Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika MASHINDANO ya mtu na HAMU ZAKE za KUKATA tamaa!

>> Tuesday, February 22, 2011

WASHINDI hapa DUNIANI wengi wao yasemekana hushinda kwanza hamu zao za KUKATA tamaa,...

... kitu kifanyacho HAWAACHI kuhangaika na kitu hata kama KIGUMU na kwa kuendelea kuhangaika nacho  hupata suluhisho na mwishowe hupata demu kama safari hiyo lengo ilikuwa ni kuopoa BONGE LA demu - yote ikiwa MAISHANI kama moja ya kifanyikacho MAISHANI  kitu!:-(

Ndio kwa kukata tamaa,...
.... mtu HUACHA kitu.:-(

Na chochote MAISHANI  yasemekana kuna wakati  kina magumu  yake na kama MTU huna roho ngumu kama tu LIMUME la MTU lile sumbufu kwa MKE LAKE kinaweza  kukukatisha tamaa,...
... na ukikata tamaa kama yule MKE aliyekata tamaa kabla ya kupewa mimba asivyofanikiwa kupata mimba - ndio mwanzo wa KUTOFANIKISHA kitu.:-(




Na kwa bahati mbaya MENGI MAISHANI  hayafuati muda na RATIBA kama ile WATU waitegemeayo katika KUFANIKISHA yale waliyonayo kwenye TAMAA......
.... na labda ndio maana moja ya siri ya wengi  waliowahi kufanikiwa ya MAFANIKIO YA KITU ni kutokata tamaa hata kama mambo ni magumu katika kutimiza kitu.:-(

Swali:
  • Si unajua kuwa LABDA utafanikisha MENGI kama hautakuwa na MCHEZO wa KUACHA ufanyayo KIRAHISI kwa kuwa tu kuna kitu kimekukatisha TAMAA?

Ndio,...
.....LABDA tamaa ni kitu BOMBA katika kutengeneza mazingira ya MTU kiakili ya kufanya kitu CHOCHOTE KILE  hata kama ni mpaka kitu  kile tu cha BABA ya MTOTO naye kujaribu  kunyonya TITI la mke wake a.k.a MAMA WATOTO WAKE  wakati bado linatoa maziwa ambayo ni bonge la chakula cha mtoto wao ambaye saa hiyo anabadilishwa nepi BADO  na hausigeli baada ya kufanikiwa kujiharishia,...
.... kama tu MTU hata kata tamaa!:-(



Ndio,...
....ni wazo tu hili MHESHIMIWA na wala usikonde!:-(




Hebu Little Anthony na The Imperials waingizie kipengele - Going Out Of My Head.





Au tu Niggaz With Attitude warudie-Express Yourself

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 2:55 pm  

Mkuu nimerudi , tutakuwa pamoja sooon!

SIMON KITURURU 10:12 am  

@M3: Karibu tena Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP