Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Na labda sio PATI HIYO kama PATI hiyo a.k.a SHEREHE HIYO hainyemelewi na wasioalikwa WAZAMIAJI wengine!:-(

>> Monday, February 21, 2011

Na labda ,...
...MKE sio  mzuri  HUYO kama hanyemelewi na MIDUME  mingine!
Na labda ,....
.....MUME hana mpangoHUYO  kama hanyemelewi angalau na BAADHI ya  wamuitao MKEWE rafiki ingawa kwenye urafiki wao wana MENGINE!:-(

Na labda,...
....... hata MUNGU wa MTU  bado ni wa UONGO HUYO  hata kama ananyemelewa na kukubalika na wengi  wengine!:-(
Na labda,...
....MTU bado anaroho mbaya HUYO  hata kama  hachukiwi na watu wengine!:-(

Swali:
  • Si unajua hapa DUNIANI wakati unashughulikia  LAKO bado kuna WENGINE na wenye MENGINE?

Ndio,...
....nilitaka tu tujaribu KUKUMBUKA,...
....kuna MENGINE na WENGINE wasiofanana na sisi na WASIOFANYA kama yetu  kwa kuwa ni WENGINE!:-(

Swali:
  • SI inakumbukwa labda kuna wenye matatizo kuliko SISI hata kama leo chamoto twakiona?


NI wazo tu hili BINGWA!:-(


Au ngojea Oumou Sangaré aanzishe mchepuo tofauti kwa - SeyaAu tu Oumou Sangaré amalizie tu akiwa na Boddhy Satva kwa mpekecho wa nguvu- ANH   DIYA

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 2:46 pm  

nanukuu "SI inakumbukwa labda kuna wenye matatizo kuliko SISI hata kama leo chamoto twakiona?" mwisho wa kunukuu. Kwa vile sisi binadamu huwa hatufikirii tatizo la mwingie ni kbwa kuliko lako. TUMEJAWA NA UBINAFSI.....

SIMON KITURURU 6:55 am  

@Yasinta wa NGONYANI: Mmmmh!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP