWE kama ni MTANZANIA, unakumbuka ni TABIA MBAYA zilizosababisha Mwalimu Nyerere apelekwe shule kwa sababu alikuwa kichwa ngumu ikaamini shuleni ndiko atachapwa viboko?
  • Unauhakika sio jeuri na kichwa ngumu ya Mwalimu Nyerere ndio maana mpaka leo anaitwa Mwalimu na kama hakukuongoza wewe basi alimvua hata uchifu BAbu yako?
Kumbuka,...
..... tabia nzuri ni NZURI kwa wafaidikayo na hiyo tabia ambao ndio watakusifia UNATABIA NZURI.

Na tabia mbaya hubadilishwa jina kama jamii inaanza kuikubali.
Kwa mfano;
  • Uchoyo uunaweza kuitwa kujitegemea.
  • Ngono itaitwa tendo la ndoa.

  • Jeuri anaweza kuitwa anamsimamo mkali.

  • Kujamba kutaitwa ''Kapumua''

  • Wezi wanaitwa mafisadi.
Ok ! Labda haikuwamifano mizuri.:-(
Swali:
  • Unauhakika Tabia nzuri sebuleni Dar-es Salaam Tanzania ni Tabia nzuri Dar-es- Salaam katika sopu opera kwenye TV ambayo siku hizi ndio mwalimu wa taifa la kesho la wana Dar-es Salaam kuhusiana na Tabia nzuri hata katika kujibu ni thong gani a.k.a chupi mwanadada avae chini ya gwaguro?
  • Unauhakika unatabia nzuri au tu kwa sababu katika jamii yako hiyo ni tabia nzuri kwa kuwa katika jamii yenu kunywa Gongo kwa linyama lililonona la Nguruwe ni Ruksa?

Halafu eti bado unashangaa wale wenye TABIA NZURI wafungiao wanawake zao nyumbani kwa matumizi ya starehe za MUME na kwa kuwa ni tabia nzuri!

Halafu unashangaa wengine kwa tabia mbaya wakati nawewe tunakushangaa kwa TABIA MBAYA!
LIONE VILE VIVUUU!


NIMEACHA na kumbuka kama unataka kuishi muda mrefu inasemekana Tabia Mbaya inaua haraka shauri yako!:-(
Kumbuka nawazatu hapa KINGUNGE!


Ngojea nimuachie George Carlin aongelee- The little things


Au ngojea tena George Carlin aendelee kuongelea-Life after Death


DUH!

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP