Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuwa MAARUFU watu wakustukie kama vile GHAFLA umekuwa GENIUS wa kila kitu /Una MIAKILI Kibao na MAJIBU BWELELE !

>> Thursday, May 21, 2009

Sikutanii,...
... hata kama ukipata umaarufu kwa kukaa uchi, GHAFLA mpaka hata maswala ya kilimo kuna watu wataanza kukuuliza wewe ushauri na sio BIBI KILIMO!:-(


Utashangaa nakwambia kuwa mpaka hata apataye UMAARUFU kwa kucheza FUTIBOLI a.k.a KABUMBU , kwa washabiki wake , yeye kafuzu na anafaa UBUNGE hata wa BIHARAMULO na kwao mpaka maswala ya KEMISTRI yeye Profesa.

(Ok, labda katika Uprofesa wa Kemistri hapo nimezidisha.)

Na ajulikanaye GHAFLA kwa sababu WAZAZI wake walikuwa wanajulikana KABLA, ndio kabisa kwa umaarufu wa ghafla leo , AKITAKA URAIS kuna watakaodai ANAKWALIFAI.

Swali:
  • Kwani wewe pia sio msikilizaji wa watu maarufu kuliko wale wajuao siri ya kitu umuulizacho maarufu?


Haki ya nani tena,...
... baadhi ya binadamu kwa kuzimia watu maarufu hawakawii kutosita hata kuwagawia sehemu zao za faragha a.k.a PIPI na wakataka mpaka kukushawishi na wewe uamini kuwa Lijamaa Maarufu wanauhakika likijamba hakitoi harufu! ( samahani kwa matumizi ya lugha ya faragha)


SIKATAI lakini,...
.... maarufu mjinga LABDA hujulikana na kumuuliza maswali kabla ya kumzoea ni bomba KWA SABABU ni BOMBA la staili nzuri ya KUJIGONGA kwake!

Tatizo ni pale kujigonga kukizidi na pamoja na kumgawia sehemu zako za faragha unaanza kuamini kuwa anafaa kukuongoza kama KAtibu KATA.
Halafu eti mara ghafla eti nalo LIMAARUFU linaanza kupandisha nyege MPAKA za Ubunge na hata Urais!:-(



Swali:
  • Au?
NIMEACHA wazo!
Nakutakia siku KIBONGE Kingunge na TUTAFIKA TU!


Ngojea Sammy Davis Jr amzungumzie- Mr Bojangles


Au tu Miles Davis azungumzie - Human Nature

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:07 pm  

muhimu sana nakuomba:-)

Yasinta Ngonyani 2:53 pm  

Kaka Simon tafadhali nina ujumbe wako ni muhimu

Fadhy Mtanga 10:43 am  

Da Yasinta unaweza ukadata na hii blOGU hadi ukadhani una ujUMbE muhimu (najaribu kuiga kuwa mawazoni)
ngoja leo nikomee (siyo kufuli) hapa.

Simon Kitururu 5:32 pm  

@Yasinta: Samahani kwa kupotea na nitawasiliana!
@Fadhy: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP