Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Baada ya KUKUMBUSHWA kuna wenye TABIA NZURI tu watu wengine WAKIWEPO

>> Monday, February 28, 2011

WATU wengine wasipo kuwepo,...
.... kuna wenye JUHUDI!

Na kama kuna WATU WAZURI pale tu wengine wakiwepo,...
.... bado ntatilia MASHAKA zihitajizo tu MASHAHIDI hizo JUHUDI!


Kwa kuwa WATU wana ya faragha pia -kwa hiyo twajua sio lazima  kila kitu  kifanyike watu wengine wakiwepo,...

.... ila inasikitisha kama MTU anabadilika kabisa TABIA kwa madhumuni tu ya kuficha MAKUCHA yake ya TABIA MBAYA kwa madhumuni tu  ya kufanya MABAYA ili asistukiwe na ili tu kuwe na MASHAHIDI watakao mtetea kuwa ni MTU MZURI  kwa JUHUDI!:-(


NIMESIMULIWA na MTU nimuheshimuye kuhusu MTU MWINGINE ni MHESHIMUYE ambaye ni MAMA WA KAMBO ambaye ananyanyasa MTOTO wa KAMBO wakati watu wengine HAWAPO na kujifanya ni MTU MZURI watu wengine wakiwepo!

BADO sijajua la kufanya na USHAHIDI sina na wakati NATAFAKARI HILO nikaamua kuandika tu  HILI hapa wakati najaribu kuamua la kufanya!:-(SAMAHANI bado mambo kibao yananizunguka KICHWANI kuhusu hili!:-(

BAADAYE!


Hebu FELA KUTI ajaribu kubadili filingsi kwa kujaribu kuchakachua hiihii MASANTULA ngoma ya mpwito-Gentleman

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 11:16 am  

Watu hawo wanavaa ngozi ya kondoo, kumbe ni mbwa mwitu, au sio mkuu!

SIMON KITURURU 11:22 am  

@M3: SI ndio hapooo! Halafu huyu ni rafiki yangu na kama ni kweli yani nishai kweli!

Si unajua mambo kama haya kuna marafiki ukiwaeleza watadai unaingilia mambo yao na urafiki ukaishia hapohapo! Lakini kuna mambo hata kama afanyaye ni rafiki nafikiria labda ni muhimu rafiki aambiwe hasa na rafiki yake!

Tatizo sina ushahidi na labda ndio maana nawaza kwa sauti hapa!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP