Penzi kiboko mpaka unaweza kuanza kulisingizia vitu!
Likinoga unalisingizia mpaka utamu lisionalo , likiingia uchachu mpaka saizi ya chuchu inakuwa ishu.:-(
Na mara nyingi kikuvutiacho kwa mtu sio kidevu ndio maana husiti ukipewa chansi gizani kuendelea kumpapasa umpendaye bila kumuona vizuri .Na ukipapasa labda hubobei kwenye kidevu.
Na haki ya nani tena, wakati unamtumbulia macho mpenzi, kama unampenda bado huoni kila kitu ingawa yuko mbele yako!:-(
Ndio! Mapenzi sehemu nyingi hufanyika gizani au kwa kuyafumbia macho. Na kama wewe unaweza kufanyapenzi huku unastukia utandu wa buibui kwenye silingibodi , basi ufanyalo sio penzi.
Narudia! Mapenzi sehemu nyingi hufanyika gizani ndio maana mara zote UNAHITAJI MWANGA ili umjue MTU kabla HUJAMTEMA a.k.a KUMUACHA SOLEMBA!
Nachojaribu kusema ni; DAIMA PENZI HUNOGA ukiwa GIZANI na ukianza KUJUAJUA SANA kwa kuwa uko MWANGANI , kwa wengi hilo ndio misingi ya mwisho wa PENZI au kutonogewa na penzi kama juzi. Swali:
AU?
Sikatai! Labda utadai kuwa kwa kumjua sana mpenzi ndio msingi imara wa penzi. Na labda ni kweli kama unaoanisha tafsiri ya PENZI na KUISHI PAMOJA bila MAKEKE na Limtu.
Ndio ! Nakubali kuwa kuna ukweli kuwa kuna aina nyingi ya mapenzi na labda moja ya tafsiri ya penzi ni hiyo yako na unasaidiwa na kutaka kujua kila kitu au kustukia mpaka NDEVU.
Sikufichi!
Inawezekana DEMU wako ana nywele za kutosha tu kifuani a.k.a LAVU GADENI , na sababu za WEYE kutojua hicho kama ni kweli hujifanyi hujui ni kwa sababu YEYE mwenyewe zinamkwaza kwa hiyo anazinyoa ndio kisa hajastukia mpaka leo mapenzi yako ya nywelenywele hata za kiboxi manyoya.
Swali:
Hivi unakumbuka binadamu ana nywele mwili mzima ndio maana limtu lako linatoka jasho mwili mzima na ukilipa chansi lanuka kikwapa?
Turudi kwenye Mwanamke Mwenye ndevu....
Naweza kusema,... ....UKIPENDA umependa na umpendaye akiwa na ndevu hizo ndevu kwako za mpendeza. Swali:
Au?
Kwani UTU na UKE kwako havitoshi?
Kumbuka ,.. ....KAMA WEWE nimtafutaji wa KASORO kila MTU ANA KASORO ingawa katika kasoro ;NDEVU SI KASORO!
Swali:
AU?
NIMEACHA wazo na samahani kama nimekukwaza na kumbuka HILI ni moja tu ya wazo! Nakutakia WIKIENDI KIBONGE na kama unapumzika nakutakia MAPUMZIKO JEMADARI!
Tupumzike tena kwa kujifunza kunyoa sehemu sehemu kwa msaada wa Gillette..
Labda ni kweli KUBWA inatisha ingawa pia kubwa inaweza kupwaya!:-(
Saikoloji ya muogopa makubwa hutegemea kwa muogopaji dogo ni nini.
Ukubwa wa jambo KWAKO unategemea na UBONGO wako ulivyojengeka ili kustukia MADOGO ni nini. Na kwa kawaida unaujenga mwenyewe UBONGO KUSTUKIA MAMBO ingawa pia MAZINGIRA na JAMII inamsaada mkubwa katika kukuponza kwa hilo.
Na sababu za kuhofia kwa kuwa unahisi ni kubwa basi itauma au kukushinda ni jambo lako ULILOJIFUNZA tu!
Na kumbuka,... .... chochote ujifunzacho kinafundishika kukiacha.
Swali:
Unafikiri wakati umezaliwa ni vingapi vilikuwa vikubwa kwako na hukuviogopa kwa kuwa mtoto mwenye umbo dogo na vimekuzidi kimo?
Unafikiri ni kwanini kwa kukua na woga wako wa makubwa umekua?
Unafikiri makubwa ni yapi ikiwa ukweli ya yako makubwa kwa mwingine ni madogo?
Na ,... ....tunajifunza ukubwa wa mambo hata kwa kusikiliza tu wadaio yaliwaumiza.
Lakini katika mchezo wakuumiza labda na wewe ni muumizaji ndio maana mara kwa mara kuna mambo unayastukia kabla hujaumizwana sio kwa kuwa ni marudio ya maumivu.
Kumbuka tu,.. ... TAFSIRI ya ukubwa wa jambo kwako labda kwa mwingine ndio saizi yake na inatosha kabisaaa!
Kumbuka tu,.. ... LABDA ukubwa wa jambo kwa MWIZI ni kichekesho kwa JAMBAZI, ingawa duniani hapa kati ya wezi na majambazi waliotajirika zaidi ni wezi .
Swali:
Hujastukia wanasiasa wako uliowapigia kura?
Na USISAHAU,... .... Udhaniapo ni UDOGO wa jambo ndivyo UMUUAO MWENZIO ambaye kwake SWALA ni kubwa na halina udogo kama tu maumivu USIVYOJUA ukubwa wa maumivu ya mkeo kujifungua au ya mjusi kutoa mimba.
Swali:
AU?
NIMEACHA! Ngojea Rolling Stone wanipe- Satisfaction
Au tu Akon na Michael Jackson warudie-Wanna be Startin' Somethin'
You must include the name of the blogger who bestowed the award on you and link back to the blogger
You must choose a minimum of seven (7) blogs that you find brilliant in content or design.
Show their names and links and leave a comment informing them that they were prized with Honest Weblog.
List at least ten (10) honest things about yourself. Then pass it on with the instructions
1. Mapishi
I love cooking and I've been cooking for myself since 1996.
Sadly, I have never cooked for my mum yet!:-( She still prefer doing everything for me her last-born.:-(
2. Mawazoni.
I think too much about everything.
When I am listening to Ur story, there is a possibility I might be paying more attention to the part of the story you don't intend to tell me with Ur story.
3. Anger
I don't easily get angry when provoked simply because I tend to find comedy in the strangest of places.
4. Appearance
Most people I meet are surprised that professionally I do business and I majored in economics since High School. I guess it is because I don't comb my hair which makes people automatically shift to the artistic mode when they see me.
Well, I do art too as a hobby though! Another thing is, I think my father still struggle to accept my dreadlocks and hasn't forgiven me for not wanting to be a medical doctor because I was very good in science subjects.:-(
5. Wanawake wanaonikuna roho
I have a weakness for smart women. A stupid lady always succeeds to turn me off!
I am polite and try to learn something through the experience though!
6. Technically I am a Muslim
I was once a Muslim and there those who say once a Muslim always a Muslim until death as there is no way out.
In short;
I was born in a family that attends Lutheran Church although my mum is of Mennonite denomination.
Nilifanikiwa kwenda Sunday School mpaka kupata mademu ndani ya shughuli za kanisa hili la Kilutheri Well, niliimba kwaya pia sana tu pale Bungo, Morogoro .
I became a born again Christian through Moses Kulola.
Rastafarianism followed through my own curiosity.
Changed to Islam through my own curiosity.
Doubted God through my own curiosity.
Returned to beliving in God without ties to any religion through the same curiosity of mine and thats where I am right now. Na labda ni kweli Curiosity iliua Paka!:-(
7. Creepy Crawler I hate
Of all the creepy crawlers , I hate scorpions!
I would easily have a sleepless night if U tell me U've seen a scorpion in my room.:-(
Anyway, a glass of Cognac , a shot of Tequila or.. always helps.:-(
8. Relationships
I have problem with love ,and I am not suggesting that I am not loved!:-( The people who I love always think I take more than I give!:-(
I have been dumped once so far and that is when I was form three in Morogoro Secondary.
9. Uvaaji. I tend to over -dress most of the time.:-(
10. Weakness for News
I watch news a lot while feeling guilty that I am wasting time because of loads of BS in what is considered news.:-(
11. How I talk
For a lot of people finds me talking very slow and I get teased a lot for that!:-) .On top of that ....most people who know me find it funny when I rap fast or when I sing with a very low voice that they don't associate with me.:-) Yes I do play music as a hobby everytime I find time....... and it has been Progressive Rock the style I do often for quite sometime now .
12. Inawezasemekana kuwa Mie Mjinga I always think I have to improve on what I know!
Serina umefurahi sasa? Basi ngojea nami niwaonee wengine hawa ambao ni baadhi ya Wanablogu nipitiao kazi zao kwenye zao blogu mara kwa mara, nao ni;
Kafuraha kakujiridhisha NDIO CHANZO cha kuhangaikia uridhike!
Si UKWELI ndio ukusababishao utake kujua UKWELI , bali kafuraha KAKURIDHIKA na ahueni ya kuwa sasa unajua ndicho kikuhangaishacho na kukugalagaza utake kujua UKWELI.
Tatizo ni,... ... hata ukitaka kudanganya halafu ukafanikiwa kudanganya vizuri, mwili huachia kemikali a.k.a homoni a.ka kibaruti kile kile kilichokufanya uridhike kwa kujua UKWELI.
Kwa kifupi,.. .. labda KAFURAHA kakusema kweli tu kwa madoido KANA UTAMU sawa na KAFURAHA ukapatako kwa kumwaga bomba la uongo VIZURI!
Swali:
Hivi si bado kuna uwezekano KAUKWELI kako bado kana KAUONGO?
Na,... ... LABDA mpe tu shughuli BINADAMU ili umcheleweshe kufikiria ukweli au uongo wa lini ni siku yake ya kufa.
NA labda MTU akiwa bize na maisha , UKWELI hauna tofauti na UONGO katika umuhimu wakufanya wewe kama BINADAMU ustukie unaishi.
Na labda ndio maana,... .....UONGO na ukweli vina mchezo wakufuatana hata mpaka chooni, ukizingatia vingi wadanganyanavyo watu huambatana na shughuli ziambatanazo na jinsi ya kupata uhakika wa maakuli usaidiao kumpatia mtu choo!:-(
DUH!
Swali:
AU?
NIMEACHA na samahani kama unastukia ujinga zaidi ya busara katika hili MHESHIMIWA!
Nakutakia siku Kibonge na mapumziko Bwanyenye!
Au ngojea CHRISETTE MICHELLE akuongelee katika- Love is U..
Au tu BAABA MAAL airudishe AFRICA kwa kibao-Souka Nayo(I will follow U)
Na ukikosea unajisikia vibaya,... ... wakati UKIPATIA hata ukisifiwa kujisikia vizuri bado HAKUDUMU!
Na kumbuka;... .. ..kama ulipatia juzi leo ni mpaka ujikumbushe kuhusu juzi ndio kumbukumbu ya ladha na sio ladha halisi ya ulivyopatia ndio hurudi na kukuchekelesha leo.
Na usisahau,.. .... kama ulikosea juzi ni mpaka ujikumbushe ya juzi ndio kukosea kwako juzi kunaweza kukuumiza tena leo.
Kwa hiyo kama ULIPATIA au KUKOSEA JUZI ndio ilitoka hiyo mchezo leo unaanza upya na KUKOSEA au KUPATIA sasa hivi kwenye umuhimu ni utakavyofanya leo.
UKIKOSEA bado watu watajifunza kutokan na makosa na kama unatumia akili usitishike na wababaishwao na KUSIFIA KUPATIA TU.
KUPATIA kwaweza kukawa ni CHANZO CHA UZEMBE hasa kwa vigezo vya kwa kuwa leo UMEPATIA!
KUKOSEA mara zote ni CHANZO CHA MAARIFA hasa kama UNAHIARI ya kujaribu tena hata kama UTAKOSEA TENA!
Swali:
Kwani wewe ni mara ngapi huwa unakosea makusudi?
Naweza kusema,.. ....KOSEA mwanawani kama nia yako sio KUKOSEA! Swali:
AU?
NIMEACHA na kumbuka MWANIWANI hili ni moja ya WAZO TU!
Labda,.. ... kama unajihami na mtongozo basi weye UNATONGOZEKA!
Lakini,... ...inasemekana KUNA watu inabidi uwakwepe KUWASIKILIZA usipotaka kuwakubalia MTONGOZO!
Kuna watu hata kama hukubaliani nao kisiasa,... .... ukiwapa muda wa kuwasikiliza unaweza kujikuta unawapigia kura wakati bado hukubaliani na siasa zao.
Kuna njemba mwanadada akijilogo alipe muda limng'ate sikio hukawii kustukia mwanadada anavuta majani kwa kukosa tikitaka ya maneno ya kukataa zaidi yakutoka mbio a.k.a baruti!
Nachojaribu kusema ni kuwa kuna watu unaudhaifu nao na ushakaa mkao wa kukubali na kikusitishasho ni woga wa kuwa ni dhambi, itauma, watu wengine watasemaje kama ukikubali kula bata wakati kwenu chakula ni nguruwe.
Nachojaribu kusema,.. ... LABDA sio ukali wa kauli ya mtongozaji ikufanyayo upende CCM, bali ni mkao wako wa kuzimia CCM ndio usababishao hustukii hoja za Mchungji MTIKILA kama zina kuna KIPELE!
Na ukimkalia mkao wa kumkubali Mwanadada,... ... hata akibinya chunusi inavutia na kukutia mshawasha.
Swali:
AU?
Sikatai lakini kuwa kuna watoaji Mtongozo kama akina Nyerere ambao wakikukalisha chini na kukuambia a.k.a kukupiga siasa kuhusu UMUHIMU wa chama kimoja utakubali, na wakidai vyama vingi bomba unakubali na wakikaa kimya bila kukujibu unajazia mwenyewe wanafikiria nini hata kama hawafikirii kitu na fikira zimekwama!:-(
Narudia ,... ... LABDA ukijihami na mtongozo basi weye unatongozeka!
Na atongozekaye kunauwezekano alikaa mkao wa kutongozwa na atongozaye!
Swali:
AU?
NIMEACHA!
Ngojea Papa Wemba alete za-Ye TE OH
Au to tujikumbushe Geto BOYS waongelee - 6 feet Deep
Uhakika wa ya vitendo vya binadamu LABDA ni kama wa mbegu za kiume mamilioni zipiganiazo yai moja la kike wakati mmoja na kwenye shahawa zenye mbegu mabilioni ,mbegu mshindi kwa kawaida ni moja.
Chakutia moyo ni kwamba,... ..... katika mbegu mamilioni moja ikifanyakazi yake binadamu tutasahau uzembe na bahati mbaya za mamilioni ya mbegu kwa sababu mbegu moja imehakikishia uhakika!
Chakutisha ni kwamba,... ..... mamilioni husahaulika kwa sababu tu ya vurugu ya moja na kama hilo moja lina pua kubwa kuliko sura ndio imetoka hiyo kwa UHAKIKA.
CHA KUTISHA ni kwamba,... .... hata sasa hivi unavyonisoma , kunashughuli mamilioni lakini kuwa kwenye internet ndio iliowini na shughuli ya kwenda kumvizia SISTA wa KIKATOLIKI umgeuze awe mke wako kwa sasa hivi labda ndio imetoka hiyo kama hayuko mtandaoni , e-mail hana na gia za kumuingilia bado hazijaandikwa mtandaoni.:-(
DUH hivi nilikuwa natakakuongelea nini vile?
Ok turudi kwenye swala la UHAKIKA KESHO!
Na KUHUSU KESHO,.. ...sina UHAKIKA!:-(
Uhakika wakumalizia leo yenyewe SINA UHAKIKA, ingawa ni mwepesi kudhania mipango ya kesho nimeimaliza.
Na KUHUSU MIPANGO YAKESHO,... ...sina UHAKIKA,... .....Ingawa nasifiwa kwa hata mipango ya kesho kutwa kwa jinsi nilivyoipangia ratiba na kuisimulia kwa UHAKIKA!:-(
CHA ajabu NAANZA kuwa na wasiwasi na hili neno UHAKIKA kuwa labda lina kasoro kama likitumiwa na BIN-ADAMU kudai anauhakika!:-(
Swali:
Inawezekanaje Mtu akawa ni binadamu halafu anauhakika?
Sikubishii!
Labda,... ... unauhakika na hata wakwenda Mbinguni ingawa hupajui mbinguni ingawa hata kwa kulia utashuhudia kwetu siye walokole kuwa UNAUHAKIKA!
Na labda ni kweli ,.... .... ninauhakika sitakupa MIMBA, kwanza sikujui halafu labda weye TASA kama tu WEYE ulivyokuwa na uhakika kuwa sasa hivi hujabanwa mkojo!
Halafu HAPA labda wote tutabishania ni nini unauhakika na kipi unadhani kila mtu inahitajika awe anauhakika na lazima kuna uhakika , lakini MUHIMU KULIKO VYOTE;....
Unauhakika wewe ni kweli ni wewe na sio akili zako zinakuchezea akili na ukweli labda wewe ni yule?
Narudia;..
Unauhakika wewe ni wewe ?
Unauhakika wewe ni nini?
NIMEACHA wazo Kingunge na kumbuka ni moja ya wazo tu USIZINGUKE! Nakutakia siku KIBONGE Mkurugenzi ndani ya lako LIBENEKE!
Ngojea Sade abadili hali ya hewa...-King of Sorrow..
NDIO,... .....alikufanyia, na unafikiri roho haitatulia usipo mparura na utafaidi ukimfanyizia! Swali:
Hivi tukibadili jina la KISASI na kuliita URODA ukimfanyia kama alivyokufanyia hivi nyie hamtazalisha MTOTO MAUMIVU ambaye atakuwa nimaumivu yenu wote wawili ?
NI kweli,.. ....KISASI kwake ni KISASI kwako!
Na hata ukibisha ,... ... inasemekana kisasi kizuri ni KUSAMEHE! Swali:
Unafikiri unaweza kujilazimisha kusamehe?
Unafikiri utamu wa kisasi ni nini?
Na,.. ...kusamehe ni sanaa,kusamehe ni taaluma na kila mtu ni bingwa katika hii fani ingekuwa hatuchagui ni nini cha kusamehe!
NDIO,.... .....NAAMINI Bin-adamu huchagua vya kusamehe na mara nyingi hudai hawajasamehe leo baadhi ya vitu ambavyo walivisamehe tokea mwaka juzi ila hawajastukia tu kuwa walisamehe kwa kujiamisisha kuwa mpaka leo vina leta MAANA.
UKINIULIZA mimi ntakuambia KISASI NI UGONJWA WA AKILI na kama unabisha, hebu tazama kuanzia mkao wa alipizaye KIASASI hata kabla ya kushuhudia VITENDO vya alipizaye KISASI!:-(
Ni wazo TU Kingunge na kuna uwezekano nakudanganya! KASIRIKA basi na tunza kisasi kama unadhani inalipa!:-(
Sikutanii,... ... hata kama ukipata umaarufu kwa kukaa uchi, GHAFLA mpaka hata maswala ya kilimo kuna watu wataanza kukuuliza wewe ushauri na sio BIBI KILIMO!:-(
Utashangaa nakwambia kuwa mpaka hata apataye UMAARUFU kwa kucheza FUTIBOLI a.k.a KABUMBU , kwa washabiki wake , yeye kafuzu na anafaa UBUNGE hata wa BIHARAMULO na kwao mpaka maswala ya KEMISTRI yeye Profesa.
(Ok, labda katika Uprofesa wa Kemistri hapo nimezidisha.)
Na ajulikanaye GHAFLA kwa sababu WAZAZI wake walikuwa wanajulikana KABLA, ndio kabisa kwa umaarufu wa ghafla leo , AKITAKA URAIS kuna watakaodai ANAKWALIFAI.
Swali:
Kwani wewe pia sio msikilizaji wa watu maarufu kuliko wale wajuao siri ya kitu umuulizacho maarufu?
Haki ya nani tena,... ... baadhi ya binadamu kwa kuzimia watu maarufu hawakawii kutosita hata kuwagawia sehemu zao za faragha a.k.a PIPI na wakataka mpaka kukushawishi na wewe uamini kuwa Lijamaa Maarufu wanauhakika likijamba hakitoi harufu! ( samahani kwa matumizi ya lugha ya faragha)
SIKATAI lakini,... .... maarufu mjinga LABDA hujulikana na kumuuliza maswali kabla ya kumzoea ni bomba KWA SABABU ni BOMBA la staili nzuri ya KUJIGONGA kwake!
Tatizo ni pale kujigonga kukizidi na pamoja na kumgawia sehemu zako za faragha unaanza kuamini kuwa anafaa kukuongoza kama KAtibu KATA. Halafu eti mara ghafla eti nalo LIMAARUFU linaanza kupandisha nyege MPAKA za Ubunge na hata Urais!:-(
Swali:
Au?
NIMEACHA wazo! Nakutakia siku KIBONGE Kingunge na TUTAFIKA TU!
Hata kama ingekuwa ni YESU ndani ya stori, umuhimu wa stori bado ni imgusavyo mtu tu hiyo stori!
Na hata kama stori yako ni tamu namna gani lakini HAITEKENYI HALELUYA a.k.a kipengele muhimu, hiyo stori kwetu si muhimu ingawa ipo HATUKUBISHII!
Na kama ukikutana na bingwa wakutoa stori,... ... stori hata ya MENDE MJAMZITO ndio stori utakayodhani ni baba la stori.
Na aihitajiki stori iwe inahusu Mungu ili utishike,.... .. ukikaa mkao wa kutishwa stori ya viroboto inatosha kukufanya ughairi kufanya uasherati a.k.a ngono a.k.a uroda a.k.a KULA N'GE angalau kwa leo kama tu ya MUNGU, kama akushushiaye stori ya viroboto anaweza kuioanisha vizuri na wako mshawasha.
Ni kweli ,... ... ukikaa mkao wakutishwa SISIMIZI ni SIMBA!
Swali:
Ushawahi kustukia STORI ZOTE HUFUNDISHA na inategemea tu UNATAKA KUJIFUNZA NINI?
Hebu turudishe manyanga kwa POPO BAWA kiduchu;....
.... kwani hukustukia kilichokuwa kinatisha watu katika stori za popobawa ilikuwa sio POPOBAWA bali hofu ya kulawitiwa?
Mie mvivu kwa hiyo jazia mwenyewe kuhusu KIDUDU MTU , Chinjachinja, Ndondocha au tu demu umpendaye kwanini kuna stori anakutisha!:-(
Kumbuka tu,... ... ukitaka kujifunza, hata sentensi moja na wala sio stori nzima huhitajika ili ujifunze.
Na mara nyingi stori au hata kijitabu kimoja kinawadakisha watu UJUMBE TOFAUTI na pia huwafundisha watu mambo tofauti. Swali:
Kwani hujawahi kukutana na mjanja atumiaye BIBLE au KORANI kutongozea ?
Kwani hujifunzi kwa kustukia stori ulioifuatilia kama hii ya POPOBAWA labda haina funzo ukitaka na wala haimhusu POPOBAWA?
NIMEACHA! Kumbuka ni moja ya wazo tu KINGUNGE!
Au ngojea Clouds Production( Sindila , Njaidi, Kolumba , Pamela, Dj Bonnie Luv na Steve kwenye Keyboard.) enzi hizo Bongo Fleva inapewa mimba 1992 wazungumzie - MSELA
Kama unaamini,... .... kwako hilo uaminio ni UKWELI.
Halafu ETI labda unashangaa kwa nini binadamu wanauana,... ... wakati kila kona a.k.a chobisi uipigiayo chabo, KILA MTU ana KWELI YAKE .
Na ukikutana na aaminiye kweli yake ukakosea staili ya kumstua ajuacho si kweli,... ... anaweza kukurukia kichwa, kabla haja kukaba roba, huku akikupiga ngwala halafu ni mpaka baadaye akienda kuoga ndio atastukia naye kachubuka halafu chakusikitisha pamoja na yote hatastukia ''UKWELI YAKE bado ni UONGO!'':-(
Swali:
Unauhakika KWELI yako sio UONGO?
Inasemekana na huu asemao JF Kennedy na.... ni Ukweli...
Na inasemekana asemacho I Jahman Levi nacho kwa watu fulani ni kweli katika- I want to be Free...
Au tu mwanadada kwa jina Truth HurtsftRakim aondelee kunasa labda nao ni kweli katika -Addictive
Kama unafuga mbwa BONGO, ni kawaida KUMSINGIZIA kuwa ni MKALI.
Hukawii kukuta mpaka NYUMBANI kwa kijeba mpaka na kibao wamekuandikia;''JIHADHARI MBWA MKALI!'' kama vile ni kweli mwizi atumiaye akili ni tatizo mbwa mkali.
Lakini kama tu WAZAZI wa Libinadamu wadhaniavyo kuwa watoto wao ni spesho kuliko mtoto wa jirani, labda mbwa wa kwenye tangazo mbwa mkali ni mbwa koko na akibweka ni katika kujihami kwake tu na mapopo.
Swali:
Hivi bado hujawahi kufikiria kuwa labda kama Tanzania inalindwa na mbwa basi huyo mbwa ni KOKO?
Kumbuka lakini kwa wajanja nchi za magharibi jibwa koko kuwanalo ndio ujanja!
Na haki yanani tena utakuta Profesa wa lilesomo unaloamini linahitaji akili za hali ya juu ndio yuko bize anaongea na jibwa lake na anaamini linamuelewa kuliko binadamu na urafiki na bin-adamu haupi tena kipaumbele ukizingatiwa dogi linahitaji KWALITI TAIMU na usisahau linahitaji kwenda kutembezwa ili liende haja kubwa na lazima likijisaidia uzoe kinyesi.
Kumbuka tu tamaduni na mazoea ndio vyaweza vikawa vinasababisha hustukii mbwa koko ni koko .:-(
Na kama wewe ni miongoni mwa waogopa mbwa, LABDA mbwa koko ni MKALI!
Kama kuna kitu unakijua, basi hicho kilishaacha kukuumiza kichwa!
Na labda,... ... kama kuna unachokifikiria, KUNA UWEZEKANO hukijui bado hicho!
Na kama unafikiri unakijua kitu,... ... lakini bado kinakufikirisha, LABDA labda kunamapungufu ya ukijuavyo au kinakasoro hicho .
Na kasoro ya udhaniacho unakijua inaweza kuwa ni mtazamo wako wa kudhani unakijua:-(
Na unachokijua unaweza kusahau kipo,... ... kwa kuwa hukifikirii tena hicho.
Na hata kama ukifikiriacho ni MUNGU,... ... kuna uwezekano unafikiria ya MUNGU kwa kuwa kuna kitu kuhusu MUNGU hujui bado hicho.
Na ungemjua MUNGU,labda SHETANI na vya shetani yasingevutia na kukudaka hivyo!:-(
Swali:
Unafikiri kuna mtu hapa duniani unauhakika anakujua?
Unauhakika hakuna limtu nyumba ya jirani zuuriii NA kwa kuwa unalijua unasahau kulistukia kuwa ni zuri na linafaa kwa matumizi yako ya kuumiza mtu roho?
Unaweza kunibishia,..... .... LAKINI ni kweli mambo yako unayoyajua kama vile kutawaza, huwa unafanya bila kuyafikiria .
Na unachokifikiria, bado hujakimasta ndio maana kunasiku unajistukia mnyonge na katika kujaribu kusawazisha unyonge kuna WATUTISHAO na watakavyotudhaniye wanajua na katika prosesi wanatuboa.
Swali:
Au?
Unauhakika kwanini unafikiri unajua wakati wadaio kujua hata kufinyanga tonge la ugali kunasiku hudondosha tonge?
NIMEACHA! Kumbuka ni moja tu ya mtazamo na wazo Kingunge , usitishike! Ngojea Marvin Gaye abadili hali ya hewa kwa kibao - Lets get it on
Au tu aendeleze simulizi za uasherati katika- Sexual Healing
Mara nyingi ni ghali kutunza siri yako hasa kwa kuwa asilimia kubwa za siri za watu zitunzwazo zilishaexipaya longitaimu!:-(
Na kwa kuwa wote tunajua jinsi gani watu ni wasahaulifu, labda siri yako isingekuwa wewe binafsi unaiendekeza iendelee kuwa siri , siye wengine tungelishasahau uhusiano wako na hiyo yako siri.
Siri kiboko!
Inaweza ikasababisha unogewe na hata visivyovitamu kwa kuwa tu unavilia migombani kisiri na kama ungetandikiwa mkeka ungelistukia zamani unogewavyonavyo vimechacha kwa mbaali na vinanuka kwa kuwa si siri kuwa ni kweli vinakosewa kuoshwa.
Na,... .... umuhimu wa siri mara nyingi unazidishiwa sifa zaidi kuliko unavyostahili. Matokeo yako unaweza kunogewa na kutunza siri huku kumbe kama tungeijua hiyo siri wala tusingeioanisha na huo udhaniao ni umuhimu.
Swali:
Unauhakika siri zako bado hazijaexipaya na unaendelea kuzitunza kwa mazoea tu?
Hivi weye sio miongoni mwa wadaio kwa kuwa siri yako anajua mtu mmoja tu a.k.a rafiki mpendwa, basi hiyo unadhani bado ni siri?
Kumbuka, kutunza siri ghali kinoma!
Inashangaza lakini kwa jinsi watu wasivyostukia ughali wa kutunza siri ingawa hao hao ni mabingwa wa kunyemelea vitu vya chee!:-(
Kumbuka kama siri yako ni kuwa unamakengeza, kama nakupenda basi wewe kwangu KAMWE HAUNA MAKENGEZA na ukiniuliza ntakuhakikishia kuwa hayo ni macho malegevu na kwa kurembua katika mahaba hauwezekani.
Swali:
AU?
BADO unauhakika na umuhimu wa siri yako?
NIMEACHA na kumbuka ni moja ya wazo tu Kingunge! Nakutakia siku KIBONGE na kila la kheri kwa kupafekti sanaa ya kuficha siri!
BAADAYE basi KINGUNGE!
Ngojea tu Lupe FIASCO amkaribishe mtu katika - Welcome Back Chilly
Pamoja na BAA kulalamikiwa,.... ..... ukitaka naweza kukuhakikishia kuna masomo ambayo baa ni Chuo Kikuu.
Na mara nyingi ni watu wasioijua baa huwa mstari wa mbele kuilalamikia baa!:-(
Siwalaumu lakini kama kwa kuwa kwako baa pamoja na mengine kama ya kujisomea hufanyi na tunaweza kujumlisha pia na tabia yako ya kuwa huwa Unalia NA Kujikojolea ukilewa, wakati mtoto wako anavaa midabwada na hajawahi kushiba.:-(
Lakini waweza kujifunza WATU na SILIKA ZA MTU baa zaidi ya uwezavyo kujifunza mtu Kanisani , Msikitini au Shuleni.
Ila BAA kama tu Msikitini au Kanisani,.... ..... ukienda na ajenda zako zisizohusiana na kikao, ujumbe wa SHEKHE au PADRE unaweza usipande!:-(
Swali:
Au?
Ila baa kiboko , ... .....usipoangalia unaweza ukanywa mpaka kodi ya nyumba na kuanza kuifikiria kuinywa pesa ya kununulia padi za mke kama tu ulivyowahi kunywa za mpenzi hausigeli.:-(
Swali:
Lakini si unakumbuka kila swala binadamu kaamua kuwa lina mahali pake?
Na kwani darasani huwa unaelewa kemistri wakati unamfikiria Khadija?
Nimeacha!
Au ngojea Bunny Wailer aongelee- Mellow Mood
Au tu Peter Tesha aongelee- Why Must I Cry
Au tu Bob Maliya aje katika- All in one medley mix
Nakuacha na baadhi ya picha zangu za juzi ya jana..
Papara za nini, .... .....sikilizia hiki kama unafanya hiki, KILE kina baadaye.
Swali:
AU?
Na kama wakati huu hiki ni penzi,... ...unaweza kuharibu utamu wa penzi kama wakati unafanya penzi , hapohapo unafikiria baiskeli yako iliyopata pancha.
Na ni kweli.... ..... mambo mengi yanagombea USIKILIVU wako.
Sikilizia basi!
Swali:
AU?
Ni kweli ingawa unaweza kula makande kwa parachichi,.... ...... lakini kama unataka kuwa na uhakika na ujazo wa utamu wa parachichi, kula parachichi wakati unalifikiria parachichi na sio mchikichi.
Na kama umeshikwa makende,.... ...... stukia uumeshikwa makende na huo si wakati wakufikiria kaswende.
Swali:
Au?
NI wazo tu KINGUNGE!
Swali:
Au?
Si unakumbuka daima huwa unafanya kitu zaidi ya kimoja na hata wakati wa haja kubwa unaweza ukafanikisha haja kubwa wakati unafikiria kodi?
Ngojea St Germain watupe - So Flute
Au tu Msondo Ngoma wadai ingawa kuna vitu vingi muungwana anaweza kuvikaza,- Kaza Moyo
Mpaka unaweza kusahau ni UTU sifa unaostahili,... ... na unajua ni kwa nini!
Kama USHAPENDEZA,... ..... halafu iwe nini... ......wakati wajua mwisho wa siku utaishia kwa kutopendeza,... ... sasa waringia nini?
Kwani tukisema UMEPENDEZA,... ... unafikiri tunamaanisha nini... ....wakati wajua kupendeza kujichoni mwa akupendaye,.... ..... na kwa siye wengine weye maning'ining'i, au unabisha nini?
Kwani matumizi ya aliyependeza na asiyependeza,.. ... tofauti yake nini... ...wakati wote wafaa katika utengenezaji wa mimba,... ..... asifiwayenawe anacha zaidi nini?
Ukifikiria sana , dhana ya KUPENDEZA ni mtindio wa akili,.. ... hapo ndio utajiuliza; hivi binadamu wenye akili huwa wanafikiria nini?
Kama bin-adamu ajua maisha na uhai huishi ndani ya ulio uchi mwili,..... .... dhana ya kupendeza kwa kujisitiri ,yasababisha mtu amtoe uhai mtu kwa nini?
Mahitaji ya mtu kwa mtu hayako kwa alivyopendeza mtu,.. .... au wafikiri uchi na ukiwa uchi haupendezi nini?
Na kupendeza kwa Kigogo ni tofauti na kwa Kibena,.. .... Je wafikiri Mmasai asilia ukipendeza na bichikoma anaona nini?
Swali:
Unakumbuka ni udhaifu kujisikia vizuri kwa kupendeza?
Unakumbuka ni kukiri mapungufu wakati unajisikia umependeza?
Ukipendeza unafikiri umependeza ili ufae kwa matumizi gani?
Kwani usipopendeza unauhakika hailipi?
Ni wazo tu Kingunge na NIMEACHA!
Hebu basi twende tena KameruniRichard Bona atusaidie wimbo uitwao- - Ekwa Mwato
Au tubaki tu KameruniManu Dibango alete tena kibao - Africa....
Ukipatia KUJIPENDEKEZA kwa asiyekupenda,... ...... ni maudhi.
Kwa kuwa kujipendekeza ni maudhi,.. ... labda unaudhi!
Lakini MAUDHI ni mpaka ujishughulishe na maudhi,... ....ili yakuudhi.
Na kama unajipendekeza kwa akupendaye,... .... kuna mbwembwe uzidishazo ingawa sasa hivi anapenda ingawa ni maudhi.
Cha ajabu hakuna binadamu aliyefanikiwa ,... .... bila mtu fulani kumuudhi!
Na Binadamu asiyefanikiwa,... .... kunamtu anamuudhi.
Kwa hiyo ,.... ..... labda binadamu wote kujumlisha wewe na mimi wanaudhi!:-(
Na wazo hili la kuwa kuna wajipendekezao hata pasipohitaji kujipendekeza,... .... labda LINAUDHI,... ... hasa kama linakuudhi na wala hayakuhusu MAUDHI!:-(
Swali:
Unauhakika kuwa hujihusishi na maudhi ndiomaana YANAKUUDHI?
Unauhakika unamjua mtu yeyote ambaye ukimpachansi hatakuudhi?
Unauhakika huwa unajistukia kila ukijipendekeza?
Nakutakia Wikiendi Mchelemchele!
Ngojea Mlimani Park Ochestra kwa hisani ya Tizedboy waongelee- Maudhi
Au tu Pablo Francisco aongelee wanamuziki wa RnB...
Au tu Rupee arudishe soca katika- Tempted to Touch
Ukiwa TAJIRI amani inapotea,... .... kwa kuwa unadhani tutakuibia ndio kisa cha geti kali huku unawasiwasi tutakuomba.
Ukiwa MASIKINI amani haipo,... ... kwa kuwa unadhani huna na unahitaji kuwanacho kwa kuwa unadhani wengine wanacho na wanakuhisi utaomba.
Ukiwa na DINI amani haipo,... ... kila siku unakimbizana na maandiko na pia hofu za jehanamu au kugeuka bata , labda ndio maana unadini.
Ukiwa huna DINI amani haipo,... ... kila kukicha kunaatakaye taka kukutisha au umhisiye anataka kukutishia jehanamu wakati hapahapa duniani chamoto unakiona.
Ukiwa na NDUGU amani hakuna,... ... kwa kuwa inamaana lazima kama una ndugu utafiwa na ndugu na kifo kinamchezo wakutozoeleka.
Ukiwa huna ndugu amani hakuna,.. kwa kuwa unadhani wenye ndugu kuna wakunyimacho.
Ukiwa na MARAFIKI amani hakuna,... ..... ndio wasababishao umeingia mpaka mikopo uchangie, kitcheni pati, begi pati na kwenye pati unaanza kuingia wasiwasi kama ni kweli udhaniaye rafiki kweli ni rafiki.
Ukiwa Mtanzania amani hakuna,... ... ikiwa mpaka leo huna uhakika na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kama bado unajisikia Mbara zaidi au Mzanzibar zaidi na ni Mtanzania kwakuwa katika kikao hiki si bomba kujitambulisha kuwa unajisikia Mchaga.
NIMEACHA! Na kumbuka ni wazo tu KINGUNGE, usitishike!
Ngojea tubadilishe hali ya hewa kwa kuangalia jinsi Kigoma wafanyavyo katika - How to Flirt
H-Town wazungumzie- Knockin the boots
Au tu Scarface asifie tabia mbaya enzi hizo katika- Recognize
Mke wa kwanza amemzoea,... .. na ubunifu kaacha , kashazoea.
Na hata kwa harufu chooni ajua ni yeye,... ... na mpaka kwa harufu ajua alichokula, kamzoea.
Na hata akimdanganya hanuki kikwapa ajua amdanganya,.. ... ingawa haachi kuulizia ya kikwapa au ya atingishavyo singida dodoma, kazoea.
Sijui ni kwa mazoea,.... .... ghafla mwanawani wa nyumba ya jirani ukifumba macho anasogea.
Sijui mazoea yaua shahuku,.... ..... uhakika wa kitu wamfanya asiharakishe kutoka sokoni awahi ile ile faragha aliyoizoea, kaizoea.
Na kama nguo na kitafunio cha chai hubadilishwa,... ... sijui mke wa kwanza asipobadilishwa nayo tuite ni mazoea?
Na labda mme wa kwanza anafaa zaidi kwa porojo,.... ..... na wa sita ananoga kama gari jipya kwa tendo na kitengo , hujamzoea.
Na kama unahamu na nyama ya kuku,.. ..... kunauwezekano nyama ya bata si tamu , hujaizoea.
Tatizo la mazoea,... .....ukianza kubadilisha itafikia unatakakubadili visivyobadilishwa na unafanya kwa mazoea.
Na mazoea ni mabaya,... ..... na hata kuumizwa roho waweza zoea.
Na labda hamu ya mme wa pili,.... ..... hainatofauti na ya mke wa sita kama ukizoea.
Na kabla hujabadili chuo,... .... jiulize kama kuna umuhimu au ni yako tu mazoea.
Na katika kujizoelesha mazoea,... ..... waweza kujikuta umejilimbikizia wakati yote ya muhimu katika utamu yalikuwapo kwenye ya mke wa kwanza uliyoizoea.
NIMEACHA! Kumbuka ni moja tu ya wazo! Ngojea twende Zimbabwe kwa Oliver MUTUKUDZI adai -NDAKUVARA.....
Au tu tupitie tena Zambia kukutana na K'Millian adai-NIZAKUKONDA
Kizuri na cha maana mara kenda kadhaa huwa HAKIONEKANI na wala HAKISIFIWI!
Na,... .... UTAGUNDULIKA kirahisi uko HAI kwa kukosea na sio kupatia!:-(
Na kwa unafiki wa BIN-ADAMU,... ... kuna watakao kushangaa kwanini UNATUKANA wakati kwa kuongea kilokole na ukiongelea korosho na magimbi waliovaa raizoni hawakustukii UPO na wanakunyima mpaka sehemu za faragha na angalau wanageuka ukiwatukana na ukiachia msonyo!:-( Swali:
Unauhakika kweli na sababu zako za kutukana uzifichazo nyuma ya vihasira vyako vilivyokonda?
Unauhakika huwaruki wafanyao mazuri na kustukia wakoseao na wewe ni mmoja wa waliosababisha TAARIFA ZA HABARI zimejaa mambo mabaya ambayo huitwa NEWS?
Na kuna uwezekana hata hapa unaendelea kusoma ili uone kama ntatukana , na kama ungekuwa na uhakika niandikacho ni mahubiri ungesha hama kwa kisingizio fulani bashasha kama vile '' NAKUBOA''.
LIONE VILE!
Na NAACHA TOPIKI umeniudhi!:-(
Ngojea basi tena DANY ENGOBO azungumzie-FRANCHA...
Au tu tutulize hali ya hewa kwa kuwaachia MAKOMA wamrudishe mtu kanisani kwa kibao- Ola OLE
Kuna jinsi unavyojigundulisha kwa,.... ..... KWA jinsi unavyojitahidi usigundulike!:-(
Na ni kweli,.. ....Hamu ya bagia haifichiki ingawa unaweza kudhani unaificha hasa kama WEYE mtaalamu wa tabia nzuri, hujulikana kwa ujitahidivyo kuficha utamanivyo bagia wakati una ya bagia , NYEGE MSHINDO!:-(
Na maisha nishai kwakua yanaweza yakasababisha usifiwe kwa kuficha na sio kwa kutumbua kitumbua.
Na katika swala hili LABDA kusawazisha matibabu , TIBABU labda ni kutumbua na si kuficha hamu a.ka. NYEGE MSHINDO. Swali:
Unauhakika namaanisha nini kwa kuropoka kauli bashasha a.k.a NYEGE MSHINDO?
Hivi unauhakika nyege mshindo ni nini?
Na usipojua ni nini, unauhakika hapa kwa tafsiri yako mheshimiwa kingunge situkani?
NA NI KWELI kuwa katika MATATIZO ya kuficha,.... ..... nasikia hii TABIA HII ilisababisha mpaka kuna MWANIWANI hakuzaa.:-(
Na kwa kuficha pia nasikia kuna mtu a.k.a MWANIWANI FULANI, kafanikiwa na katunza mpaka cha kesho kwa kudhania kinamatumizi kesho.
Na ni kweli pia,... .....udhaniacho ni cha kesho kinalika leo ukiwa na hamu na unahitaji kutibu nyege baruti a.k.a NYEGE MSHINDO.. DUH!
Swali:
Sasa unafikiri tutunze au tutumie wakati unajua nyege mshindo ni kishawishi?
Hivi unauhakika ni ujinga nikisema inawezekana kujisikiasikia unadhambidhambi ni nyege za kujisikiasikia una nyege a.k.a hamu za kimbingunimbinguni na yote ni kwa sababu kunaaliyekuambia kuna mbinguni ili uwe na cha kukusababisha uteseke kwa staili kwa kudhani kuna uliowazidi dhambidhambi?
NIMEACHA na kumbuka ni moja tu ya wazo MAWAZONI mheshimiwa KINGUNGE!
Binadamu kila akijazia HUKU, kule inapungua. Na KILA akijazia KULE, huku inapungua.:-(
NA hakuna furaha kwenye UPUNGUFU:-( Na hakuna AMANI kuliko na UPUNGUFU.:-(
BIN-adamu akijazia kwa KUZAA WATOTO,... ... ya binafsi isiyohitaji watoto HUPUNGUA.
AKIJAZIA kwa kujali ya BINAFSI,... ... ya WENGINE na ihitajiyo wengine au ya watoto huwa ndio upungufu na KILICHOPUNGUA.
Na hakuna amani,... ...PENYE kilichopungua.
Na hakuna FURAHA,.. .. penye ambacho kimepungua.
Na MTU akioa anajazia hata kwenye YASIOPUNGUA. Na Bin-ADAMU AKIOLEWA ,labda ANAJINYIMA kujazia ya yule JIRANI kama ndiye ALIYE kwenye ujazo wa kuonjesha nanihii KAPUNGUA.
Na kabla ya KUFA,.. ... hata IMANI HAITOSHI kama kujazia nyege haihitaji imani na nyege ndio KISTUA KACHOLI kilichopungua.
NA kama huu ndio wakati wa kustukia HIKI,.. .....na kama hiki kimejaa na kama hujisikii vizuri, basi kile KIMEPUNGUA.
Swali:
AU?
Unauhakika kama ungejazia kile ungehisi kwa hiki mimi mshamba?
NIMEACHA!
Ngojea tupate kutoka kwa huyu MGANDALOU BEGA alete -MAMBO No-5
au ngojea tu LOS DEL RIO watusumbue tena na kibao - MACARENA..
Tupendao HIPHOP tusingemshangaa P.DIDDY kwa kumzalisha mtu akiwa katikati ya kampeni ya MTV ya kuhamasisha matumizi ya KONDOMU.
Tusingemshangaa mgombea URAIS wa Marekani JOHN EDWARDS kumpa mimba msaidizi wa kampeni yake ya Urais ili amshinde Obama wakati anasafiri na mke.
Tusinge mshangaa PAPA WA KIROMA a.k.a Papa BENEDICT akichukuliwa kama mshauri mkuu wa maswala ya KONDOMU wakati yeye bikira na ujuzi wake wakuvaa kondomu ni ziro au ni ule wa kuvalisha kidole gumba cha mkono kondomu katika kuwaza inakuaje jidume linaweza kuvalisha kajidume kake mpira yote ikiwa ni katika kuwania kikojoleo.
Tusingemshangaa Rais ZUMA kwa kuwa na watoto wa mke na mke mtarajiwa wapishanao mwezi na kudhani akioga anaepusha UKIMWI.
Tusingeshangaa ni kwa nini kampeni za matumizi ya kondomu Afrika zinachukua muda mrefu namna hii na mpaka sasa tunafundishana jinsi ya kuvaa soksi, wakati barani chakula hakitoshi.
Swali:
Unauhakika ni kweli Mungu aliumba wanadamu ili wagundue Kondomu na madawa na sio aliwaumba ili wazaliane na kufa upesiupesi dunia isijae kirahisi kiisidingo?
Unauhakika na asilimia za utamu ambazo kondomu inashea nawe au huvai kwa kuionea wivu tu?
NIMEACHA!
Nakutakia siku KIBONGE Mkuu!
Ngojea nimuachie tena MATONYA aongelee -Taxi BUBU...
Au tu James Dandua.k.a Mtoto wa DANDU adai-- Sina Makosa..
Ndani ya mtu,... ..... kichaa ni KICHWA Akitulia mtu , .... ......kilichotulia ni KICHWA.
Kichaa akitulia bado ni kichaa,..... ....na akifanya fujo kichaa atahakikishia tu umati kuwa yeye kichaa.
Cha ajabu aaminikaye si kichaa akifanya ukichaa kwa kufanya fujo ,... ... atajulikana kwa fujo na hataitwa kichaa.
Na asiyeaminika ni kichaa hata katika kuonyesha penzi akilamba vikojoleo ,... ... bado itaonekana anatoatu staili ya penzi na huo si ukichaa.
Lakini ukimwangalia vizuri kichaa,... ... waweza kusahau kujiuliza kwanini unadhani yeye ni kichaa,... ...hasa katika dunia hii kichaa ambayo mpaka wasio vichaa ilikuonyesha jamii kuwa si vichaa wanafanya ukichaa.
Na kichwa na jinsi ya kubalansi yaliyo mukichwa,... .... bado kisipotulia kichwa cha ajabu unaweza usiitwe na walimwengu kichaa.
Ingawa maadili na vitendo,.. ...mwanawani ukimuangali tayari ni kichaa.
Katika dunia hii kichaa,.. ...unauhakika nani katuliza kichwa wakati kazungukwa na ukichaa?
Na katika dunia kichaa mtu akitulia,.. ... unadhani utulivu huo wa mtulivu atuliaye kwenye ukichaa si ukichaa?
Hebu angalia wasifiwao kwa akili,... .... na ugunduzi wao wa vitu viharibuvyo dunia na kugeuza watu vichaa!
Hebu nenda kuwachungulia waomba Mungu,... ... utajiuliza hivi Mungu hajiulizi kwa nini kaumba vichaa?
Hebu watazame waumini walio wengi,... ...washafikia mpaka kumtetea Mungu muweza yote asiyehitaji utetezi, ... na kuchukia na kumua binadamu mwenzao mnyonge kama vile vichaa.
Hebu leo muangalie tena vizuri umuitaye mheshimiwa,... ..... unadhani huyo hata kwa kukubali uheshimiwa yeye si kichaa?
Hebu muangalie na ajifikiriaye mzuri na kwa juhudi ajaribu tingisha tako,.. ....au hata ajifikiriaye ni mbaya sura kama tako, wadhani hao kwa wazo hilo si vichaa?
Na yule udhaniaye ana akili,.... ......umesahau yasemekana wenye akili sana ndio huonekana vichaa?
USAHIHI wa kitu maarufu ni ule waaminio wengi wadhaniao ni SAHIHI!
Ukiwa pekee sahihi hukawii kuchekwa hasa kama wewe si maarufu katika jamii hii iwasikilizao waliozoeleka kusikilizwa mpaka imefikia matumizi ya kondomu anaulizwa Papa Benedikti wakati inasemeka hajawahi kufanya ngono a.k.a kutumia koni / kitumbua.
Lakini,... .... USAHIHI wa kitu ni sahihi hata kama wahusika hawaamini ni sahihi na wanajishughulisha KUSAHIHISHA. Na kuishi siku kwa siku katika KUSAHIHISHA labda hilo ndilo liitwalo MAISHA YA BINADAMU.
Na mara nyingi ni kweli,.. ....Kwa BIN-ADAMU usahihi wa kitu ni ule UDHANIWAO TU KUWA NI SAHIHI pale WAHUSIKA wadhaniapo wanajua nini ni SAHIHI.
Binadamu ni mabingwa wakudhania wanajua nini sahihi kwa mfano:
Dunia ilikuwa na umbo la meza na mtazamo huo ulikuwa sahihi na wabishi mpaka wakauawa mpaka na KANISA, mpaka baadaye kidogo ilipohakikishwa kuwa dunia ina umbo la kinyeo a.k.a mduara( samahani kwa matumizi ya lugha ya faragha).
Na labda Bin- adamu huamini kalaaniwa kwa kuumwa hata kipindupindu, mpaka akistuliwa kuwa staili ya kunya au usafi tu huwa unachangia gonjwa na dawa ya kipindupindu ipo. Na labda ni kweli UKIMWI itaaminika ni laana mpaka utakapo pata dawa na kugeuka kuwa kama gono baada ya dawa kugundulika na uasherati KUFANIKIWA kuibua kaka yaye UKIMWI ambalo litakuwa ni gonjwa ambalo ukimchekea tu mwenye kaka yake UKIMWI basi makende na nyeti yatakuwa ya shadaka KAKA YAKE MDUDU na sio kama sasa hivi ambapo ni mpaka uhangaikenaye.
WANYAMWEZI, WAPARE; WACHAGA, WANDENGEREKO,..... nk yalikuwa ni mataifa na ilikuwa ni mtazamo sahihi, mpaka ilipogunduliwa dhana ya kuyaita kuwa ni makabila, na hilo ndilo mpaka sasa hivi huitwa SAHIHI.
Tanzania haikuwa nchi na ilikuwa ni SAHIHI, mpaka waaminio katika dhana ya UINCHI walipodai ni NCHI ingawa asilimia tisini ya wananchi wake hawajawahi kufika hata mpakani mwaTanzania na Kigoma, na wakifika hawajui kuwa huu ni mpaka na kama unabisha waulize Wamasai.
Na labda ukitaka mifano zaidi jaribu kufuatilia nakadhalika kadhaa saba na nusu zilizo sahihi!
Na,.. ....kuna uwezekano kabisa USAHIHI wa UJUACHO utaujua baada ya kufa au katika zile dakika za mwisho kabisa wakati unaingia UVIVU WA KUPUMUA na MOYO kuanza kukosea KUDUNDA KWA kufuata miondoko ya SEBENE, ndipo kuna lijamaa ulilodhani maishani mwako yote linakupenda, linaweza kuingia ujasiri na KUKUNG'ONG'A kabla halijakutakia kheri ya kufa itakayofuatwa na msonyo mnene na wenye uzito wakutosha huku likichekelea afadhali unakufa.
Kuna uwezekano pia kuwa USAHIHI SI MUHIMU na chamuhimu ni KUISHI ukisahihisha na hayo ndiyo MAISHA.
NAACHA TOPIKI hii lakini ingawa ,... ......LABDA kunamambo udhaniayo ni SAHIHI mpaka unagombana au unanipandishia sketi kunisuta( kitu ambacho napenda hata ukiwa hunisuti mwanawali weye ), we yape tu muda MAMBO HAYO na YAnaweza YAKAKUSHUSHUA na kukusuta.
Na labda ,... .....ni muhimu kwetu WOTE kuyapa muda MAMBO ili YATUSHUSHUE tujue KUNAUWEZEKANO KILA TUJUACHO si SAHIHI.
Na labda,... .... maisha yote haya wakati tunamfikiria Mungu Mbinguni, ukweli ni kwamba tunaishi ndani ya TUMBO la MUNGU kama tu minyoo idhaniavyo tumboni kwako BIN-ADAMU ni ulimwengu na ukienda haja kubwa, minyoo hudhania kuwa imepelekwa jehanamu baada ya kustukia kijoto cha kwenye tanki la mavi(samahani kwa matumizi ya lugha ya faragha), na ukinya kichakani minyoo wanadhani wamepelekwa mbinguni.
Swali:
AU?
Unauhakika na mtazamo wako kama unadhani wangu si sahihi?
DUH! NIMEACHA! Kumbuka ni moja tu ya wazo KINGUNGE! Nakutakia tena SIKU KIBONGE!
Hebu twende kidogo tukamsikilize JAJI Saudi Arabia aamue -tumchape kidogo kofi mwanamke....
Au turudi tu kwenye DANCE tujikumbushe staili - ELECTRIC BOOGALOO
Pendo ni hongo,.. .... ukinipa pendo wanishawishi nikupe pendo mwanawani.
Pendo kama Pesa lanunulika,... ..... na vyote thamani zake ni mpaka kwa watu ziaminike zinathamani na hazinyonyi kama kupe.
Pesa aina ya noti ni makaratasi na si pesa kama anunuaye na anunuliwaye haamini manoti ni pesa.
Na hapa tunaweza tukabishania tu aina aina ya hongo utumiayo katika kutaka upendwe na kuanzia peremende umpayo mtoto wa binamu nyama ya hamu, sadaka kanisani, mpaka kumpa mtu sehemu zako za faragha pale faragha ,vyote ni hongo na labda walengwa tu ndio tofauti.
Na uchoyo ni bonge la hongo kama linamlenga mlengwa atakaye kustukia kwa kuwa ndio weye pekee umnyimaye, hasa ukikumbuka kuna wazidishiwao kupewa mpaka hawakumbuki burungutu tamutamu ni lipi katikati ya maburungutu tamutamu yaliyopoteza ladha kwa wingi wa utamu .
Nachojaribu kukutonya ni,.. ....KWA ujumla kila kitu kinafaa kuhongea na ni staili tu za kuhonga zimleteaye sifa atoaye peremende na lawalawa nyama kwa watoto na zimleteazo achunwaye BUZI sifa mbaya mbele ya wachunwao buzi kwa staili nyingine kama ya kuogeshwa na maji ya karafuu nyumbani, zote katika kuhonga zinalenga KUDAKA atensheni, a.k.a kuhusishwanishwa na UBAB K .
Na hongo lako hata la kujitia mnyonge kwa apendaye WANYONGE ladaka mahaba ili ujistukie babu kubwa na kunasa hata kama kwa mtazamo wako hilo si hongo.
Swali:
Unauhakika hakuna utoacho kwa nia ya kupendwa hata kama ni lifti kwenye baiskeli yako ya foneksi ?
Kwani unafikiri hongo ni nini?
Na hondo ya pendo ya weza kuwa ni kupenda na kama makaratasi kwa imani huaminika yana thamani na ni manoti-pesa, basi tukiamini ,pendo ni pesa.
Na magimbi yaweza kuwa ndio msaada kwa pendo la leo litamanio mihogo kwa chai na kwa bahati mbaya chai ipo pekee bila kitafunio , na hatuna pesa.
NAACHA WAZO! Lakini,... ...LABDA uaminivyo ni kweli na kuna haja za MTU kutaka kukubalika au hata kupendwa .
Na,... ....katika kujaribu kudaka upendo unaweza kujikuta unahonga na hongo yako inaweza ikawa ni kukaa tu vibaya kila jamaa likipita wakati unachagua mchele.(samahani kwa wazo la faragha)
Lakini,.... ... LABDA kwetu wote , kama unachojaribu NI kupendwa na wenzetu ,labda dawa ni kujaribu kupenda tu WENZETU. Swali:
AU?
Unauhakika pendo lako halina masharti kama udaivyo weye mwenye roho nzuri ?
Kumbuka hili NI moja ya wazo tu hapa Kingunge na NIMEACHA!
Tabia nzuri ni ile jamii imeizoea hata ikiwa ni ile ikubalikayo katika jamii , hata kama ni ile ya kulamba makamasi kama jamii inaamini huleta afya.
Swali:
Unauhakika ni kwa nini kwa mtoto kulamba makamasi kwake mtoto sio tabia mbaya?
Unauhakika watoto wasingekatazwa kulamba makamasi utotoni halafu wakakua na taaluma hiyo, unafikiri kusingekuwa na MISS KULAMBA MAKAMASI siku hizi au tu wakumbwa wasinge sifiwa kwa staili zao za kulamba makamasi ukubwani kwa mrija?
Unauhakika na sababu zaidi ya kinyaa kwa nini konokono hummezei mate Dar wakati Ufaransa ni chakula cha wajanja?
Na,... .... kuna uwezekano kabisa WEWE au MTU a.k.a BIN-ADAMU atastukia anatabia nzuri kwa kusifiwa na watu wengine kuwa anatabia nzuri. Kabla ya hapo TABIA ni TABIA tu ndio maana kila mtu akiwa chooni pekee kila tabia ni nzuri kama hujiumizi.
NA ukishasifiwa unatabia nzuri , ndio mwanzo wakujiwekea mipaka ya wapi mwisho wakupekecha ili isitokezee kwenye uwigo wa TABIA MBAYA.
Ukiweka mipaka, ndio imetoka na ndio mwanzo wakuanza KUJAJI WENGINE kuwa wamezidisha hasa kama wanavuka mipaka ambayo umejiaminisha na UMEAMINISHWA kuwa ndio TABIA NZURI.
Na kumbuka ,... .... kunatofauti kati ya TABIA NZURI ikufaayo na TABIA NZURI ambayo jamii inaiita TABIA NZURI ingawa inaaminika iitwayo tabia nzuri na jamii ndio itakuletea maisha marefu. Na,... ....Kuna vigezo visababishavyo uamini kuwa tabia nzuri usifiwayo na kundi ndio bomba kwa kuwa tu binadamu ni vigumu kuishi bila kundi ndio maana anampaka Mwenyekiti wa Kijiji. Swali:
WEWE kama ni MTANZANIA, unakumbuka ni TABIA MBAYA zilizosababisha Mwalimu Nyerereapelekwe shule kwa sababu alikuwa kichwa ngumu ikaamini shuleni ndiko atachapwa viboko?
Unauhakika sio jeuri na kichwa ngumu ya Mwalimu Nyerere ndio maana mpaka leo anaitwa Mwalimu na kama hakukuongoza wewe basi alimvua hata uchifu BAbu yako?
Kumbuka,... ..... tabia nzuri ni NZURI kwa wafaidikayo na hiyo tabia ambao ndio watakusifia UNATABIA NZURI.
Na tabia mbaya hubadilishwa jina kama jamii inaanza kuikubali. Kwa mfano;
Uchoyo uunaweza kuitwa kujitegemea.
Ngono itaitwa tendo la ndoa.
Jeuri anaweza kuitwa anamsimamo mkali.
Kujamba kutaitwa ''Kapumua''
Wezi wanaitwa mafisadi.
Ok ! Labda haikuwamifano mizuri.:-( Swali:
Unauhakika Tabia nzuri sebuleni Dar-es Salaam Tanzania ni Tabia nzuri Dar-es- Salaam katika sopu opera kwenye TV ambayo siku hizi ndio mwalimu wa taifa la kesho la wana Dar-es Salaam kuhusiana na Tabia nzuri hata katika kujibu ni thong gani a.k.a chupi mwanadada avae chini ya gwaguro?
Unauhakika unatabia nzuri au tu kwa sababu katika jamii yako hiyo ni tabia nzuri kwa kuwa katika jamii yenu kunywa Gongo kwa linyama lililonona la Nguruwe ni Ruksa?
Halafu eti bado unashangaa wale wenye TABIA NZURI wafungiao wanawake zao nyumbani kwa matumizi ya starehe za MUME na kwa kuwa ni tabia nzuri!
Halafu unashangaa wengine kwa tabia mbaya wakati nawewe tunakushangaa kwa TABIA MBAYA! LIONE VILE VIVUUU!
NIMEACHA na kumbuka kama unataka kuishi muda mrefu inasemekana Tabia Mbaya inaua haraka shauri yako!:-( Kumbuka nawazatu hapa KINGUNGE!
Ngojea nimuachie George Carlin aongelee- The little things
Au ngojea tena George Carlin aendelee kuongelea-Life after Death
Fanya nayosema sio nayotenda, kuna waungwana ndio washaurivyo.
UTAAMBIWA:
Usizini.
- kama uletewavyo ujumbe kutoka kwa Askofu-mchungaji au na sheikh mzinzi.
Twendeni gezaulole tukajishughulishe na kilimo.
- ujumbe wa bwana kilimo kutoka chuo cha kilimo asiye na shamba na ni chekibobu asiyependa tope wala kwenda shambani.
Miye sipendi wanafiki
-ujumbe kutoka kwa mnafiki.
Acha ujinga
-ujumbe kutoka kwa mjinga.
Usifanye nakadhalika kadhaa
-ujumbe wako na nakadhalika.
Na ni kweli labda binadamu huwa wanakuambia wanachofikiri ila wanaondoa kipande kikubwa cha wanachoamini na kufikiri ambacho ndio unaita UMEWAFUNANIA ukikuta wanakigina sehemusehemu.
UJUMBE wa mahubiri ya usidokoe mboga pia yanaweza KUKUSHANGAZA kwa kukutia nyege za kudokoa mboga kama tu ukimdaka aliyekuhubiri usifanye uasherati ATAKAVYOKUSHANGAZA ukimfumania ANAKULA KITENGO a.k.a tunda.
LAKINI bado wakati unamtumbulia macho anaweza kutumia sentensi maarufu na kukukata kauli kwa kukukumbusha:
''FANYA nayosema na usiige VITENDO VYANGU NAVYO TENDA! Ubarikiwe sana mpendwa tutakutana basi kwenye BIBLE STUDY!:-(''
NA kama WASEMAVYO WATANZANIA wangekuwa wanatenda, TANZANIA INGEKUWA NI NCHI ILIYOENDELEA NA INAFUATA UJAMAA na KUJITEGEMEA MPAKA LEO, halafu wala wasingekuwa wanamuhisi Rais Mkapa naRais MTARAJIWA LOWASSA kuwa labda kuna kitu wamedokoa ambacho mwalimu wao MJAMAA a.k.a NYERERE alikataza .
Kama wasemavyo watu wangekuwa wanatenda kweli , labda sasa hivi ungekuwa na LIMCHUMBA zuriii ambalo uliliona kwenye gazeti na unamapesa BWELELE , mwenyewe umetulia ukifyonza aishikirimu kwa juisi ya UKWAJU.
Swali:
Unauhakika ungefanya yote unayosema ungekuwa hai?
Hivi wewe na mimi sio wanafiki kwa kukana hamu ya kitendo hadharani kama ni kitendo fulani ?
Hivi unasema zaidi au unatenda zaidi?
Hivi kusema sio kitendo?
MIE TOPIKI imenishinda na labda nachosema sifanyi kwa vitendo!:-(
Namuacha tena SHIHAN azungumzie - FLASHY WORDS
Au tena SHIHAN azungumzie -This Type of LOVE
Au tu Babyface arudishe kitu katika -I'll make love to you & end of the road
Tatizo la UBWABWA wa harusi, unahitaji uuvalie ULIMBWENDE na probulemu za UBWABWA wa MSIBANI , wahitaji staili za mkao wa MAJONZI!:-(
Kuna wengi watakao kuambia kuna kautamu tofauti kapatikanako kwenye pilau ya Msibani au Harusini ambako hakako kwenye pilau iliyopikwa kwa ajili yako nyumbani.
Afadhali hata na pilau ya kimada ambayo hata kama ni mbichi hutastukia kwa sababu ya kuharakisha kuila ili mvue nguo upate muda wakuwahi nyumbani bila kustukiwa.
Na wapo watakao kuambia hustukia MSIBA kutokana na harufu ya ubwabwa na sio KILIO kutokea kona ya sita.
Lakini ukitaka kustukia jinsi gani ubwabwa wa msibani au harusini unamvuto tofauti, mtafute aliyezamia msibani iliuone umahiri utumikao katika kuhakikisha pilau linanoga.
Ngojea nikupe kastori ka enzi za High School Mazengo DODOMA......
''Nisikufiche chakula kilikuwa kibaya ile mbaya pale shuleni mpaka ikifika siku ya ubwabwa ingawa ubwabwa wenyewe ulikuwa kama ugali , shughuli yake mesini lazima uistukie maana hakuna aliyetaka kumisi siku ya ubwabwa.
Halafu eti wajanja walikuwa wanaonekana wajanja kama wakipata mchuzi wa maharage wenye dalili za mafuta tuliokuwa tunauita TOP LAYER.
Basi bwana pale Mazengo kulikuwa na akina mama watuuziao , Vitumbua, maandazi na Chapati. Hawa walikuwa wanasababisha mpaka baadhi ya watu wale mpaka ada, ikiwa yote ni katika kukwepa kula chakula cha shule.
Na kwa bahati mbaya naweza kusema kwa uhakika kuwa kuna miezi ilikuwa inafika karibu kila mtu kachacha, na labda hata nauli shule ikifungwa hajui ataitoa wapi.
Kipindi hiki kili saidia kuwapa watu ujasiri wa kuzamia misiba na harusi kwa mafanikio.'' STORI yakijinga IMEISHA hapa .
AU ngojea nirudie!
Tatizo la UBWABWA wa harusi inabidi uuvalie suti na wamsibani uukalie mkao wa MAJONZI. Basi hapa ndio kazi ilipo katika shughuli nyeti ya kuzamia SHUGHULI!
Unaweza ukajikuta unalilia mtu mzima MSIBANI kumbe aliyefariki ni mtoto.
Afadhali ya kuzamia harusini unaweza ukaonyesha juhudi mpaka ndugu za mme wanafikiri wewe ni ndugu ya mke na ndugu ya mke wanafikiri kuwa wewe ni ndugu ya mme , kama sio tu pande zote wanadhani wewe ni A LONG LOST NDUGU, wakati wewe unasubiria mlo HUKU huachi kupiga chabo upande wa jikoni.
Halafu kuna staili za kula msibani kama unataka ubahatishe kukuta nyama kwenye pilau.
DONDOO ya jinsi ya kula UBWABWA msibani:
Safari ya mkono ya kwanza kwenda kwenye sinia ni yakutafuta nyama!
Ikiwezekana nenda na kachumbari yako kabisa kwenye mfuko wa rambo.
Kula haraka tu ukikumbuka kuna kitu kinaitwa baadaye kitakachokupa muda wakufikiria kuwa umeshiba au UMEVIMBIWA.
NJAA NISHAI kweli! Halafu nasikia eti WAAFRIKA tulitawaliwa na TUNATAWALIWA kwa sababu wengi wetu ni WAVIVU halafu tunasikia NJAA HARAKA!:-(
NAIKATISHIA hii stori hapa nikupe muda wa kwenda kujenga TAIFA. Swali:
Umestukia ilivyo noma nazungumzia maswala ya ubwabwa msibani na sio marehemu msibani?
Unauhakika marehemu huwa anakuwepo msibani?
Unauhakika msibani unamfikiria marehemu?
Unauhakika sababu zako za kwenda harusini sio kwa sababu ulilazimika tu kuchangia harusi wakati libwana harusi linakuudhi na bado harusini ninamcheki demu wako?
Kama umeoa au kuolewa lini utafuata fasheni mpya ya KUDIVOSI?
Tatizo la LEO ni kuwa huwa inakusanya mpaka na ya JANA.
Na ya leo yanaongeza utakayokutana nayo KESHO.
Hata kama umejifunza kutokana na ya JANA,..... ..... YAJANA yalishafanyika na yamekuingia mpaka KUMOYO hata kama huyafanyi leo na unafikiri yanapunguza uzito wa utakayofanya kesho.
Lakini bado LEO ni kiboko na inaweza kukuamulia ya KESHO.
Na kumbuka MZEE LEO alishawahi kuwa KIJANA.
Swali:
Hivi bado unaamini kuwa yakutokeayo leo ni MIPANGO ya MUNGU?
Kama unaamini katika mipango ya Mungu iliyokutokea leo , unauhakika si kwa mpango wa Mungu wewe utaenda JEHANAMU hivi karibuni?
Ni moja ya wazo tu USITISHIKE na kama umetishika TUBU shauri yako!:-(
Ngojea hawa WAMAREKANI watukumbushe SIASA YA UJAMAA kidogo...katika -Umoja - Unity
Au ngojea tu BOB RUDALA atongoze katika -NIMEKUCHAGUA WEWE