Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ndani ya JITIHADA za KUJIPENDEKEZA!

>> Friday, May 15, 2009

Ukikosea KUJIPENDEKEZA,..
..... unaudhi!


Ukipatia KUJIPENDEKEZA kwa asiyekupenda,...
...... ni maudhi.

Kwa kuwa kujipendekeza ni maudhi,..
... labda unaudhi!


Lakini MAUDHI ni mpaka ujishughulishe na maudhi,...
....ili yakuudhi.


Na kama unajipendekeza kwa akupendaye,...
.... kuna mbwembwe uzidishazo ingawa sasa hivi anapenda ingawa ni maudhi.

Cha ajabu hakuna binadamu aliyefanikiwa ,...
.... bila mtu fulani kumuudhi!

Na Binadamu asiyefanikiwa,...
.... kunamtu anamuudhi.

Kwa hiyo ,....
..... labda binadamu wote kujumlisha wewe na mimi wanaudhi!:-(

Na wazo hili la kuwa kuna wajipendekezao hata pasipohitaji kujipendekeza,...
.... labda LINAUDHI,...
... hasa kama linakuudhi na wala hayakuhusu MAUDHI!:-(


Swali:
  • Unauhakika kuwa hujihusishi na maudhi ndiomaana YANAKUUDHI?
  • Unauhakika unamjua mtu yeyote ambaye ukimpachansi hatakuudhi?
  • Unauhakika huwa unajistukia kila ukijipendekeza?

Nakutakia Wikiendi Mchelemchele!

Ngojea Mlimani Park Ochestra kwa hisani ya Tizedboy waongelee- Maudhi


Au tu Pablo Francisco aongelee wanamuziki wa RnB...


Au tu Rupee arudishe soca katika- Tempted to Touch

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 4:22 pm  

Kaka Simon kuna mtu kakuudhi au unawaza tu kama kawa yako? Hili ni swali tu

Simon Kitururu 9:02 am  

@Dada Yasinta: Nawaza tu wala sijaudhika!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP