Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Nani ana amani TANZANIA?

>> Friday, May 15, 2009

Ukiwa TAJIRI amani inapotea,...
.... kwa kuwa unadhani tutakuibia ndio kisa cha geti kali huku unawasiwasi tutakuomba.

Ukiwa MASIKINI amani haipo,...
... kwa kuwa unadhani huna na unahitaji kuwanacho kwa kuwa unadhani wengine wanacho na wanakuhisi utaomba.


Ukiwa na DINI amani haipo,...
... kila siku unakimbizana na maandiko na pia hofu za jehanamu au kugeuka bata , labda ndio maana unadini.


Ukiwa huna DINI amani haipo,...
... kila kukicha kunaatakaye taka kukutisha au umhisiye anataka kukutishia jehanamu wakati hapahapa duniani chamoto unakiona.


Ukiwa na NDUGU amani hakuna,...
... kwa kuwa inamaana lazima kama una ndugu utafiwa na ndugu na kifo kinamchezo wakutozoeleka.


Ukiwa huna ndugu amani hakuna,..
kwa kuwa unadhani wenye ndugu kuna wakunyimacho.

Ukiwa na MARAFIKI amani hakuna,...
..... ndio wasababishao umeingia mpaka mikopo uchangie, kitcheni pati, begi pati na kwenye pati unaanza kuingia wasiwasi kama ni kweli udhaniaye rafiki kweli ni rafiki.

Ukiwa Mtanzania amani hakuna,...
... ikiwa mpaka leo huna uhakika na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kama bado unajisikia Mbara zaidi au Mzanzibar zaidi na ni Mtanzania kwakuwa katika kikao hiki si bomba kujitambulisha kuwa unajisikia Mchaga.



NIMEACHA!
Na kumbuka ni wazo tu KINGUNGE, usitishike!


Ngojea tubadilishe hali ya hewa kwa kuangalia jinsi Kigoma wafanyavyo katika - How to Flirt



H-Town wazungumzie- Knockin the boots


Au tu Scarface asifie tabia mbaya enzi hizo katika- Recognize

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 4:49 pm  

Mm hapa kazi ipo kweli

Simon Kitururu 9:02 am  

@Yasinta: Si utani!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP