Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati tunakumbushwa Albert Einstein asifikaye kwa AKILI alikuwa sio mzuri DARASANI!

>> Tuesday, February 01, 2011

Shule muhimu,....

....hasa kama kuna KITU tunajifunza MASHULENI,...
.... kwa kuwa labda SHULE hazifanyikazi za SHULE,...
.... kama  kwa kwenda shule tunajifunza tu kutafsiri ELIMU  na kupata vyeti hata kama hatujifunzi kitu KIELIMU.:-(

SHULE ni muhimu,...
..... lakini labda inaweza kuchangia UJINGA wa watu  kwa kufanya walioenda shule kuwekewa wigo wa nini ni KUELIMIKA kwa kufanya watu kuamini kuelimika mipaka yake ni yale tu yafunzwayo MASHULENI yafanyao watu tuwenaushahidi mtu KAELIMIKA kwa kuwa kaenda shule wakati twajua kunatofauti ya kwenda shule na kuelimika KIELIMU!:-(


Swali:

  • Si unakumbuka labda wote uwasomao kwenye BIBLIA labda hawakwenda SHULE  kimatazamo wa ziitwazo shule siku hizi hata kama twajua baadhi walikuwa wanamuita YESU mwalimu?

Ndio,...
.... labda SHULE ni popote, YEYOTE na chochote,...
.... na kwangu WEWE lazima kuna kitu sijui  utakuwa tu KWANGU hatabila kujua ni MWALIMU!:-(

Na labda inabidi tukumbuke tu kuwa,...
.... bado cha muhimu ni tulichojifunza na SHULE tulizokwenda kukutana na WAALIMU.:-(




NAWAZA tu hapa MHESHIMIWA!



Hebu KHALED abadili wazo kwa-AICHA

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Unknown 11:20 am  

Tushikamane kuvuta kamba hii.

Simon Kitururu 5:11 pm  

SI utani MKUU kamba hii inahitaji nguvu za wengi kuvuta!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP